Je, jeshi linalolinda mfumo usio wa haki bado ni la wananchi? (mtazamo kutoka Afrika Mashariki hadi Sahel)

Ndio nimeuliza hicho kizazi kimefanya nini dhidi ya serikali ila naona hunipi jibu la kueleweka mzee
Milenia walikuwa wanahoji mfumo, Gen Z wanahoji kama kuhoji kuna maana.

Kipindi chetu tulikuwa tunafuatilia midahalo kwa umakini, tulikuwa tunaandamana tofauti na nyie wazee wa tik tok na memes

CCM Iliogopa “kumwaga unga” kwa uwazi

Ila kipindi chenu mambo mabovu yanapitishwa kwa uwazi tu mmekaa kimyaa

Ila siwalaumu nyie asilimia mia moja

Haya yamesababishwa na awamu ya 5 kwa asilimia 80
 
Jwtz lina ma generali waliong'olewa meno kwa mema ya nchi na hulinda maslahi yao ya upendeleo.

Generali yeyote akistaafu hupewa manufaa makubwa kwenda kufa huku wakitabasamu.

Generali mwenye madaraka ya Cdf hustaafu kwa kufumba jicho moja huku jingine likiona, namaanisha kuanzia heshima yake, mshahara, magari, walinzi na stahiki zingine huondoka navyo na huendelezwa kwa 80% mpaka kufa kwake.

Sasa hawa viongozi kwa asali wanayokuwa wamelambishwa na taifa kikatiba, hawawezi kufanya fyoko kwa watawala hata iweje, wataimba kulinda katiba kumbe ni kulinda watawala pamoja na maslahi yao binafsi hata kama ni utawala wa kimumiani na kisultani.

Mara ngapi katiba imevunjwa wazi wazi na hatujaona wakiilinda kama walivyoapa kuilinda?

Wanajeshi wanaoweza kufanya coup detat ni wale ambao hawapo kwenye vyeo vikubwa na ambao ni wazalendo halisi wa nchi hii kama ilivyo kwa wenzao wa Burkina Faso na Mali huko, huwezi sikia Brigedia na kuendelea kahusika.

Na atakayeplot atumie akili nyingi sana za ziada na pia akubali kufanya mapinduzi ya kumwaga damu, kufa na kupona yeye ama kuua kwa sababu kuna informers wengi sana kuweza kuharibu mission kwa kuripoti kila mwenendo usiokuwa wa kawaida ambao ni wengi wametapakazwa sana kwenye majeshi.

Nakumbuka saga la kina Uncle Tom, Mbogoro, Eugene Maganga, Hans pope, MacGhee na Jnr Offrs wengine walioshiriki kutaka kumpindua Nyerere, lakini walikuja kufelishwa na hao informers.

Mabaya yote yanayofanywa na watawala yanawakera sana wanajeshi, ila hawana viongozi wa kuweza kuwawakilishia kero na chuki zao kwa watawala.

Madaraka ya Cdf wa Tz ni ya kisiasa huteuliwa na Rais, hana sifa kama wanazobeba maCdf wa nchi kama Kenya na kwingineko ambako sifa ya kuwa Cdf lazima abebe sifa halisi za kuwazidi wenzake kwa seniority na sifa zingine za uadilifu na medani na ni lazima aidhinishwe na Bunge.

Hapa kwetu hakuna kitu kama hicho, mtu Junior kabisa kwa Seniority ama rank ya chini, anaweza kupandishwa leo kwa kuvuruga taratibu zote za upandishwaji wa vyeo na kumfanya awe mkuu wa Majeshi ghafla bin vuu.

Muda wowote anaweza kutumbuliwa kwa tangazo la 'msemaji wa Ikulu' na kutupiwa madaraka dhaifu yasiyo ya kitaaluma na hawezi kufanya lolote.

Wadhani mtu kama huyo ana uwezo hata wa kumnong'oneza jambo Rais masikioni kumweleza yanayokera waTz na askari wa chini yake?

Hao wapo mbingu nyingine kabisa.
 
Mimi nataka useme mlifanya nini wewe unaniambia kuhoji uhoji wewe umekua polisi jibu hili swali mlifanya nini naona swali langu hulijibu
 
Mkuu kwa hali hiyo hii nchi ngumu mnooo kubadilika

Nyerere alifanya mengi ya kujipendelea akifikiri atatawala milele
 
Tafuta kazi ya kufanya acha kuandika huu ujinga utakufa maskini. We hujui kazi ya jeshi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…