Je, dini ni upendo au ni chuki? Vita na mauaji yaliyokithiri

Wayahudi wanaua kina nani
Vyote vipatinavyo juu ya ardhi pasipo kuacha hata kimoja hai. Je haya maagizo hawa kupewa wayahudi na huyo Mungu kutekeleza ?
 
Vyote vipatinavyo juu ya ardhi pasipo kuacha hata kimoja hai. Je haya maagizo hawa kupewa wayahudi na huyo Mungu kutekeleza ?
Kama kaagiza kuua asingewapa amri kumi usie.
Amri kumi zote zinahimiza upendo.Zimegawanyika fungu mbili juu ya mwanadamu kumpenda Mungu na zilizobaki ni maagizo ya mwanadamu kumpenda mwanadamu mwenzake.
SAsa uoni dini ni upendo hapo
 
Kama kaagiza kuua asingewapa amri kumi usie.
Amri kumi zote zinahimiza upendo.Zimegawanyika fungu mbili juu ya mwanadamu kumpenda Mungu na zilizobaki ni maagizo ya mwanadamu kumpenda mwanadamu mwenzake.
SAsa uoni dini ni upendo hapo
Ni upendo upi wa kufyeka vichwa vya watu kwako huo ni upendo ?
 
Unaitazama dini in negative way.
Hakuna dini inayoamrisha mabaya
Sawa ndugu asante kwa muda ulio nipatia.

hatutafika muafaka kama tuna badilisha nyeusi kuwa nyeupe ili tu kufurahisha mioyo yetu kutokana na pande tulizopo.
 
Dini haifundishi mabaya
Mkuu nimefuatilia uko active kweli ila ngoja nikupe hoja...

Yapo madhehebu ambayo ukiingia tu wanataka ujitenge na watu wa madhehebu mengine, hata kama ni ndugu zako,

Pia inatakiwa utambue kuwa kuna watu hawana dini na wanayaishi maadili kuliko wenye dini, biblia ni kitabu kama vitabu vingine
 
Duh muogope hata Mungu...kwanini udanganye kiasi hiki?
 
Ishu ya maadili imekuwpo kwa mwanadamu hata kabla ya ujio wa dini.Mfano hata kabla ya ujio wa dini waafrika waliishi kimaadili.Dini na maadili ni kitu kimoja.
Mtu kuwa na dini na kuishi nje ya maadili hapo shida ni mtu na sio dini.Feki haiwezi kuwa original.
Chochote kile kifanywacho na mwanadini nje ya muongozo wa dini shida sio dini bali ni mtu.
Thus kuna Mkatoliki na mkatoroka, mpentekoste na mpendakote.
Means Mkatoroka, mpendakote hawa ni Wana dini lakini matendo yao sio ya dini yaani kwa Mungu wapo na kwa shetani wapo.Mfano mtu akiua kupitia dini hali dini hio hio inaamuru usiue shida ni mtu na sio dini.
 
Madhara ya watu kuacha dini ni makubwa Sana kwenye Jamii, tutapata kizazi kisichojua jua kutenganisha mabaya na mema. Kupata Jamii isiyo na maadili,Jamii isiyo na maadili utoa viongozi wabovu.
 
Kwahyo kipindi wana wa israel wanaenda kuua vijiji na kuchinja watoto ilikuwa sio maagizo ya mungu?
KWA wakati ule na KWA kusudio lile ambalo halikuwa endelevu.
Kumbuka hakuna mwanadamu yeyeto mwenye kuweza kutoa uhai wa Mwanadamu yeyeto pasipo Mungu kuruhusu. Hata mchawi hauwi mtu bali umficha mtu yaani kumuhamishia ulimwengu mwingine.
 
