Jasmine Razack: Yanga wana Roho mbaya, wamegoma kumuuza Mzize, wanataka dola Million moja

15 kwa mwezi au ? kube walikuwa wanamlipa 2 million ila sie watanzania tunauana maskini sana
Hata hio 15 ni ndogo sana sema basi tu at least hamna hamna angekunja hata 40 hivi au 50 /Mwezi angalau angalau kidogo
 
Wabongo wengi linapokuja swala la mikataba wanaanza kuililia serikali. Mazoea ya longolongo yametuharibu sana. Dunia imebadilika, soma maandishi kwa makini kabla hujamwaga wino.
Njaa inauma sana nitasomaje na huku njaa inauma mkuu sijabeba mihogo yangu, nimekuja kusaini mkataba unaniweka na njaa kuanzia saa 12 asubuhi mpaka 11 jioni sijala kitu kisha unanipa mkataba mimi si ninaangalia namba tu pale zinasomaje ili nipooze njaa muda huo unanipa mkataba unaniambia ukishasaini tu msosi ule pale mezani nenda kale ila kabla hujala saini kwanza mkataba
 
Kuna pande mbili za mkataba wakati wa mauzo ya mchezaji. Kazi ya wakala wa mchezaji ni kuhakikisha dili linalofanyika lina maslahi mazuri kwa mchezaji kwa upande wa mshahara na marupurupu mengine. Nadhani ndiyo anachokifanya hapa.
 
Kama kuna timu imetoa ofa ya $900k meneja wa mzize asingeelezea ofa ya 600k, angezungumzia ya 900k.
Ofa pekee iliyopelekwa wa Wakala wa Mzize ilikuwa ni hiyo ya Al Masry. Hawezi kuongelea ofa ambayo haijaletwa.
 
Hapo anazunguka tu kuichafua team eti anatafuta huruma kuwa kijana anategemewa na familia yake .

Kwani ndio anajua sasa? Mzize mwenyewe ana furaha kuwa yanga shida sio kumuuza shida ni ofa nzuri kama unavyosema mkuu ila huyo mama sijui anatumwa na nani? Kila mara anawachokoza yanga sasa safari hii ataona mwenyewe
 
Huenda Mzize mwenyewe ndiye anayelalamika sio Jasmine.

Ukiona wakala anaongea sana tambua mchezaji ameshaanza kulalamika kwa wakala wake.
 
Huenda Mzize mwenyewe ndiye anayelalamika sio Jasmine.

Ukiona wakala anaongea sana tambua mchezaji ameshaanza kulalamika kwa wakala wake.
Hapana Mzize hana mambo hayo na anafurahia sana kucheza soka lake.

Huyu mama ndiyo kichomi hapo anapiga hesabu ndefu za kuingiza pesa yake bila kujali mchezaji wake anakokwenda kuna future yoyote kwa carrier yake ya soka?

Au ndiyo msimu mmoja kisha arudi bongo?

Huyu sio wakala ni muharibifu tu bongo wakala ni mmoja tu anayetambuliwa na FIFA sio hawa madalali

Hapo ataanza kumjaza mchezaji sumu mpaka basi
 
Jasmine mhuni na tapeli tu, hafai hata kuwa wakala wa mchezaji yeyote
Ukimsikiliza ti utajua kuwa pale ni tapeli tu hakuna kitu

Ifike wakati iwe mwanzo na mwisho yanga kuwa na wachezaji wa huyo mama
 
Tayari hili wanalofanya ni zengwe. Hapo wanataka Mzize aachane na huyo wakala wake halafu utaona jinsi dili litakavyokwenda fasta na wanaweza kumuachia hata bure. Yale yale ya Aziz Ki hawakutaka kumuuza kisa kocha. Hawa ni watu wa visirani na visasi.
Aisee
 
Kwahyo yeye anajali biashara yake lakini ya wengine wakijali zao wanaroho mbaya?

Tanzania wajinga bado wengi sana, subiri nkajaze zangu mtungi kwa pastor
Huyo Jamaa kama mngese 😂😂

Yaani Mitanzania sijui ikoje imagine watu wakulishe wakuvishe wakutengenezee branding name kubwa halafu wanapo hotaji fidia Yao unawasema kuwa Wana roho mbaya really!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…