Je, kuna mtu yeyote aliyewahi kushuhudia na kuthibitisha uchawi? Njoo tuongee hapa!

Things are getting interesting..
Ngoja nisogee karibu,

Eheeee, so kwenye maugomvi ya USA-Israel na Iran nao wanaweza kutumia uchawi na problem ikawa solved.? πŸ€”

Kwamba uchawi unaweza kumponyesha au kumpa maradhi mtu? πŸ€”

Kwamba uchawi unaweza kusolve kesi (legal case)? πŸ€”

Kwamba uchawi unakusaidia kwenye mapenzi (sexual relationship)?

Kaaaazi kweli kweli... imani potofu hizi.

Eehee wewe huo uchawi umekusaidia nini?

Maana mie nikianza kuelezea vitu ambavyo sayansi imenisaidia tunaweza kuvi-count alfajir mpk jua linazama, na i can prove them all.

I repeat, mtu akishindwa kukielezea kitu, akishindwa kuking'amua, akishindwa kufanya reasoning, basi anatafuta excuse na kusema ni uchawi. Finding a scapegoat.
 
Hivi sababu zao za kutaka watu waamini uchawi upo ni nini? Wakinipa sababu moja tu ingekua poa sana
 
Hivi sababu zao za kutaka watu waamini uchawi upo ni nini? Wakinipa sababu moja tu ingekua poa sana
Nadhani ni wapigaji tu hawa, wanataka watu wajae hofu na kuleta taharuki (wana-create demand) kisha wawaambie watu wanalo suluhisho (wa-create supply)
ili wapige pesa.

Sabb majority ya sisi asians na africans, tunaamini sana katika hizi imani potofu.
Cheki mwaka huu watu tulivyoamini kwenye hili la wanaume kuibiwa nyeti kwa kuguswa tu bega, as simple as A,B,C......
 
mkoloni kaja na gun with gun powder.
 
πŸ‘†πŸ½That is a joke, right!?
Au ndo tangazo lako la kibiashara ili watu wakutafute, uwatapeli.

Daah, kwa akili hizi ndo tutegemee kulikomboa taifa kweli? πŸ€” safari ni ndefu aisee.

Mkuu, ila hatukukatii tamaa, usipoelewa ww, watalewa hata wajukuu zako. Tutafika tu mdogo mdogo.

Imagine, mtu wa mindset kama yako awe ni mtendaji kata, mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa, n.k. si ndo atazidi kuleta chaos kabisa.

Kwa hii mindset, hufai hata kuongoza japo ubolozi wa nyumba 10 tu, coz utatupoteza.

Anyway, tusiongee sana, wewe tafuta hiyo dawa ya kukukinga na panga, halafu mimi nije na panga (machete) tuone.
 
Upo nilishawahi kupigiwa lamli chonganishi na mama mmoja nilikutana nae njiani tu
 
Hujawahi kushuhudia mazingaombwe?
 
Mapenzi ,kesi ,ugomvi maradhi unathibisha vipi ni uchawi na sio sababu nyingine tu ambazo wewe huenda haujazijua ?
Hizo sababu zengine sijazijua kwa namna ipi? Mfano mwanamke mumewe kamuacha na kwenda kuishi na mwanamke mwengine kisha huyo mwanamke akataka kumrudisha huyo mumewe na kumfarakanisha na huyo mwanamke mwengine, sasa hilo suala likifanyika na kweli kila kitu kikawa kama alivyotaka je hapo ni sababu gani nyengine unaweza ukampa huyo mwanamke ili aache kuamini kuwa kilichotokea sio uchawi ni sababu nyengine?
 
Wewe ni mwanasayansi mkuu?
 
Hivi sababu zao za kutaka watu waamini uchawi upo ni nini? Wakinipa sababu moja tu ingekua poa sana
Mkuu hapa imeletwa mada tena na nyie wenyewe halafu unaona watu ndio wanawataka muamini uchawi?

Sasa hii mada ya nini mmeleta kama mnaona wenye mitazamo tofauti wanataka kuaminisha uchawi?
 
Unahisi wewe umeelimika sana mkuu eh?
 
mkoloni kaja na gun with gun powder.
Sasa ulitaka aje na matunguli?

Mkuu hiyo hoja yako ya wakoloni haina mashiko, yale yenye kuhusishwa na uchawi yaliyopo mnayapinga kwa hoja ya kwamba hakuna ushahidi hivyo yanaweza yakawa ni mambo mengine tusioyoyajua halafu hapo hapo mnaenda kuuliza mbona wachawi hawaibiki bank? Mbona wazee hawakutumia uchawi kuwashinda wakoloni? Ni mitazamo ya ajabu sana.
 
Reactions: Lax
Kama mtu yeyote humu haamini uchawi basi atembelee mpanda,sumbawanga, achukue mke wa mtu au binti tu amdanganye anamuoa kisha asimuoe aone kitakachomtokea. Hii si kwa kusimuliwa ni kwa kuona kwa macho yangu. UCHAWI UPO.
 
Kuna kijijin kimoja kipo chunya walimfukuza Mzee kijijini kisa mchawi akaenda kuishi nyuma ya mlima na familia yake wakaanzisha mshamba polini kweli wakaja watu WA madini wanachukua maeneo yote kuzunguka mlima baadae ya uthaminishaji Mzee na familia yake amekula karbia billion mbili Ivo πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mkuu hapa imeletwa mada tena na nyie wenyewe halafu unaona watu ndio wanawataka muamini uchawi?

Sasa hii mada ya nini mmeleta kama mnaona wenye mitazamo tofauti wanataka kuaminisha uchawi?
Hakuna uchawi ni ujinga unataka watu waamini sijui kwa maslahi gan
 
Duh tuishie hapa
 
Hakuna uchawi ni ujinga unataka watu waamini sijui kwa maslahi gan
Mkuu mimi siaminishi watu uchawi ukizingatia sio mimi niliyeleta hapa huu uzi, sasa badala ya kumwambia aliyeleta uzi wewe unaniambia mimi mchangiaji tu hapa kama wewe.

Hii ndio JF mkuu, kama ambavyo baadhi ya wauamini wa Mungu wamekuja kujulia humu watu ambao wanapinga katakata uwepo wa Mungu, hivyo nawe pia usione kero unapokutana na watu wana mitazamo na experiences tofauti na wewe.

Kama ulikuwa unadhania uchawi kwenye jamii zetu hizi ndio hizo story tu za kuibiwa nyeti basi fanya tena utafiti wako mkuu. Mimi naeleza nayoyajua wala sio lengo langu kutaka wewe uamini uchawi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…