MUNGU ni pendo upenda wote thus utoa baraka kwa wema na waovu. Unyesha mvua kwa wema na waovu,
 
Dini zote ziliua zote zilitesa kwa kutumia Jina LA Mungu. They can't now try to separate eti kuwa yalikuwa maamuzi Yao binafsi........ DINI NI kazi ya mwanadamu. So cha mwanadamu lazima kina MAKOSA NA MAKOROKORO KIBAO
 
Dini zote ziliua zote zilitesa kwa kutumia Jina LA Mungu. They can't now try to separate eti kuwa yalikuwa maamuzi Yao binafsi........ DINI NI kazi ya mwanadamu. So cha mwanadamu lazima kina MAKOSA NA MAKOROKORO KIBAO
Hata shetani upotosha watu kupitia dini
 
Ktk waleta mada za kukosoa dini wote angalau wewe umefanya ‘Homework’ yako.


Ongezea ‘Baltic Crusades’

Lakini pia kuna
Trojan war 1194-1184 BC
Greco-Persian war 499-448 BC
Paleponessian war 460-445, 431-404 BC
Corinthrian war 395-387 BC
Punic wars 264-146 BC

Vita zote hapo juu zimepiganwa si Yesu wala Muhammad (PBUH) aliyekuwa amezaliwa.


Majimaji war 1905-07
Algeria war of independence 1954-62
Kagera war 1967-69
Ukraine war 2022-
Chinese civil war 1945-49
WWI 1914-18
WWII 1939-45

Hii ni baada ya wote Yesu na Muhammad (PBUH) kuishi na kufa lakini sababu za vita hapo juu haikuhusisha dini yoyote ile na orodha ni ndefu sana siwezi andika yote hapa.

Hii inatokea pale wanaodai wanafuata dini fulani (hizo tatu ulizotaja) hawafuati kikamilifu.
Maana ya dini ni; Dini ni mfumo wa maisha ya wanaadamu, kwa maneno mengine ni muenendo mzima wa maisha ya mwanaadamu ndiyo dini.

Dini hizi ktk ile hali ya uhalisi wake kama alivyokuja nayo Mussa (AS), Yesu(AS) na Muhammad (PBUH) hazina shida kabisa na zilikua ktk misingi na lengo lake.
2. Kwa nini hizi dini zina imba wimbo wa amani huku zikiwa zimeshika mapanga?
Dini ktk uhalisi wake hakuna kushika mapanga, haya mapanga ya akina Anti Baraka, Al Qaeda, Alshabaab, Lord Resistance Army na wenzao wako kinyume kabisa na mafundisho ya dini zote tatu.

Mathalani, Uislam unahalalisha vita endapo moja ya sababu ya kuingia vitani ni pale ambapo jamii itapokonywa ardhi yake, na hata katika vita hivyo kuna sheria za kufuatwa ikiemo kutokata miti bila sababu, kutoua watoto, wanawake, wazee wala walemavu na hata wakishinda vita basi ni dhambi kulazimisha maadui wao kusilimu wala kubomoa makanisa na masinagogi wala kuua wachungaji, marabi na watumishi wa dini.

3. Kwa nini hizi dini zina endekeza ubaguzi, chuki, masengenyo na uharibifu mkubwa kwa wale wasio wa amini ?
Dini hizo zote zinahimiza upendo na ushirikiano baina ya watu wa imani tofauti.

Mathalan ukristo unahimiza watu kuwapenda majirani zao kama wanavyozipenda nafsi zao.

Uislam pia unahimiza kuwatendea wema majirani, na tafsiri ya ujirani ni nyumba arobaini toka nyumbani kwako hao wote wanahesabika kuwa ni majirani.

Uislam unaruhusu Muislam kumuoa Mkristo.

Uislam unaruhusu Muislam kula nyama ya mnyama aliyechinjwa na Myahudi ama Mkristo (sharti mchinjaji awe amemtaja mungu mmoja wakati wa kuchinja)

Kwahiyo Mafundisho ya dini hizi tatu hayafundishi chuki, ubaguzi wala uharibifu wowote bali kinyume chake.

4. Je hizi dini zina abudu Mungu wa upendo au zina abudu Mungu wa Vita, chuki, visasi, ubaguzi na masengenyo ?
Mafundisho ya dini hizi zote yanafundisha Mungu wa upendo.

5. Je hizi dini zime shindwa kustaarabika ?
Hapana, kimsing jamii unayoiona hii leo ni matokeo ya wao kwenda makanisani na Misikitini, unadhani zimeharibika? Basi jaribu kuondoa hizi dini uone uharibifu ulio wa kweli.

