Je, harusi ya Adam na Hawa ilifanyikia wapi, nani aliwafungisha ndoa?

Je, harusi ya Adam na Hawa ilifanyikia wapi, nani aliwafungisha ndoa?

... iliwahusu Adam na kizazi chake hadi pale Mungu alipobadili sheria. Kwani mwanzo palikuwa na Amri Kumi? Zilikuja baadaye kutokana na mahitaji ya wakati vivyo hivyo kwa masuala ya ndoa na mengineyo kama utawala, n.k.
Unajichanganya sana,Amri kumi inaingiaje hapo?
 
Tunazungumzia kauli ya ‘mzaane mkaijaze dunia’ , ambayo ndio imetumika kama ndoa mnavyodai, kwamba mmdai imewahusu wote Adam na hawa na vizazi vyao hadi pale sheria mpya ilivyokuja (lack of consistency by the way), kwahiyo vizazi vyote vya Adam na Hawa walikuwa wamefungishwa ndoa na kila kljinsia tofauti iliyokatiza mbele yao kwa hiyo kauli ya Mungu? Kama wanyama?
Maneno ya Mungu zaeni mkaijaze nchi yasikusumbue sana
 
UOTE="FRANCIS DA DON, post: 36746978, member: 168549"]
Kwahiyo bila nyoka binadamu wote duniani tusingekuwepo, kwahiyo tumshukuru ibilisi kwa uwepo wetu then?
[/QUOTE]
Sijui mnatoa wapi tafsiri hizi,maana Muu aliagiza Adamu na Hawa mkewe wazae wakaijaze dunia hapo ni Mara baada ya kukamilisha uumbaji soma Mwanzo 1:26 na kuendelea,lakini sura ya tatu inatuonesha namna ni namna gani walikosa kwa kula mti wa ujuzi wa mema na mabaya,ndiyo maana baada yahayo Mungu akawafukuza katika bustani ya Edeni wasije wakala matunda ya mti wa uzima
 
Hapa ni kama Mungu anawaumba watu ili wakosee makusudi na kisha awachome moto. Alishindwa nini kuwaaumba binadamu waliokamilika ili wazingatie maagizo yake?
Yaani umuumbe mtu pasipo ridhaa yake na kisha na bado unamuumba akiwa na kasoro halafu eti akikosea unamchoma moto wakati yeye mwenyewe Mungu ndio kafanya makusudi kukuumba hivyo
Mungu alimuumba mwanadamu na kumfanya awe na Uhuru wa kuchagua siyo awe anaongozwa kwa lazima
 
Sijui mnatoa wapi tafsiri hizi,maana Muu aliagiza Adamu na Hawa mkewe wazae wakaijaze dunia hapo ni Mara baada ya kukamilisha uumbaji soma Mwanzo 1:26 na kuendelea,lakini sura ya tatu inatuonesha namna ni namna gani walikosa kwa kula mti wa ujuzi wa mema na mabaya,ndiyo maana baada yahayo Mungu akawafukuza katika bustani ya Edeni wasije wakala matunda ya mti wa uzima
Kabla ya kula mti wa ujuzi wa mema na mabaya, nani aliwafundisha namna ya kufanya ngono ili wazaane? Na walizaana kabla au baada ya kula mti wa ujuzi?
 
Mungu alimuumba mwanadamu na kumfanya awe na Uhuru wa kuchagua siyo awe anaongozwa kwa lazima
Uhuru wa kuchagua huwa anapewa kabla au baada ya kuletwa duniani? Kama ni baada ya kuletwa duniani inakuwaje hatmanyake inakuwa imeshafahamika kabla ya kuletwa duniani? Kuna haja gani ya kusema tunaweza kuamua kwa uhuru wakati tayari tumeshahukukiwa kabla hata ya kuumbwa? How?
 
Anajua kwa sababu ana ujuzi juu ya mambo yetu ya baadae.

Na ujuzi huo hajaufungamanisha na kuziprogram nafsi zetu,yeye atabaki anajua tu bila kututenza Nguvu tuyapitie yale anayoyajua,atabaki anajua,kuhusu kutenda sisi tuna hiyari yetu.
Ujuzi lazima unafungamana na kuziprogram nafsi, kwasababu yeye ndiye anayeumba mtu kila kitu hivyo mtu hawezi kwenda kufanya matendo ya uovu ikiwa yeye Mungu hajataka huyo mtu akatende uovu. Ikiwa mtu anatenda uovu basi hakuna shaka kuwa Mungu mwenyewe ndiye ametaka huyo mtu akatende huo uovu.

