Janeth Magufuli akifurahi na wanafunzi nyumbani kwake Chato Machi 18, 2023

Janeth Magufuli akifurahi na wanafunzi nyumbani kwake Chato Machi 18, 2023

Hata mimi nimefarijika sana.
Wenye kumbeza na kumtukana JPM, watafanya hivyo kwa muda tu, lakini ukweli utabaki pale pale kwamba JPM alikuwa ni Rais mara 10 zaidi.

Uzuri ni kwamba, kila wakimbeza, kumtukana na kumdhihaki JPM, ndivyo wafuasi wake wengi zaidi wanavyoongezeka.
 
JPM ni alama ya pekee na ya thamani sana hapa Tanzania ambayo haiwezi kufutika kwa urahisi.

Yeyote atakayejaribu kuifuta alama hii, atafutwa yeye mwenyewe mara 10 zaidi.
 
Japo Kiswahili ni lugha yetu, lakini inaonekana wengi hawajui.

Neno kufariji limetumika pasipo mahali pake.

Kipindi cha msiba kiliisha.

Kipindi cha maombolezo kiliisha.

Anafarijiwa mfiwa.

Mjane, kama hajimudu, husaidiwa, hafarijiwi.

Kipindi cha msiba na maombolezo, mke wa marehemu huitwa mfiwa, na hivyo watu huenda kumfariji mfiwa.

Baada ya kipindi cha maombolezo kwisha, mke wa marehemu huitwa mjane. Mjane kama hajimudu husaidiwa na watu mbalimbali hasa wanafamilia. Na akitaka, kwa kuwa amemaliza kipindi cha maombolezo, anaweza hata kuolewa tena. Akiolewa tena, hawi mjane tena.

Hata biblia haisemi kwamba mjane anatakiwa kufarijiwa bali inasema kuwa kama mwanamke amefiwa na mumewe, na huyo mwanamke amefikisha miaka 60, basi huyo ni mjane kweli kweli. Anatakiwa kukumbukwa. Bado haielezwi kuwa anatakiwa kufarijiwa.

Baada ya kipindi cha maombolezo kwisha, watu wakienda kwenye kaburi la marehemu, ni ishara ya kumkumbuka marehemu, siyo kuwafariji waliokuwa wafiwa.

Ilitosha kuandika kuwa watoto walienda kumsalimia mjane au kuliona kaburi la marehemu.
 
Sio kwamba wewe ndio unatumia nguvu nyingi zaidi?
tena wapo kila nyuzi hawa Mabeberu na Vibaraka vyao.

Mada inazungumzia Watoto na Mjane wa Hayati. Wao wanaleta siasa. Mijitu mizima na nywele za masikioni. Karaha tupu. Very disgusting.

na ndio utaona wana leta za kuleta kama huyo mparamia nyuzi. Magaidi hayo.
 
JPM ni alama ya pekee na ya thamani sana hapa Tanzania ambayo haiwezi kufutika kwa urahisi.

Yeyote atakayejaribu kuifuta alama hii, atafutwa yeye mwenyewe mara 10 zaidi.
Afrika na Duniani.
Amebadilisha njia na namna za Uongozi ambao ulikuwa wa Kihafidhina na sheria na misingi ya wazungu....cha ajabu, na wao wameiga, wanaenda na mkumbo pamoja na kwamba wanajidai sio hivyo. Minafiki kweli.
 
Aache watoto wa watu wasome..

Huwez kuuwa watu ukabaki hata siku moja.
Nani alimuua? Yaani kuna mijitu mijinga ka wewe mnaendekeza propaganda za kipumbavu, ukute wewe ni li mtu lizima na fanya kazi la serikali linalipwa kodi zetu halafu linaamini ujinga. Acheni kumzushia Dkt Magufuli kwa sababu Mungu yeye hutenda kulingana na wakati, watanzania sasa wapo kwenye maombi makali sana ya kuliombea taifa hili na Mungu akilinde kiti cha Urais na kiendelee kukaliwa na mtu sahihi, so expect anything anytime. Mtu ka wewe hamfai katika jamii ni hasara kwa taifa.
 
Japo Kiswahili ni lugha yetu, lakini inaonekana wengi hawajui.

Neno kufariji limetumika pasipo mahali pake.

Kipindi cha msiba kiliisha.

Kipindi cha maombolezo kiliisha.

Anafarijiwa mfiwa.

Mjane, kama hajimudu, husaidiwa, hafarijiwi.

Kipindi cha msiba na maombolezo, mke wa marehemu huitwa mfiwa, na hivyo watu huenda kumfariji mfiwa.

Baada ya kipindi cha maombolezo kwisha, mke wa marehemu huitwa mjane. Mjane kama hajimudu husaidiwa na watu mbalimbali hasa wanafamilia. Na akitaka, kwa kuwa amemaliza kipindi cha maombolezo, anaweza hata kuolewa tena. Akiolewa tena, hawi mjane tena.

Hata biblia haisemi kwamba mjane anatakiwa kufarijiwa bali inasema kuwa kama mwanamke amefiwa na mumewe, na huyo mwanamke amefikisha miaka 60, basi huyo ni mjane kweli kweli. Anatakiwa kukumbukwa. Bado haielezwi kuwa anatakiwa kufarijiwa.

Baada ya kipindi cha maombolezo kwisha, watu wakienda kwenye kaburi la marehemu, ni ishara ya kumkumbuka marehemu, siyo kuwafariji waliokuwa wafiwa.

