Je, kuna faida gani ya kuwa na mikutano ya vyama vya siasa baada ya uchaguzi?

Je, kuna faida gani ya kuwa na mikutano ya vyama vya siasa baada ya uchaguzi?

RNA

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2013
Posts
1,647
Reaction score
2,803
Habari JF, Tuweke mbali uhalisia wa namna CCM inavyoingia madarakani.

Hivi kuna faida gani baada ya chama kimoja kushinda uchaguzi kwa mikutano ya vyama vya siasa kuendelea?

Uchaguzi umeisha kwanini chama kilichoshinda kisiachwe kitekeleze ilani yake na kuongoza nchi tuje tuwa hukumu kwenye uchaguzi unaofuata?

Chama kishashinda kwanini hiyo mivutano isiachwe Bungeni na kwenye mabaraza ya Madiwani badala ya kuendelea kutuchanganya wananchi?

Uchaguzi ushaisha kwanini wananchi tukaachwa kusumbuliwa vichwa na tukatekeleza malengo na matakwa ya Chama kinachotawala?

Hivi mama yuko bize na majukumu ya kazi anasikia CHADEMA au chama chochote wanaandaa mkutano na maandamano kuhusu katiba mpya au mfumko wa bei au ugumu wa maisha au safari za Mama au mikopo kwa Maneno makali mengine ya kweli na mengine uzushi kama tulivyo zoea mikutanoni. Je, haiathiri utendaji wa serikali?

Je, ni mikutano pekee wanaweza tumia kufikisha ujumbe kwa wananchi? Magazeti, televisheni, mitandao ya kijamii?

Mi nadhani kuna haja ya hili jambo kuangaliwa upya ,Mikutano ifanyike mwaka mmoja kabla ya uchaguzi au kipindi cha uchaguzi.
 
Kwanza watu washalamba asali unategemea watakuja na nini cha Maana? Hapo tusubiri maamuzi ya CCM wenyewe wakiamua walete katiba au la, wapunguze kukopa, tozo nk
 
Habari Jf , Tuweke mbali uhalisia wa namna CCM inavyoingia madarakani .

Hivi kuna faida gani baada ya chama kimoja kushinda uchaguzi kwa mikutano ya vyama vya siasa kuendelea....
Hebu weka kichwa chako sawa kiangalie kasikazini ili ueleweke, CCM inayojipa ushindi wa lazima ndiyo inayofanya mikutano kila kukicha na kila kichochoro! Kila siku tunaona makundi ya wanaccm wakiongozana kama mbuzi wa mijini, kazi yao ni kuzurula tu huku wakilipana hela ya maji!

Hivyo vyama unavyodai vinafanya mikutano ni vipi na wapi! CCM ni kikwazo kwa ukuaji wa maendeleo ya Tanzania na tunachoshuhudia ni viongozi wake kuchukua nafasi ya matajiri toka kwa wahindi na ndicho kinachowaganya waikatae katiba mpya, amka kijana ziteme propaganda za viongozi wako.
 
Kwa mitazamo wangu mimi hakuna ulazima wowote, mikutano ya vyama vya siasa iwe kipindi cha uchaguzi tu.
Ni kupotezeana muda tu.

Tatizo ni masheria mabovu uanyoruhusu maujingaujinga hayo. Hata mabendera ya vyama hayana maana.

Viongozi wa chama wa kata, wilaya na mikoani ni mavyeo ya kipuuzi
 
Naona kwa namna nyingine unapingana na sheria inayoruhusu uwepo wa mikutano ya siasa, kama hivyo ndivyo, bora ungekuja moja kwa moja kuipinga hiyo sheria, kuliko kupinga matokeo ya utekelezwaji wa hiyo sheria.

Kwa mtazamo wangu, watu aina ya mleta mada naona mmeathiriwa na mawazo ya kidikteta na kibabe, na mawazo haya kuna uwezekano mkubwa yalipandikizwa kwenye vichwa vyenu pale hii mikutano ilipozuiwa kinyume cha sheria, ndio mkaanza kuona haina maana, japo inawezekana kabla ya pale, hamkuwahi kuwa na wazo hilo.