Mungu kutokana na uwezo wake alijua fika kabisa kuwa huyu mtu niliyemuumba akienda duniani atakuwa muovu na atakuwa ni wa motoni, nafasi ya huyu kurekebishika haikuwa pindi akifika duniani bali ni pale pale alipokuwa anaumbwa kabla hata hajapelekwa duniani. Kitendo cha kumwacha aende duniani akiwa anajua kuwa nini atachoenda kufanya basi hakuna shaka kapenda iwe ivyo. Au unataka kuniambia Mungu hana uwezo wa kumbadilisha huyo mtu pindi anamuumba ili akienda duniani asichague uovu?
 
Walichozidiana ni matumizi yao ya nafsi.
Mungu katuumba na nafsi zisizo na ukomo katika kuyaendea mambo.

Kwa hiyo juhudi zako ndio zitazidisha utashi wa nafsi yako.sote ametuumba na nafsi zenye uwezo wa kufanya mambo pale tutakapofanya juhudi na kuyaendea wenyewe.

Hivyo mwenye kisu kikali ndo atakula nyama.

Labda nikupe mfano hivi

Nafsi zetu ni kama kapu ambalo halina kitu,kule kutokuwa na kitu ndo kila mmoja aliumbwa hivyo.

Kwa maana kila mmoja nafsi yake iliumbwa na nafasi(uwezo)wa kutia kitu fulani katika ile nafasi ya kapu(nafsi)
tujadili hapa kwenye neno uliloweka kaenye mabano "uwezo" nadhani litatupa taswira ya kuona ni namna gani mmoja achague jambo tofauti na mwingine. Ikiwa wote wameumbwa na Mungu mmoja, na kisha wote kupewa uwezo ulio sawasawa na wengineo bila shaka tunategemea wote wafanye maamuzi yaliyo sawasawa (wafanye chaguzi moja linalofanana kwa wote) kwasababu hakuna walichozidiana. lakini Kama maamuzi ya uchaguzi yanatofautiana basi bila shaka huo uwezo unazidiana kati ya mmoja na mwingine.
 
Aya maswali mengine bhana unaweza uliza funza kaingiaje kwenye kokwa la embe
 
Ujuzi lazima unafungamana na kuziprogram nafsi,
Nimeshakueleza kuwa ujuzi huo haufungamani ku kuziprogram nafsi,hiki kipengele ni muhimu sana ukikielewa.

Unaposema ni lazima ujuzi ufungamane na kuziprogram nafsi hapo sasa unaonesha ni wazi kuwa umekuwa na msimamo wako hata baada ya kuambiwa kuwa ujuzi haufungamanishwi na nafsi.

Huu ulazima unaouweka wewe Mungu mwenyewe hakusema hivyo,yani kana kwamba unamsemea mwenyewe.

Ama unawaza kuwa Mungu anauwezo kama binadamu tu,ndiyo maana unaona haiwezekani Mungu kuwa mjuzi wa yajayo bila kufungamanisha na ku program hayo mambo.

Sasa bila shaka unataka tumjadili Mungu kwa mujibu wa ule uwezo wa kibinadamu.

Kwa sababu kinachokufanya ukatae wewe kuwa ujuzi wa mungu hajaufungamanisha na kuprogram nafsi ni kwa sababu wewe umeona kuwa binadamu hawezi hilo kwa hiyo unahisi pia hata Mungu hawezi.

Ama umeona kibinadamu haiwezekani,wakati unasahau kuwa lisilowezekana kwa binadamu basi kwa Mungu analiweza.

Mimi nazungumza na wewe hapa kwa zaidi ya uwezo wa kibinadamu,wewe unabakia na mazungumzo yale yale ya uwezo wa kibidanadamuv
kwasababu yeye ndiye anayeumba mtu kila kitu hivyo mtu hawezi kwenda kufanya matendo ya uovu ikiwa yeye Mungu hajataka huyo mtu akatende uovu
Mungu haingilii maamuzi ya mja,yaani Mungu hajatufanya sisi kuwa maroboti.

