Jasmine Razack: Yanga wana Roho mbaya, wamegoma kumuuza Mzize, wanataka dola Million moja

Huyu huyu Jasmine hata kwa mayele alianza chokochoko hivi hivi na sasa hata kwa Feisal akaja hivyo hivyo mbona sasa Feisal kule azam katulia mbona halalalamiki kuwa mchezaji wake Feisal amenyimwa na azam ofa ya kwenda simba? Mbona Hasemi azam wana roho mbaya??

Huyu mama ni kirusi na ana tamaa kubwa sana atampeleka kijana shimoni,

Yanga imemtengeneza mzize kuwa aliyepo leo hii na amepata exposure akiwa na yanga!

Tate Mkuu
vibertz mnasemaje?
 
Wewe mwenyewe hujui chochote kuhusu uwakala na Biashara ya Soka kwa upabde wa Wachezaji.

Na kama Yanga imemkuza Mzize na wamemjengea Brand, si wamuuze huko Kuwait? Wanasubiri nini?
 
Yanga inabidi waache kufanya kazi na huyu Jasmine, ndio maana FIFA waliweka utaratibu wa jinsi ya kuwa wakala, walijua kutakuwa na fujo kama hizi. Tz nzima kuna wakala mmoja tu anaye julikana na FIFA baada ya kufaulu mtihani wao,wengine wanaungaunga tu.

Mpira biashara kila timu ina target zake kwa mchezaji wake.Man Utd kuna kipindi walikuwa wanapata tabu sana na Mino Raiola mpaka wakatishia kutokuja kufanya nae kazi tena, wachane nae na ikiwezekana wasichukue mchezaji yoyote kutoka kwake.
 
Uyo mama yanga wameamua kumpuuza tu ndio maana viongozi wameamua kumfungia vioo,,yeye anachokiangalia ni 10% yake aingize mfukoni basi ajui klabu Ina malengo Gani baada ya kumtengeneza uyo mzize
 
Wewe mwenyewe hujui chochote kuhusu uwakala na Biashara ya Soka kwa upabde wa Wachezaji.

Na kama Yanga imemkuza Mzize na wamemjengea Brand, si wamuuze huko Kuwait? Wanasubiri nini?
Nilichokupa ni ukweli wala sibahatishi sawa?

Tunachosubiri CHAN iishe ndiyo biashara ifanyike

Kwa akili ya kawaida tu wewe unanunua bidhaa dukani kwako.kwa buku unaiuza buku 200 una akili kweli wewe?

Na wakati huo huo kuna soko la kuiuza kwa 2000 utachqgua wapi?

Yanga wamemtengeneza mzize ndiyo unabisha??
 
Hilo ndio muhimu waache kufanya kazi na huyu mama anachoangalia ni tamaa yake binafsi hapo al masry kuna mgao mkubwa kaupangia tayari ukute sawa na mzize kabisa

Mchezaji ana mkataba bado alisaini miaka mitatu means bado ni Mali ya yanga yeye anataka mambo yaende anavyotaka tu

Eti anakuja mchezaji wangu ana ofa nataka kuvunja mkataba!

Kirahisi tu?
 
Uyo mama yanga wameamua kumpuuza tu ndio maana viongozi wameamua kumfungia vioo,,yeye anachokiangalia ni 10% yake aingize mfukoni basi ajui klabu Ina malengo Gani baada ya kumtengeneza uyo mzize
Na hana sifa za kuwa wakala

Unaambiwa kwenye list ya mawakala wanaotambuliwa na FIFA yeye hayupo na hatambuliki .

Anataka yanga wamuuze mzize kama nyanya tu sokoni eti mchezaji wangu nataka tuvunje mkataba aende al masry

Yaani hajui biashara mzize amepewa mkataba wa miaka mitatu wakati wengi wamepewa miwili miwili tu means ana umuhimu kwa yanga !

Zaidi yanga pia wanataka kumuuza mzize ila ofa ndio kigezo muhimu biashara inaendeshwa kwa faida Kuwait ni bora kuliko Egypt
 
Jasmine anatapa tapa,timu ya qatar ilifika pesa wanayoitaka Yanga,jasmine na genge wakawa wanataka mshahara wa mln 70 hadi ile deal ikabuma,sasa hivi kwa ujinga wake anataka lawama aibebeshe Yanga
 
Mashabiki wa Yanga mtaacha ujinga lini? Huyo dada "hajajitokeza" na siyo dalali. Hiyo ni msimamizi rasmi wa Mzize anayetambulika na mamlaka zote za soka na hadi familia yake. Ni jukumu lake kulinda na kutetea maslahi ya mteja wake.
 
Jasmine anatapa tapa,timu ya qatar ilifika pesa wanayoitaka Yanga,jasmine na genge wakawa wanataka mshahara wa mln 70 hadi ile deal ikabuma,sasa hivi kwa ujinga wake anataka lawama aibebeshe Yanga
Kiufupi tamaa ilikuwa kubwa sana kwake na sasa natafuta huruma tena ila this time atabugi sana

Yeye ndiyo anamuharibia kijana kipaji chake kwa tamaa zake binafsi nadhani hata leo hii ukiwauliza wazazi wa mzize watakwambia mchango wa yanga kwa mzize na sio huyo jasmine muongo muongo sana mbona?

Na sasa anataka kumpeleka mzize popote apate hela yoyote ile sasa yanga na al masry wapi kuna future zaidi ya mzize mwenyewe kucheza?
 
Jasmine ni tapeli ambaye uwadaka wachezaji juu kwa juu
Na anadai yeye eti ndiyo alimtengeneza mzize!

Muongo mkubwa sana kwahiyo na mayele pia atadai alimleta yanga yeye kumbe alimdakia hapa hapa bongo tu

Dalali tu huyu kama kina jemedari
 
Mwisho ni kuwa al masry wametuma ofa ya Dola 70000

Na yanga wanataka kwanzia 100000

Huku klabu moja kutoka uarabuni Kuwait imetuma ofa ya 90000 dollar

70k, 90k na 100k. Hela ndogo sana au umekosea?
 
Huyu wakala Yanga lazima wakatae kufanya nae kazi watamfanyia zengwe mpaka basi,, ila pia maneno ya wakala hayajakaa poa sip profeshino na ni mbaya kwa carrier ya mchezaji.
Tayari hili wanalofanya ni zengwe. Hapo wanataka Mzize aachane na huyo wakala wake halafu utaona jinsi dili litakavyokwenda fasta na wanaweza kumuachia hata bure. Yale yale ya Aziz Ki hawakutaka kumuuza kisa kocha. Hawa ni watu wa visirani na visasi.
 
Huyo mdada anaonekana ni kichomi na anaonekana ni wakala mwenye mashinikizo ya kipuuzi na asiye heshimu mikataba ya timu na wachezaji wake! Yeye anachotaka ni biashara kufanyika muda wowote ule ili apate 10% yake! Hata kama timu inaona hiyo ofa haina faida kwao ukilinganisha na thamani ya mchezaji.

Inashangaza kuona anaichafua Yanga kwenye vyombo vya habari, na wakati ina mkataba halali na Mzize! Yeye kama wakala hana mamlaka ya kuipangia Yanga kumuuza mchezaji wake, isipokuwa ni Yanga yenyewe ndiyo inayotakiwa kukaa mezani na mchezaji kama kuna ofa yenye maslahi ipo mezani!
Aachane na mashinikizo yake ya kipuuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…