Je, jeshi linalolinda mfumo usio wa haki bado ni la wananchi? (mtazamo kutoka Afrika Mashariki hadi Sahel)

Je, jeshi linalolinda mfumo usio wa haki bado ni la wananchi? (mtazamo kutoka Afrika Mashariki hadi Sahel)

Msela Wa Kitaa

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2021
Posts
2,217
Reaction score
4,280
Katika siasa za Afrika, kuna tofauti kubwa kati ya majeshi ya baadhi ya nchi. Wengine hujiona kama watumishi wa dola, wengine kama watumishi wa watawala, na wachache kama wakombozi wa kweli. Nimekuwa nikifuatilia mifano mbalimbali, na hii ndiyo taswira niliyoona:

1. Madikteta wengi huweka watu wao kwenye nafasi nyeti​

Hili si jambo jipya. Watawala wa muda mrefu kama Museveni wa Uganda, wamejenga utawala unaotegemea watu wa karibu – hasa kutoka kabila lao (kwa Museveni: Banyankole). Si idadi ya watu wake wa karibu tu inayohesabika, bali nguvu ya maamuzi kwenye usalama, fedha, na mawasiliano.

2. Mfano wa Uganda – Buganda wakihisi kunyimwa mamlaka yao ya kihistoria​

Ingawa Buganda ina uwakilishi mkubwa wa mawaziri (9) ukilinganisha na Ankole (8), bado hoja kuu ni kwamba mawaziri wa Ankole wanashikilia nafasi nyeti zaidi. Aidha, majina ya kihistoria ya Buganda kama Ssingo, Kyaggwe, Buddu yamebadilishwa—hali inayochukuliwa kama kufuta utambulisho wa kifalme wa Buganda.

3. Vyama vya upinzani havina nguvu ya kubadilisha mfumo​

Afrika Mashariki, upinzani mara nyingi huwa dhaifu kwa sababu vyombo vyote vya dola (jeshi, polisi, tume ya uchaguzi) vimejikita ndani ya mfumo wa chama tawala. Hakuna “fair play.” Upinzani hulemazwa kwa kutumia sheria, vitisho, na mizengwe ya kisiasa.

4. Wanajeshi wa Sudan vs Burkina Faso/Mali/Gabon​

Sudan ilitoa mfano wa jeshi lililompindua dikteta lakini likabaki kupigania madaraka – SAF na RSF sasa wanapigana wenyewe kwa wenyewe. Hawakuwa na malengo ya ukombozi, bali walitaka kuchukua nafasi ya Bashir.

Tofauti kabisa na:

  • Burkina Faso (Traoré) – amejitambulisha kama mzalendo anayepambana na ukoloni mamboleo.
  • Mali (Assimi Goïta) – amefukuza wanajeshi wa Ufaransa na kusimama kidete kama taifa huru.
  • Gabon – jeshi lilimwondoa Ali Bongo na kukataa kurithishwa madaraka ya kifalme.

5. JWTZ ya Tanzania – Jeshi la nidhamu, lakini limefungwa kimfumo​

Wanajeshi wa Tanzania wanaheshimika kwa nidhamu yao, lakini bado wako chini ya mfumo wa chama. Wanafaidika na nafasi baada ya kustaafu, hivyo si rahisi kuikosoa au kuibadili Serikali ya CCM. Hawajawahi kuwa chombo cha mabadiliko ya kisiasa – wao ni walinzi wa utulivu uliopo, hata kama si haki.

6. Je, hali hii inaweza kubadilika?​

Ni vigumu. Bila presha kutoka kwa wananchi au mgawanyiko ndani ya dola, hakuna jeshi Afrika Mashariki litakalovunja mfumo huu kirahisi kama ilivyofanyika Sahel.

Swali la mwisho kwa wana JF wenzangu:

Jeshi linalolinda mfumo wa kimabavu, hata kama halifyatui risasi, bado ni sehemu ya ukandamizaji,Au tunalipa heshima kwa sababu halijaonekana wazi likitumia nguvu?

Karibuni tujadiliane.
 
Ngoja waje ila Tutaamka tu Mkuu ipo siku inakuja.
Kuna mtu nilikutana na maoni yake humu JF akidai CCM inatengeneza jeshi la vijana wasio na ajira akitumai siku moja litaiwashia moto CCM

Ngoja tusubiri maana Millenial tulijitahidi tukashindwa, hawa Gen'z wetu wape Amapiano na habari za Simba na Yanga hawana muda na mambo ya maana INAUMA SANA
 
Ni janga la kitaifa mkuu kizazi cha tik tok wasiojitambua ambao hawajui nini wanachofanya, chakusikitisha wasomi tulio nao hawa nao hawajitambui pia, hii nchi Mungu atusaidie.
 
Kuna mtu nilikutana na maoni yake humu JF akidai CCM inatengeneza jeshi la vijana wasio na ajira akitumai siku moja litaiwashia moto CCM

Ngoja tusubiri maana Millenial tulijitahidi tukashindwa, hawa Gen'z wetu wape Amapiano na habari za Simba na Yanga hawana muda na mambo ya maana INAUMA SANA
We umefanya nini au hukua kijana ?
 
We umefanya nini au hukua kijana ?
Nakuona Gen'z umepaniki hatupo hapa kukasirishana bali kueleweshana

Milenia tumefanya kwa kiasi chake sio kama kizazi hiki cha Insta mmelala sana huo ndio ukweli

Japo wanasema ukweli unauma
 
Nakuona Gen'z umepaniki hatupo hapa kukasirishana bali kueleweshana

Milenia tumefanya kwa kiasi chake sio kama kizazi hiki cha Insta mmelala sana huo ndio ukweli

Japo wanasema ukweli unauma
Hujajibu swali umefanya nini elezea hapa tuone ulichokufanta kabla ya kulaumu wenzio
 
Katika nchi nyingi za Afrika, viongozi hawawajibiki kwa wananchi wao. Hii inatokana na taasisi dhaifu za kidemokrasia na ukosefu wa mifumo madhubuti ya kuwawajibisha viongozi. Hali hii inawapa viongozi uhuru wa kufanya maamuzi bila kuzingatia maslahi ya wananchi.
 
Afrika Mashariki, upinzani mara nyingi huwa dhaifu kwa sababu vyombo vyote vya dola (jeshi, polisi, tume ya uchaguzi) vimejikita ndani ya mfumo wa chama tawala. Hakuna “fair play.” Upinzani hulemazwa kwa kutumia sheria, vitisho, na mizengwe ya kisiasa.
Mwisho wa kunukuu
 
Sudan ilitoa mfano wa jeshi lililompindua dikteta lakini likabaki kupigania madaraka – SAF na RSF sasa wanapigana wenyewe kwa wenyewe. Hawakuwa na malengo ya ukombozi, bali walitaka kuchukua nafasi ya Bashir.
Hii kitu ilitokea pia kwa Waliojiita Wapigania Uhuru miaka ya 60s.

Akina Robert Mugabe, akina M7 na kina Mobutu ni mifano.

Walifukuzana na wazungu sio kwa sababu ya uzalendo bali ugomvi wa madaraka. Akina Daniel Moi
 
Mwisho wa kunukuu
Hizo kada nyingine sina shida nazo, shida yangu kwa Jeshi linalojiita la Wananchi na bado linakumbatia udhalimu wa watawala

Likiamka kama Sahel walivyofanya hizo kada nyingine kama NEC, PoliCCM hazitakuwa na uwezo wa kuvuruga
 
Back
Top Bottom