Mungu hataki kumuingilia mja katika mtihani wake alafu ampe majibu,haitokuwa maana ya myihani

Kama ingekuwa Mungu analazimisha mtu afanye analotaka Mungu,basi hakuna maana ya kutujaribu.
Mungu kutokana na uwezo wake alijua fika kabisa kuwa huyu mtu niliyemuumba akienda duniani atakuwa muovu na atakuwa ni wa motoni, nafasi ya huyu kurekebishika haikuwa pindi akifika duniani bali ni pale pale alipokuwa anaumbwa kabla hata hajapelekwa duniani. Kitendo cha kumwacha aende duniani akiwa anajua kuwa nini atachoenda kufanya basi hakuna shaka kapenda iwe ivyo. Au unataka kuniambia Mungu hana uwezo wa kumbadilisha huyo mtu pindi anamuumba ili akienda duniani asichague uovu?
Shida nikuwa unafikiria mambo ya Mungu kwa muono wa uwezo wa kibinadamu.

Mimi najadili hapa kwa muono wa uwezo wa Kimungu sio kibinadamu kama ambavyo wewe unafikiria.

Mungu kutokana na uwezo wake alijua fika kabisa kuwa huyu mtu niliyemuumba akienda duniani atakuwa muovu na atakuwa ni wa motoni,
Ujuzi huo haifungamani na kumtenza nguvu(kumlazimisha mja)kwa namna yeyote ile.

Hapa kwa uwezo wetu wa kawaida binadamu tunaona haiwezekani.

Ukikataa jambo hili basi bila shaka unafanya marejeo uwezo wa kibinadamu.
nafasi ya huyu kurekebishika haikuwa pindi akifika duniani bali ni pale pale alipokuwa anaumbwa kabla hata hajapelekwa duniani.
Mungu anajua anachokifanya,hivyo kumrekebisha mtu huyo maana yake wakati anamuumba hakujua kua ni muovu ndio maana anataka amrekebishe.

Kwa hiyo akisema amrekebishe maana yake alikosea kumuumba hajui anachofanya mungu,upo hapo ?
Na Mungu anajua analofanya.

Na akisema awaumbe watu wote wema basi hakuna maana ya kutuleta duniani ili tujaribiwe nafsi zetu kwa sababu wote tushakuwa wema.

Sasa kwa kujua hilo Mungu akamuumba mtu huku akijua kuwa huku ataenda wapi na yule ataenda wai.

Na katika kujua huko HAJAKUFUNGAMANISHA NA KULAZIMISHA NAFSI HIZO.

Kitendo cha kumwacha aende duniani akiwa anajua kuwa nini atachoenda kufanya basi hakuna shaka kapenda iwe ivyo
Mungu Alishaamua kuwa amewaleta watu katika chumba cha mitihani.

Hivyo katika hilo alijua fika kuwa kuna ambao watafeli na kuna ambao watafaulu.

Na aliumba pepo kwa wema na moto kwa wabaya,hivyo kusema alipenda kuumba moto sio sahihi kwa sababu Mungu anapenda mazuri tu.

MUNGU ANAPENDA MAMBO MAZURI TU.

Na huruhusu ama kuumba mazuri na mabaya,lakini katika kupenda yeye anapenda mazuri tu,lakini katika kuumba huwa kuna mabaya na mazuri yamo.
 
Na akisema awaumbe watu wote wema basi hakuna maana ya kutuleta duniani ili tujaribiwe nafsi zetu kwa sababu wote tushakuwa wema.
.
Nilichogundua ni kwamba Kuna Baadhi ya mambo unayatoa kwenye uwezo wa Mungu. Mungu anaumba package yote kwa binadamu kwanzia hardware (mwili) mpaka sofware (akili na utashi) hapa naona kwenye software ndipo unapopaweka kando uwezo wa Mungu. Huyu mtu anayechagua mema, anafanya kutokana asilimia ya utimilifu wake katika mfumo wa software yake aliyowekewa na Mungu. Na huyu anayefanya au kuchagua uovu pia anafanya kwa kuongozwa na mfumo wa software yake aliyowekewa na Mungu pia. Hakuna binadamu anayejiwekea utashi wa aina yake. Nakupa mfano unaohusiana na wewe mwenyewe.

Bila shaka wewe hutaki kabisa kufanya jambo utakalomkosea Mungu wako, lakini ukiamka asubuhi mpaka inafika usiku ukitathmini matendo ya siku nzima utakuta tu aidha ulimuongopea mtu ama ulisengenya ama umefanya lolote lile ambalo halimpendezi Mungu wako. Hivyo yote hayo unayafanya kwavile mfumo wako wa software umeamua kuyachagua kuyafanya.