Hivyo watu wenye mawazo ya sampuli yako ni kuwapa muda tu, naamini mtabadilika mitazamo yenu baada ya muda fulani, au kama haya mawazo yenu yakipata nguvu zaidi, basi mwisho wa siku itakuwa wengi wape, tusubiri watanzania wenyewe wataamua.

Lakini binafsi siamini kama hiyo mikutano huwazuia watu kufanya kazi, kwani mwenye kujielewa hawezi kukubali familia yake ife kwa njaa kisa yeye anahudhuria mikutano ya siasa... hii maana yake wanaohudhuria wanakuwa wameshajipanga kwa siku yao, kwani kila mtu na mipango yake.
 
Kwa mitazamo wangu mimi hakuna ulazima wowote, mikutano ya vyama vya siasa iwe kipindi cha uchaguzi tu.
Ni kupotezeana muda tu.
Tatizo ni masheria mabovu uanyoruhusu maujingaujinga hayo.
Hata mabendera ya vyama hayana maana.
Viongozi wa chama wa kata,wilaya na mikoani ni mavyeo ya kipuuzi
Taifa linakuwa kama binadamu au mmea kwahiyo kila uchao kuna mambo mapya, unadhani kwanini CCM wanafanya hiyo mikutano si watulie tu wafanye kazi zao kama ni kutueleza wanachofanya vyombo vya habari vipo watatutangazia.
 
Unadhani saizi wabunge walio bungeni Kuna Cha maana wanafanya? Mikutano inasaidia waliochaguliwa miaka yote mitano kuwa busy) active kusolve matatizo ya wananchi, kuplan na kufikiria nje ya box namna ya kuboresha makwazo ya wananchi wasipokosolewa usitegemee chochote.
 
Habari Jf , Tuweke mbali uhalisia wa namna CCM inavyoingia madarakani .

Hivi kuna faida gani baada ya chama kimoja kushinda uchaguzi kwa mikutano ya vyama vya siasa kuendelea...
Simple, SIASA ni kazi! Kila wakati lazima ufanye kazi, ili upate ujira wako. Siasa/chama cha siasa mtaji wake ni watu, siasa ni iteraction na watu, lazima utafute watu, hivyo lazima kuimarisha upatikanaji wa wanachama kila dakika! Simple!

Nisamehe, it seems wewe ni darasa la saba with quite a low level of reasoning! ! Unisamehe!X3!
 
Simple, SIASA ni kazi! Siasa ni watu, hivyo lazima kuimarisha upatikanaji wa wanachama kila dakika! Siple!

Nisamehe, it seems wewe ni darasala saba with quite a low level of reasoning! ! Unisamehe!X3!
Hakuna namna nyingine ya kuwapata
 
Kwa mitazamo wangu mimi hakuna ulazima wowote, mikutano ya vyama vya siasa iwe kipindi cha uchaguzi tu.
Ni kupotezeana muda tu.
Tatizo ni masheria mabovu uanyoruhusu maujingaujinga hayo.
Hata mabendera ya vyama hayana maana.
Viongozi wa chama wa kata,wilaya na mikoani ni mavyeo ya kipuuzi
Umenena vyema mkuu, hawa wanasiasa wanaturudisha nyuma
 
Mtoa hoja hii be honest, wewe unaamini kuwa nchi hii tumekuwa tunafanya chaguzi za huru na haki toka tuwe huru? Nijibu hili maana ndio tutapata the way forward na mada yako, ccm inashinda uchaguzi kihalali kabisa, yaani watanzania wanakipa mandate ya kutawala nchi, sidhani kama CDM hata wakiitisha mikutano yao watafanikiwa na pia elewa ni wajibu wa political parties kujitahidi kunadi Sera zao, hii ni haki yao maana huwezi kusikia mtihani ni next week eti uanze kujisomea now!mitihani ni maandalizi ya muda mrefu, sawa na vyama vya siasa na chaguzi, yaani mkuu ungetembelea zambia/Botswana now uone demokrasia in the making kwenye hizo nchi.
 
