Jasmine Razack: Yanga wana Roho mbaya, wamegoma kumuuza Mzize, wanataka dola Million moja

Hiyo pesa inayowekwa kwenye clause ya kuuzwa siyo msahafu, inabadilika katika mazungumzo. Timu ikitokea kumtaka mchezaji ndiyo maana wanakaa mezani. Kawaida karibu mara zote huwa haifiki hiyo bei iliyowekwa katika mkataba. Si kila siku hizi timu zinasajili wachezaji na kuweka hiko kipengele cha dola milioni 1, niambie nani wamewahi kumuuza kwa bilioni 2.

Ni sawa na watu wanavyosajili makampuni BRELA, kwenye kiwango cha mtaji ni kama wanafanya copy and paste ila wengi wanakuwa hawana huo mtaji.

Mikataba ya wachezaji ipo hivyo hivyo. Wanaweka tu viwango vya kuvunja mkataba au kumuuza mchezaji bila tathmini ya kweli ya thamani ya mkataba inayoendana na malipo anayopewa mchezaji. Ni mazoea tu na wachezaji kutokuwa na nguvu mbele ya hivi vilabu kwa sababu ya njaa.

Niliposema hayo ya Aziz Ki nilikuwa namaanisha, hawa mashabiki maandazi huwa hata hawafanyi follow up kujua kile walichokuwa wanakipigania ndiyo kilichofanywa na viongozi wao ama la. Ni kama wanaona wanatimiza wajibu wao kutetea chochote ambacho kinaonekana ndiyo msimamo wa klabu. Ndiyo maana leo wanatetea hiki kisa unaonekana ni mtazamo wa viongozi wao, kesho viongozi wao wakibadilika nao wanabadilika. Bendera fuata upepo.
 
Reactions: Tsh
Ok mkuu, kwahiyo kwanza tukubaliane kimkataba kuna uwezekano Yanga wapo sahihi kabla hatujahamia kiubinadamu na kihuruma.
 
Ok mkuu, kwahiyo kwanza tukubaliane kimkataba kuna uwezekano Yanga wapo sahihi kabla hatujahamia kiubinadamu na kihuruma.
Siyo huruma au ubinadamu, Yanga kukataa kumuuza Mzize kwa bilioni 1.2 kuna harufu ya kukomoana au uswahili wa kubaniana rizki.

Mzize huyu huyu angeuzwa fasta kama ama angekuwa mchezaji wa kigeni au kama shida ni wakala wake, akiamua kumbadilisha. Hapo ndiyo utajua suala la vipengele sijui vya dola milioni 1 wala siyo ishu.

Ukitaka kujua hiyo siyo sababu kuu, angalia mambo mangapi wanayazusha katika hoja zao. Mara wakala hatambuliki, mara wanalinda maslahi ya mchezaji ili anapokwenda asikose nafasi ya kucheza, mara wao ndiyo wamemuibua toka mitaani, mara kina Bangala. Wakati huo huo wanasema huyu wakala anamuharibia Mzize, jiulize kivipi? Wanasema Yanga iache kufanya naye kazi, sasa kumuacha Mzize si ndiyo njia ya kuachana na huyo wakala?
 
Reactions: Tsh
Siyo huruma au ubinadamu, Yanga kukataa kumuuza Mzize kwa bilioni 1.2 kuna harufu ya kukomoana au uswahili wa kubaniana rizki.
Sasa huko kukomoana kupo kimkataba au la? Yaani Yanga wanamkomoa nje ya makubaliano ya mkataba?
Japo unasema vile vifungu si msaafu lakini ndo rejea pekee inayotumika panapotokea mgogoro hivyo ni jukumu la wakala kuhakikisha mchezaji habanwi sana na vifungu. Sasa kama wewe uliyeusimamia mkataba usainiwe na ukapata na ka% kako ndo unalia tena kuwa mchezaji anaonewa na husemi kama mkataba umekiukwa moja kwa moja unaonekana unajanja janja.
 
Ni kukomoana kwa sababu kama nilivyosema mchezaji mwenye quality hii hii ya Mzize wangemuuza kama hayo mambo mawili niliyotaja yasingekuwepo. Kiwango cha mauzo kilichopo kwenye mkataba siyo sababu kwa sababu kama nilivyosema hiko kiwango huwa kinazungumzika na isingekuwa unaoonekana ni msimamo wa viongozi wa Yanga wengi wangesema hiko ni kiwango kizuri sana kwa mchezaji kama Mzize.

Hili wimbi la sasa ni la kufuata upepo tu na kutimiza wanaodhani ni wajibu wao. Ukitaka kujua hilo, rudi kasome comments za hawa hawa Yanga wakati hizi fununu zilipoanza. Wengi waliunga mkono wakawa wanasema Yanga ifanye biashara. Wamekuja kubadilika baada ya kuona viongozi wao wametia ngumu.
 