Sasa kwanini unaichukia matendo ya dhambi, na unajua kabisa haya ni matendo maovu, na upo tayari kufanya juu chini ili uyaache lakini ikifika jioni ukijaribu kuwaza lazima utakuta kuna jambo uliloenda kinyume na Mungu. Unadhani ni kwanini kitu hukipendi kukifanya lakini kinafanyika?
 
tujadili hapa kwenye neno uliloweka kaenye mabano "uwezo" nadhani litatupa taswira ya kuona ni namna gani mmoja achague jambo tofauti na mwingine. Ikiwa wote wameumbwa na Mungu mmoja, na kisha wote kupewa uwezo ulio sawasawa na wengineo bila shaka tunategemea wote wafanye maamuzi yaliyo sawasawa (wafanye chaguzi moja linalofanana kwa wote) kwasababu hakuna walichozidiana. lakini Kama maamuzi ya uchaguzi yanatofautiana basi bila shaka huo uwezo unazidiana kati ya mmoja na mwingine.
Hili hoja hujalijibu mkuu, nasubiri jibu pia hapa kwenye hii hoja yangu.
 
Hili hoja hujalijibu mkuu, nasubiri jibu pia hapa kwenye hii hoja yangu.
Sorry mkuu hapa naibia kuandika,natamani ningekuwa nimetulia sehemu kando lakini harakati bize kwa sana nyakati hizi,ila najitahidi kureply.

Hoja nimeiona nitaijibu wasaa wa utulivu.
 
Ikiwa wote wameumbwa na Mungu mmoja, na kisha wote kupewa uwezo ulio sawasawa na wengineo bila shaka
Uwezo sawa sawa upi unaokusudia ?

Kwa sababu tulishajadili huko nyuma na nikakataa ufahamu huu wa uwezo sawasawa kwa kils mtu.

Ambacho nilisema ni kuwa usawa ni kule kuwa kila mtu kapewa nafsi ambayo ina uhuru wa kuchagua la kufanya na la kutokulifanya.

bila shaka tunategemea wote wafanye maamuzi yaliyo sawasawa (wafanye chaguzi moja linalofanana kwa wote) kwasababu hakuna walichozidiana.
Mungu nafsi kaiumba na uwezo wa kupokea mambo na hiyo nafsi kukua katika yale mambo ambayo imeyapokea.

Sasa kama watu wameumbwa na nafsi zenye auwezo kupokea mambo na kuyaishi mambo hayo maana yake sasa chaguzi zao za kufanya mambo zitategemea na mazingira yao na kipi nafsi zao zimeimgiza.

Kwa hiyo kama nafsi itakuwa imekulia katika mambo ya kutisha na kikatili basi nafsi hii haitoona shida kuchagua kuuwa na kuibia watu.

Sasa nafsi hii inakuwa imechagua uovu kwa sababu ndo ilikulia katika mazingira hayo ya uovu.

Na nafsi ingine imekulia katika ustaarabu na mazingira ya uwoga,bila shaka nafsi hii sasa itaishi katika mazingira ya uoga na itakuwa inaogopa kuchagua mambo ya kutisha kama vile kuua,na kuiba kama ile nafsi ya juu.

Sasa nafsi hizi zilizoumbwa na Mungu mmoja zimekuwa na matokeo tofauti ya kuchagua mambo ya kufanya kwa sababu ya yale mazingira ambayo nafsi hizo zimelelewa kwayo.

Kwa hiyo Nafsi ambazo zina origin moja lakini zinatofautiana maamuzi kwa sababu zilipotoka kwenye orijin yao zililelewa katika mazingira tofauti tofauti hivyo bila shaka zitakuwa na chaguzi tofauti tofauti.

Tukumbuke kuwa nafsi zimeumbwa na uwezo wa kukua na kujengeka kutokana na yale inayoyapokea.

Hivyo uwezo wa nafsi kuchagua lipi afanye na lipi asifanye BILA KUANGALIA UBAYA NA UZURI basi uwezo huu Mungu kaupa nafsi zote.kwa maana kila nafsi ina uwezo huo.

lakini Kama maamuzi ya uchaguzi yanatofautiana basi bila shaka huo uwezo unazidiana kati ya mmoja na mwingine.
Maamuzi ya uamuzi yanatofautiana kutokana na mazingira ambayo nafsi hizo yamelelewa.

Uamuzi wa mtoto wa alshababu kuuwa hautakuwa sawa na uamuzi wa mtoto wako kuua.

Itakuwa ni tofauti chaguzi na uamuzi wao kwa sababu ya mazingira ambayo nafsi hizo mbili zimeishi.