Mikutano ya kisiasa ni ya MUHIMU Sana nchini.

(1) Ni chanzo kizuri cha kuamsha bongo za watu .Yaani kupitia mikutano hiyo watu huelimishwa mambo mbalimbali yahusuyo demokrasia na uchumi wa nchi hasa ambao hawakwenda shule madarasa ya ju .

(2) Mikutano husaidia watu kushare changamoto kiulahisi. Watu wanapo kutana wanawezesha kuzijua changamoto za mitaa au maeneo yao kiulahisi na kuziweka wazi mbele ya hadhira na kuwezesha serikali husika kuzijua na kuzifanyia kazi.

(3) Mikutano hiyo inasaidia watu kutua vihoro vyao ju ya changamoto na matatizo yaliyopo kwenye jamii. Vinginevyo watu watakaa na changamoto zao mioyoni na baadaye wanaweza kupandwa jazbaa na kuchukua hatua zisizo faa kwa serikali yao.

(4) Mikutano hiyo inasaidia vyama kueneza Sera na mipango yao . Ili wananchi wavijue vyama hivyo vizuri hasa Sera zao,Maona ,Mipango,na dhamira zso lazima kuwe na mahala pa kukutana na wananchi hadharani.

(5) Mikutano inatengeneza integration kwenye jamii .Watu wanajuana na kuaminiana zaidi wanapo kutana marakwamara.

Nk
 
Habari Jf, Tuweke mbali uhalisia wa namna CCM inavyoingia madarakani.

Hivi kuna faida gani baada ya chama kimoja kushinda uchaguzi kwa mikutano ya vyama vya siasa kuendelea...
Kazi ya chama cha siasa haiishii kwenye uchaguzi tu,miongoni mwa shughuli za vyama vya siasa ni pamoja na kushawishi wananchi kukiunga mkono muda wote wa uhai wa chama husika,kufuatilia mwenendo wa chama kilichopo madarakani na kutoa mrejesho kwa wapiga kura, kusajili wanachama wapya kadri inavyowezekana na kuibua na kuzisemea kero za wananchi.na njia pekee iliyo rahisi kwa vyama vya siasa ni kufanya mikutano ya hadhara ambayo ukutanisha chama cha siasa na wananchi.
 
Mtoa hoja hii be honest, wewe unaamini kuwa nchi hii tumekuwa tunafanya chaguzi za huru na haki toka tuwe huru?,nijibu hili maana ndio tutapata the way forward na mada yako, ccm inashinda uchaguzi kihalali kabisa, yaani watanzania wanakipa mandate ya kutawala nchi, sidhani kama CDM hata wakiitisha mikutano yao watafanikiwa na pia elewa ni wajibu wa political parties kujitahidi kunadi Sera zao, hii ni haki yao maana huwezi kusikia mtihani ni next week eti uanze kujisomea now!mitihani ni maandalizi ya muda mrefu, sawa na vyama vya siasa na chaguzi, yaani mkuu ungetembelea zambia/Botswana now uone demokrasia in the making kwenye hizo nchi
umeeleweka
 
Kazi ya chama cha siasa haiishii kwenye uchaguzi tu,miongoni mwa shughuli za vyama vya siasa ni pamoja na kushawishi wananchi kukiunga mkono muda wote wa uhai wa chama husika,kufuatilia mwenendo wa chama kilichopo madarakani na kutoa mrejeaho kwa wapiga Kura,kusajili wanachama wapya kadri inavyowezekana na kuibua na kuzisemea kero za wananchi.na njia pekee na iliyo rahisi kwa vyama vya siasa ni kufanya mikutano ya hadhara ambayo ukutanisha chama cha siasa na wananchi.
Hakuna namna nyingine ya kufanya zaidi ya mikutano
 
Elimu elimu elimu!! Usimwache akaenda zake!! Uchaguzi ni kilele cha mchakato, sio tukio lililosimama peke yake!! Ni aina hii ya vijana ndio tatizo la nchi hii - aina inayodhani uchaguzi ndio jambo pekee muhimu.
 
Back
Top Bottom