Ilitosha kuandika kuwa watoto walienda kumsalimia mjane au kuliona kaburi la marehemu.
Baibuli yenyewe imeandikwa na hao wasiojua maana halisi ya Lugha ya Mtanzania/ Mwafrika kuhusu 'Kufariji' ...... Kwa maoni yangu mkuu ...kutumia baibuli kuhalalisha au kuleta maana nyingine ya Vijana kuwepo katika mkusanyiko ule ni batili.

Mama wa watu hajapata kujifariji sembuse kuomboleza kwa amani kwa sababu ya Utumishi wa Mme wake kuwa Public. Mnafikiria hana watu wanaopita humu? Kama Mh. SSH? aidha kwa chawa [by proxy]wake ama kibinafsi hawezi kuona haya ya kuvuana sanda? Haya ya kufirigisa kaburi? etc... C' mon

Halafu kuna watu wanadiriki kusema ati amenenepa, amenawiri, seriously! Mtu anashindwa hata kutoka nje kwenye jua? Hata wana sayansi hawawezi kukubaliana na assesment ya hao Maharamia, magaidi ya mtandao. None. Hayo si maoni tu bali ni maoni yaliyojaa chuki na yamelengwa kutesa watu kisaikilojia. Stop this Non sense
 
Aache watoto wa watu wasome..

Huwez kuuwa watu ukabaki hata siku moja.
Usilete mantiki ambazo huwezi kushikilia. Chunga ndugu yangu chunga ulimi wako. Zipo serikali na watu wanaua watu kila siku duniani. Wengine wakiwa na usongo huwa wanapita mitaani....Be very careful.
 
Imekuwaje amenenepa ghafla?kweli alikuwa anateswa sana
 
Huu ni ukweli kwamba JPM ataenziwa vizazi na vizazi. Hawa watoto wadogo wanajua historia yake na wamepata hadi mwamko wa kwenda kumfariji Mama Janeth. Hakika Mungu si athumani.

View attachment 2561685

Nahisi katika watu waliofurahi kisirisiri kuondoka Magufuli mmojawapo ni Janeth.

Siku za nyuma, Janeth alipolazwa Muhimbili tuliwahi kuletewa ubuyu hapa JF kuwa kulazwa kule kulitokana na kipigo kutoka kwa bwana yule, nani anakumbuka hilo?
 
..familia ya Jpm inatakiwa kuwaomba radhi Watz waliotendewa UOVU wakati mtu wao akiwa madarakani.
Sawa sawa na Familia zote zilizohusishwa na Ukoloni.

Wacha Ugaidi. Kama una hoja weka hoja. Kufanya na kuendeleza ugaidi hautowasaidia kina Lissu Mbowe au CHADEMA pamoja na washika uzi. Puppeters Isitoshe haito kuongezea amani unayoitafuta kwa vijembe vyako. Muulize Lissu au Mbowe watakuambia. Sisi sote ni Binadamu...twaweza kujiondoa na kujipinda ufahamu lakini Mama wa Watu needs a Break.

Mkuu. Kaa na Amani.
 
Nahisi katika watu waliofurahi kisirisiri kuondoka Magufuli mmojawapo ni Janeth.

Siku za nyuma, Janeth alipolazwa Muhimbili tuliwahi kuletewa ubuyu hapa JF kuwa kulazwa kule kulitokana na kipigo kutoka kwa bwana yule, nani anakumbuka hilo?
Faiza, sidhani kama upo sahihi. Watu wengi, kuna nyakati hutofautiana, hufarakana na wenzi wao, na wengine kama ulivyonena (hisia), yaweza kutokea hata kupigwa na wenzi wao, hata hivyo ni nadra sana mafarakano hayo yanaweza kufikia mmojawapo kuona ni aheri huyo mwenzake aondoke Duniani. Labda kama uwepo wa huyo mwenzi mojawapo ni hatarisho kwa maisha ya mwenzake.

Siamini kama migogoro ya ndoa, hata kama ikiwepo, mwanandoa mmojawapo ataona aheri mwenzake aondoke Duniani.

Kutamka kuwa Janeth huenda alifurahia kuondoka kwa huyo mwenzi wake Duniani, ni kauli ambayo haistahili kutolewa na yeyote mwenye uzoefu wa maisha kama wewe. Kumbuka hawa watu wana watoto na ndugu, ambao wengi wao, watakuwa waliumizwa na kifo cha baba na ndugu yao. Watajisikiaje dhidi ya unayesema alifurahia, wakiamini hizi fikra zako?
 
Nahisi katika watu waliofurahi kisirisiri kuondoka Magufuli mmojawapo ni Janeth.

Siku za nyuma, Janeth alipolazwa Muhimbili tuliwahi kuletewa ubuyu hapa JF kuwa kulazwa kule kulitokana na kipigo kutoka kwa bwana yule, nani anakumbuka hilo?
Ni kweli hilo tukio lilifanyika Make Jesca ni mwanamke jasiri sana kuishi na dhalim miaka yote hiyo.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Sio kwamba wewe ndio unatumia nguvu nyingi zaidi?

Sijawahi kuanzisha uzi kuhusu JPM na sitokuja kuanzisha ila mkileta thread zenu za mchongo tutachangia kadri alivyojitengenezea hadithi yake(kulingana na matendo aliyoyafanya whether + or -).

Mnatumia nguvu sana kuaminisha umma kwamba alikuwa shujaa wakati hao mnaowaambia wameshuhudia utawala wake wote ebu msome Masese au Maloto wamemuelezea vizuri.
 
Back
Top Bottom