Reactions: Tsh
Wewe una akili sana nyingi sana unaelewa tunachomaanisha kabisa bravo sana
 
Reactions: Tsh
Mkuu kwa heshima yako naomba uishie hapa huyo mwenzio sijui ana uelewa gani? Mbishi kweli kweli yaani
 
Reactions: Tsh
Ila we jamaa utakuwa muha wewe sio bure

Hadi huyo Tsh Namfahamu ni simba kindakindaki kabisa lakini hajitoi ufahamu kama wewe elewa tunachomaanisha anakuelewesha ilivyo haegemei popote kama wewe unataka auzwe hivi hivi tu mkataba aliosaini buy clause yake ikoje??

Sio swala kuuza tu basi bali mkataba ukoje?? Kama wanaweza wanaweza ununua mkataba basi kama DUBE pale azam shida nini? Hakuna mkataba usiovunjika ila tu vipengele vyake ukiufuata
 
Mkuu, bado hujajibu lakini iwapo huko kukomoa kupo kimkataba au la.

Mfano, umesaini mkataba na mimi kuwa Simba ikishinda utaweka hadharani majina yako ma3 na picha yako na kulipa kila mwanaJF elfu moja, na mimi nikasema Simba ikifungwa ntakupa elfu kumi na tukitaka mkataba uvunjike kabla ya kuisha mechi anayevunja atalipa Milioni. Ni dk ya 70, Simba inaelekea kufungwa. Ukija kwangu ukasema unataka unipe elfu kumi tuvunje mkataba kiubinadamu ni suala linalozungumzika na naweza kukubali, ila nikisema hapana ili nikukomoe, mkataba unakufunga na mimi nakuwa sijakukomoa nje ya mkataba maana tulikubaliana kwa maandishi.

Ndo maana nakuuliza, huko kumkomoa Mzize kupo kimkataba au la?
 
Sasa huko kukomoana kupo kimkataba au la? Yaani Yanga wanamkomoa nje ya makubaliano ya mkataba?
🤣🤣🤣dah una maswali makali sana mzee huyu hajibu hili atakwepa tu
 
Mkuu kwa heshima yako naomba uishie hapa huyo mwenzio sijui ana uelewa gani? Mbishi kweli kweli yaani
Hahaha, itakuwa anachangamsha kijiwe tu sio kwamba kweli haelewi. Si unajua ubishi wetu wa utani wa jadi tukiamua hatukosi majibu.
 
Natumia neno kukomoa kwa sababu mazingira ya yanayoendelea yanaonyesha hivyo. Mzize siyo mchezaji wa kukataa kumuuza kwa bilioni 1.2 bwana.

Na hapo wanasema wanalinda maslahi yake wakati huko anapotakiwa wanamuahidi mshahara mara 3 ya anayolipwa sasa. Yaani wamejivika majukumu ya wakala na meneja wa mchezaji wakati huo huo wako vitani na wakala wake halali. Haihitaji akili kubwa kuona ukomoaji na kuzibiana rizki unaofanyika.
 
Tatizo lenu ndiyo hilo. Mkipingwa, mnadhani ni kwa sababu ya Usimba na Uyanga. Mimi nikiona upuuzi unafanyika siunyamazii. Simba wenyewe nimewakosoa mara ngapi na hata sasa nimejipa likizo ya kutoishabikia.

Yaani umeungwa mkono na mwanasimba, ushajiona umeshinda jackpot.
 
Hahaha, itakuwa anachangamsha kijiwe tu sio kwamba kweli haelewi. Si unajua ubishi wetu wa utani wa jadi tukiamua hatukosi majibu.
Hata kama anachangamsha lakini sio namna hii tangu muda sana anaongea vitu havieleweki hata maswali uliyomuuliza hajajibu anakwepa kwepa yaani ilimradi aonekane na yeye yupo tu

Mimi ni yanga unajua wazi ila sometimes kwenye mambo yaliyo wazi hakuna haja ya kupindisha kwa hili jambo mfano ila huyu analeta mambo ya kina kisugu vijiweni

Hahaha, Sijawahi sifiwa na mwana Yanga mkuu. Hii itaingia kwenye kumbukumbu.
Mpira sio vita wala nini lakini leo Umenyooka sana kuna sehemu umenikosoa na mimi wala sikukataa nikakubali ila huyu mwamba sasa 🤣
 
Reactions: Tsh
Sio huyo tu watu wangapi wamskurekebisha hapa lakini bado unakaza fuvu??? Hebu sema mwenyewe naona tukupe kombe sasa baki nalo

Kombe la ubishi wa vijiweni
 
PASADENA nadhani unaona kwanini yanga wanataka pesa nzuri kumuuza mzize kupitia mechi ya leo umepata assignment nzuri

Watu wamewekeza pale na mkataba utafuatwa tu utake usitake na Jasmine atake asitake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…