Ikiwa wote wameumbwa na Mungu mmoja, na kisha wote kupewa uwezo ulio sawasawa na wengineo bila shaka
Uwezo sawa sawa upi unaokusudia ?
Kwa sababu tulishajadili huko nyuma na nikakataa ufahamu huu wa uwezo sawasawa kwa kils mtu.
Ambacho nilisema ni kuwa usawa ni kule kuwa kila mtu kapewa nafsi ambayo ina uhuru wa kuchagua la kufanya na la kutokulifanya.
bila shaka tunategemea wote wafanye maamuzi yaliyo sawasawa (wafanye chaguzi moja linalofanana kwa wote) kwasababu hakuna walichozidiana.
Mungu nafsi kaiumba na uwezo wa kupokea mambo na hiyo nafsi kukua katika yale mambo ambayo imeyapokea.
Sasa kama watu wameumbwa na nafsi zenye auwezo kupokea mambo na kuyaishi mambo hayo maana yake sasa chaguzi zao za kufanya mambo zitategemea na mazingira yao na kipi nafsi zao zimeimgiza.
Kwa hiyo kama nafsi itakuwa imekulia katika mambo ya kutisha na kikatili basi nafsi hii haitoona shida kuchagua kuuwa na kuibia watu.
Sasa nafsi hii inakuwa imechagua uovu kwa sababu ndo ilikulia katika mazingira hayo ya uovu.
Na nafsi ingine imekulia katika ustaarabu na mazingira ya uwoga,bila shaka nafsi hii sasa itaishi katika mazingira ya uoga na itakuwa inaogopa kuchagua mambo ya kutisha kama vile kuua,na kuiba kama ile nafsi ya juu.
Sasa nafsi hizi zilizoumbwa na Mungu mmoja zimekuwa na matokeo tofauti ya kuchagua mambo ya kufanya kwa sababu ya yale mazingira ambayo nafsi hizo zimelelewa kwayo.
Kwa hiyo Nafsi ambazo zina origin moja lakini zinatofautiana maamuzi kwa sababu zilipotoka kwenye orijin yao zililelewa katika mazingira tofauti tofauti hivyo bila shaka zitakuwa na chaguzi tofauti tofauti.
Tukumbuke kuwa nafsi zimeumbwa na uwezo wa kukua na kujengeka kutokana na yale inayoyapokea.
Hivyo uwezo wa nafsi kuchagua lipi afanye na lipi asifanye BILA KUANGALIA UBAYA NA UZURI basi uwezo huu Mungu kaupa nafsi zote.kwa maana kila nafsi ina uwezo huo.
lakini Kama maamuzi ya uchaguzi yanatofautiana basi bila shaka huo uwezo unazidiana kati ya mmoja na mwingine.
Maamuzi ya uamuzi yanatofautiana kutokana na mazingira ambayo nafsi hizo yamelelewa.
Uamuzi wa mtoto wa alshababu kuuwa hautakuwa sawa na uamuzi wa mtoto wako kuua.
Itakuwa ni tofauti chaguzi na uamuzi wao kwa sababu ya mazingira ambayo nafsi hizo mbili zimeishi.
Tukumbuke kuwa nafsi Mungu akiziumba zinatawanyikia mazingira mbalimbali ya kuishi,hili linafanya wawe na chaguzi tofauti na mazingira tofauti na changamoto tofauti.
Uwezo wa kuchagua sote tumepewa sawa.
Kule kuwa tuna uwezo sawa sawa Mungu hakulazimisha kuwa lazima tufanye kwa uwezo wetu sawasawa huo,ila hatuwezi kufanya zaidi ya uwezo wetu
Kama vile tukachagua hatutaki kufa,hili hatuna uwezo nalo.
Yaani tunaweza kuwa na uwezo sawasawa lakini mtu akaamua kufanya chini ya uwezo wake kwa sababu kuwa na uwezo haina maana ya kuwa kalazimisha usifanye chini ya uwezo.
Mfano.
Bakhresa na Mo dewji wote wana uwezo wa kukupa wewe milioni moja.
Kitendo cha wao kuwa na uwezo wa kukupa wewe milioni moja haina maana kuwa ni lazima wakupe milioni.
Wanaweza kukupa laki tatu kila mtu lakini bado uhalisia ukabaki pale pale kuwa uwezo wa kukupa milioni wanao.
Hivyo basi mkuu kuwa na uwezo wa jambo hakukukalifishi ama kukulazimisha wewe kufanya chini ya uwezo wako mkuu.
Hivyo bakhresa na modewji kuwa kwao na uwezo sawasawa wa kukupa wewe milioni moja basi bila shaka kuwa na uwezo huo hakuwalazimishi wao kutoa hiyo milioni,bali wanaweza kuchagua wao kuwa watoe chini ya hapo.
Hivyo hivyo kwa Mungu kutuumba na uwezo ffulani haina maana kuwa hakutupa yhuru wa kuchagua kufanya cha chini ya uwezo wetu.
Hivyo mkuu sidhani kama unafikiria kuwa huo uwezo wetu tuliopewa kama ni 100% basi ati tumekuwa programmed kutumia huo 100%.
Ikiwa unafikiria hivi sasa maana yake tunarudi nyuma kwamba Mungu katufanya maroboti.