Jamvi la Wanawake: Mabinti mmewafanya nini hawa wanaume huu mwaka, mbona wana hasira hivi?

Jamvi la Wanawake: Mabinti mmewafanya nini hawa wanaume huu mwaka, mbona wana hasira hivi?

My dear,wao ndo wana shida ndo maana wanalalamika😂😂😂. Mi nimeolewa, lakini niliolewa kwa kupenda si kwa sababu ya pressure ya umri wala jamii. Kuna watu walijaribu kunipressurize enzi hizo sijui ohho umri unaenda, waliongea wakachoka wakaacha.
Unamuuliza mtu anaolewa lini unataka mkaolewe wote au?😂😂😂. Mimi tena nilihakikisha nimejipata kiuchumi,nikaweka standards na vigezo vya juu mnoo, nikasubiri akapatikana aliyetimiza hivyo vigezo ndo nikamkabidhi moyo wangu. Nilikuwa tayari nife single kuliko kuwa na mtu asiye na vigezo navyotaka. Na nahimiza mabinti wajitafute kiuchumi na waweke vigezo vya juu,raise the bar ,na wasilegeze msimamo.
# Bora kufa single kuliko kuolewa na gumegume
Unapotosha wewe, kuwashauri wanawake waweke vigezo vya juu ni upotoshaji mkubwa Sana.

Shida yenu nyie wanawake huwa mnabase Sana kwenye kigezo cha pesa,yaani mwanamke akipata kaajira akaanza kupata vihela vyake anaona ndo amemaliza kila kitu sasa anataka mwanaume sijui mrefu,mweusi, handsome, wealthy and intelligent

It can never be.
 
mapenzi yasiyo na kichwa wala miguu ndio yapi? Kwani mapenzi yenye kichwa na miguu huanzaje? Sasa wewe umemtongoza mtu leo,amekukubali leo na anaomba 150k ya kodi inakuja kweli hiyo?
Kutongoza kukubali ndio nini kijana? ? ?
Samahani mimi nimezeeka inawezekana this is a generation gap problem! Uelezee.
 
nimemtongoza leo,amekubali leo tayari ameniomba 150K ya kodi,huoni kama kuna shida mahala? kuhusu mwanamke mmoja kuwakilisha jamii nzima ni huwa hivyo! malalamiko yamekuwa ni mengi kuwahusu hawa viumbe.
Kwahiyo mnashauri tufanyaje kutokana na hilo tatizo?
 
Unapotosha wewe, kuwashauri wanawake waweke vigezo vya juu ni upotoshaji mkubwa Sana.

Shida yenu nyie wanawake huwa mnabase Sana kwenye kigezo cha pesa,yaani mwanamke akipata kaajira akaanza kupata vihela vyake anaona ndo amemaliza kila kitu sasa anataka mwanaume sijui mrefu,mweusi, handsome, wealthy and intelligent

It can never be.
Kama unafikiri huyo dada kamaanisha hivi, unachelewa sana brazaa!!
 
Kiufupi hao walio nyuma ya hizo I'd hawana mbele wala nyuma.
Fact 💯
Mwanamke akifika third floor ndo kwanza anazidi kuwa mtamu, standard zake anazipanga vizuri hapindishi..,. Mwanamke wa 30 + ndiye anaye hongwa pesa nyingi kiuhalisia huku mtaani na ni hot cake kwa wanaume wenye ukwasi na wanaojitambua.
Msisitizo ni hapo kwenye wanaume wenye ukwasi na wanaojitambua.

Huwezi kukuta mwanaume wa aina hiyo anauliza mwanamke aliyempenda, akamtongoza na kutaka kuwa naye; eti “what do you bring to the table?” wewe kama umeona hana ambacho kina tija na cha kukufaa, unamfuata wa nini?
Hawa wa 20th wengi wao Bado hajajua Nini wanahitaji na ndio linakuwa kimbilio la wanaume wengi ambao hawaishi katika uaname kiuhalisia hao tuite wavulana. Wavulana hupenda haosasabu anaweza kumfanyia atakavyo
Fact 👆🏽
Binafsi haya malalamiko nikiyasoma huwa nasali vijana wangu wasiwe wa hovyo....
Mimi pia, nafundisha boys wangu kujitambua na kufocus kwenye kujenga future yenye mafanikio, wawe bora kwenye wanachofanya na wajiimarishe kiuchumi.
Pia wapo wanaoandika kutaka tension tu wengine wanaenda na trendy
Ila tu niwaambie huku kwenye jamii mambo ni tofauti na kelele za humu jukwaani
💯💯💯
 
Sasa Acha wanawake wadhubutu kufanya anachoshauri afu uone kitakachowakuta
Huyo dada haongelei physical appearence bro kuna wanaume wasingeoa ingekuwa hivi! Mrefu mweusi then what?? Kuna wanaume hawana huruma na mwanamke besides love, unatakiwa kujua unaishi na mtu wa aina gani! Upendo hauta last longer, miaka miwili mingi kuanza kugundua unaoshi na mnyama gani! huko ndoani ni pa moto sana! Unaishi na mtu ukimkosea kidogo tu kama umeua kwao! Akhaa😆🏃🏽‍♀️🏃🏽‍♀️
 
Back
Top Bottom