Jasmine Razack: Yanga wana Roho mbaya, wamegoma kumuuza Mzize, wanataka dola Million moja

Kuna pande mbili za mkataba wakati wa mauzo ya mchezaji. Kazi ya wakala wa mchezaji ni kuhakikisha dili linalofanyika lina maslahi mazuri kwa mchezaji kwa upande wa mshahara na marupurupu mengine. Nadhani ndiyo anachokifanya hapa.
Huyo ni dalali anauwakala gani huyo
 
Natumia neno kukomoa kwa sababu mazingira ya yanayoendelea yanaonyesha hivyo. Mzize siyo mchezaji wa kukataa kumuuza kwa bilioni 1.2 bwana.
Mkuu, Mzize angesaini mkataba halafu hapo hapo akavunjika kisha msemaji wa Yanga akasema Mzize anatukomoa maana amesaini tu afu akavunjika, hatumpi mshahara hadi apone ungekuwa na maoni gani?.

Kama Mkataba unasema atalipwa mshahara hata akiwa majeruhi basi hata kama Mzize anawakomoa huko kukomoana kupo kimkataba kama Yanga hawataki kukomoleka watavunja huo mkataba kulingana na vifungu vya termination. Ndivyo ilivyo kwa upande wa Mzize.
 
Sio huyo tu watu wangapi wamskurekebisha hapa lakini bado unakaza fuvu??? Hebu sema mwenyewe naona tukupe kombe sasa baki nalo

Kombe la ubishi wa vijiweni
Acheni uswahili na roho mbaya. Wachezaji wa kigeni wanafaidika ila wa kibongo tunachukuliana poa na kuzibiana rizki kwa sababu ya roho mbaya. Huyo Mzize mngekuwa kweli mna nia njema naye, mngemuachia. Sijaanza kumtetea leo na simjui wala hanijui na sina maswahi yoyote kwa yeye kubaki wala kuondoka hapo Yanga. Nimewahi kuleta hata uzi humu ukimwambia aache ujinga, achangamkie fursa.

Uswahili wetu wa kuambiana na kutishana kuwa "kuna kesho" na "kuna kufeli" ni roho mbaya tu iliyopo ndani ya Watanzania.
 
Uswahili wetu wa kuambiana na kutishana kuwa "kuna kesho" na "kuna kufeli" ni roho mbaya tu iliyopo ndani ya Watanzania.
🤣🤣haya yametoka wapi?? Mkuu Tsh Mchukue ndugu yako huyu akalale ameshalewa
 
Haya mambo yashanchosha, embu niongee na demu wangu aniliwaze. Msimamo wangu unabaki pale pale, Yanga wana visirani na roho mbaya mno.

Akili, tabia na fikra za tabaka linaposhabikia Yanga zingefutika, nchi hii ingesonga mbele kwa kasi. Ni tabaka fulani la hovyo sana, haujui tu.
 
Reactions: Tsh
PASADENA nadhani unaona kwanini yanga wanataka pesa nzuri kumuuza mzize kupitia mechi ya leo umepata assignment nzuri

Watu wamewekeza pale na mkataba utafuatwa tu utake usitake na Jasmine atake asitake
Mzize ni mchezaji wa nafasi 6 anakupa 1 au 2 na nyingi ya nafasi anazopata, goli analiona liko angani. Mnataka kuuzia waarabu mbuzi kwenye gunia. Hapo bado suala la umri linabaki siri yetu kama wazalendo.
 
Mzize ni mchezaji wa nafasi 6 anakupa 1 au 2 na nyingi ya nafasi anazopata, goli analiona liko angani
Kwa kweli unahitaji upelekwe kwa pastor kapola ukajazwe hewa kichwani kama mitungi yake ya gesi sasa mkuu
 
Kwa kweli unahitaji upelekwe kwa pastor kapola ukajazwe hewa kichwani kama mitungi yake ya gesi sasa mkuu
Hakuna mchezaji wa bilioni 2.5 pale acheni kudanganyana. Nyie wenyewe mnajua hilo mnakaza tu fuvu kutimiza wajibu wenu wa kutetea viongozi wenu.
 
Duh mkuu kumbe ndiyo maana jamaa sikuhizi yeye yanga hata iweje lazima awapopoe tu .

Inaonekana ni mtu wa majungu tu yaani

Halafu yeye na Haji haziivi kabisa kabisa wale
Kuhusu gadiel kusaini simba meneja asijue kweli jemedari alizingua sana hapo
 
Hahaha, usiku mwema mkuu. Sasa huyo usije bishana nae usiku mzima. Muite kabisa umalizane nae. Mwanamke usiongee nae sana.
 
Hiyo 70M kwa wiki ama mwezi?
Jasmine anatapa tapa,timu ya qatar ilifika pesa wanayoitaka Yanga,jasmine na genge wakawa wanataka mshahara wa mln 70 hadi ile deal ikabuma,sasa hivi kwa ujinga wake anataka lawama aibebeshe Yanga
 
Kwa kweli unahitaji upelekwe kwa pastor kapola ukajazwe hewa kichwani kama mitungi yake ya gesi sasa mkuu
Kingine kabla sijakuacha, Aziz Ki huko alipo amekuwa tayari hata kukatwa mshahara ili tu asirudi Yanga na hapo ametoka kucheza dakika 6 kwenye Club World Cup yote. Nyie mko hapa mnajazana ujinga eti mnatetea maslahi ya mchezaji. Roho mbaya tu.
 
Jasmine anatapa tapa,timu ya qatar ilifika pesa wanayoitaka Yanga,jasmine na genge wakawa wanataka mshahara wa mln 70 hadi ile deal ikabuma,sasa hivi kwa ujinga wake anataka lawama aibebeshe Yanga
Al Sadd Fc ya Qatar iliweka mezani 2.2B kwa Yanga, kumbe walikuja kushindwana na menejiment ya Mzize sababu ya kutaka mshahara mkubwa hivi eeh
 
Kwani nani anapanga bei ya mchezaji??
 
Mashabiki wa Yanga mtaacha ujinga lini? Huyo dada "hajajitokeza" na siyo dalali. Hiyo ni msimamizi rasmi wa Mzize anayetambulika na mamlaka zote za soka na hadi familia yake. Ni jukumu lake kulinda na kutetea maslahi ya mteja wake.
Msimamizi yaani supervisor au?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…