6. Kwa nini vita za umwagaji mkubwa wa damu zilitwa vita takatifu? Je zilikuwa ni maigizo ya huyo Mungu wao kuzi tekeleza kwa watu ?
Zipo sababu za msingi ktk kuanziwha vita takatifu kwenye dini hizi.

Nitasemea uislam, kwenye Uislamu moja ya sababu ya jamii ya kiislam kuingia vitani ni kama kutatokea jamii nyingine itakayo lenga kuwapora ardhi yao.

Niamini mimi hata atikee mtu atake kukupora nyumba yako ni lazima huyo mtu utamuona ni shetani.

Vinakuwa vita vitakatifu kwa sababu; wakazi wa ile ardhi ni watu wa Mungu, wanaomuabudu na kufuata sheria zake kikamilifu… yeyote anayepanga kuharibu utaratibu huu mzuri wa Mungu huyo ni mharibifu na anapaswa kuonywa kuachana na chokochoko zake, ikiwa maonyo hayatafanya kazi basi ni lazima apigwe kikamilifu kwa msaada wake Mungu ili kuokoa sheria, utaratibu na watu wa Mungu.

7. Kwa nini usambazi wa hizi dini uliji kita katika visa na utiaji wa hofu kuliko upendo na amani kama wasemavyo wao kupitia picha ya nje ya dini zao ?
Wasambazaji halisi wa hizi dini Mussa (AS), Yesu (AS) na Muhammad (PBUH) walikuwa ni watu wema na mfano bora sana kwa watu wao na ndiyo maana walipata wafuasi wengi sana.

Pta picha Yesu(AS) amefariki miaka 2000 iliyopita lakini mpaka sasa kuna zaidi ya watu bilioni 2 wanamuamini na kufuata mafundisho yake

Pata picha Muhammad (PBUH) kafa zaidi ya miaka 1400 iliyopita lakni mpaka sasa kuna zaidi ya watu Bilioni 1.5 wanamuamini na kufuata mafundisho yake.

Ingekuwa watu walisambaziwa kwa hofu niamini wangekwisha achana na mafundisho yao.

Kwa maana aliyewatia hofu keshakufa yanini wabaki na mafundisho yao?

8. Je waamini wake wana zifahamu historia ya hizi dini zao kwa kina ni wapi zimetoka, zipo na ziendako au wame baki kuwa waamini tu ?
Hapana, idadi kubwa ya waumini hawajui sehemu kubwa ya historia ya Dini zao.

Na hili ni tatizo kubwa.
9. Kwa nini hizi dini kuu tatu zili kuwa na bado mpaka sasa ni hatarishi kwa dini zengine zisizo shabihiana kiutendaji ?
Ni hatarishi kivipi? Sijaelewa

10. Ipi nafasi ya mwafrika katika hizi dini ?

Mwenye swali la ziada una weza ongeza, karibuni wadau.
Mwafrika si mtumwa tena, Mwafrika ni mtu mwerevu mwenye maarifa ha mazingira yake.

Mwafrika ana uwezo na utambuzi wa kugundua kuwa Mungu yupo na ili tuishi ktk jamii yenye maadili na maendeleo ni lazima tufuate sheria zake.

Ziko dini nyingi ila ni jukumu la Mwafrika kutafiti na kujua ni ipi dini ya kweli ili aifuate.

Kwahiyo sababu ya uharibifu hapa duniani si Dini, sababu ni mwanaadamu mwenyewe.

Maana uharibifu tuliuanza hata kabla ya dini hazijaja na tunauendeleza angali dini zipo na tena tunazitumia kama kichaka cha kufichia dhamira zetu ovu.

Dini ni kama kisu, Jikoni kinakata nyanya vitani kinatoa uhainwa mtu.

Je, tunathubutu kusema kisu ni kiovu?

Hapana, mtumiaji wa kisu ndiye ana hiyari akitumie kwa uovu au kwa wema.
 
Usiongee kitu ambacho hauna uhakika nacho, jadili mambo ambayo Una elimu nayo
 
Unaweza thibitisha haya madai yako mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…