Tukumbuke kuwa nafsi Mungu akiziumba zinatawanyikia mazingira mbalimbali ya kuishi,hili linafanya wawe na chaguzi tofauti na mazingira tofauti na changamoto tofauti.

Uwezo wa kuchagua sote tumepewa sawa.

Kule kuwa tuna uwezo sawa sawa Mungu hakulazimisha kuwa lazima tufanye kwa uwezo wetu sawasawa huo,ila hatuwezi kufanya zaidi ya uwezo wetu

Kama vile tukachagua hatutaki kufa,hili hatuna uwezo nalo.

Yaani tunaweza kuwa na uwezo sawasawa lakini mtu akaamua kufanya chini ya uwezo wake kwa sababu kuwa na uwezo haina maana ya kuwa kalazimisha usifanye chini ya uwezo.

Mfano.

Bakhresa na Mo dewji wote wana uwezo wa kukupa wewe milioni moja.

Kitendo cha wao kuwa na uwezo wa kukupa wewe milioni moja haina maana kuwa ni lazima wakupe milioni.

Wanaweza kukupa laki tatu kila mtu lakini bado uhalisia ukabaki pale pale kuwa uwezo wa kukupa milioni wanao.

Hivyo basi mkuu kuwa na uwezo wa jambo hakukukalifishi ama kukulazimisha wewe kufanya chini ya uwezo wako mkuu.

Hivyo bakhresa na modewji kuwa kwao na uwezo sawasawa wa kukupa wewe milioni moja basi bila shaka kuwa na uwezo huo hakuwalazimishi wao kutoa hiyo milioni,bali wanaweza kuchagua wao kuwa watoe chini ya hapo.

Hivyo hivyo kwa Mungu kutuumba na uwezo ffulani haina maana kuwa hakutupa yhuru wa kuchagua kufanya cha chini ya uwezo wetu.

Hivyo mkuu sidhani kama unafikiria kuwa huo uwezo wetu tuliopewa kama ni 100% basi ati tumekuwa programmed kutumia huo 100%.

Ikiwa unafikiria hivi sasa maana yake tunarudi nyuma kwamba Mungu katufanya maroboti.
 
.
Kwa hiyo kama nafsi itakuwa imekulia katika mambo ya kutisha na kikatili basi nafsi hii haitoona shida kuchagua kuuwa na kuibia watu.

Sasa nafsi hii inakuwa imechagua uovu kwa sababu ndo ilikulia katika mazingira hayo ya uovu.

Na nafsi ingine imekulia katika ustaarabu na mazingira ya uwoga,bila shaka nafsi hii sasa itaishi katika mazingira ya uoga na itakuwa inaogopa kuchagua mambo ya kutisha kama vile kuua,na kuiba kama ile nafsi ya juu.

Sasa nafsi hizi zilizoumbwa na Mungu mmoja zimekuwa na matokeo tofauti ya kuchagua mambo ya kufanya kwa sababu ya yale mazingira ambayo nafsi hizo zimelelewa kwayo.

Kwa hiyo Nafsi ambazo zina origin moja lakini zinatofautiana maamuzi kwa sababu zilipotoka kwenye orijin yao zililelewa katika mazingira tofauti tofauti hivyo bila shaka zitakuwa na chaguzi tofauti tofauti.

Tukumbuke kuwa nafsi zimeumbwa na uwezo wa kukua na kujengeka kutokana na yale inayoyapokea.

Hivyo uwezo wa nafsi kuchagua lipi afanye na lipi asifanye BILA KUANGALIA UBAYA NA UZURI basi uwezo huu Mungu kaupa nafsi zote.kwa maana kila nafsi ina uwezo huo.

Maamuzi ya uamuzi yanatofautiana kutokana na mazingira ambayo nafsi hizo yamelelewa.
hapa mkuu umejibu lakini jibu lako halina uhalisia. Mimi nimekulia katika mazingira ya watu walevi, na wavuta bangi lakini sivuti bangi wala sinywi pombe.

Kuna watu kwanzia familia yao yote ni watu wanaojitahidi kushika Imani ya Mungu na pia katika malezi wanamlea mtoto katika mazingira ya hofu ya Mungu lakini huyo mtu anakuwa muovu kupindukia. Hapa mkuu hakuna uhalisia kwakile ulichokijibu. Unataka kuniambia 50-70% ya watu wa Saudia Arabia au Israel au Vatican ni wema kwavile tu nafsi zimelelewa katika mazingira ya kiimani?
 
Back
Top Bottom