Je, kuna mtu yeyote aliyewahi kushuhudia na kuthibitisha uchawi? Njoo tuongee hapa!

Mara ichane hela kidogo chuma ulete itashindwa, ukiona 10k zilizochanwa upande mmoja ujue ndio huo ujinga unaendelea
 
Reactions: Lax
Watu wanaenda kwa waganga wa mjini. Hawa janja janja wanaochuma dawa wakiwa na akili zao timamu, au ndo wale mikoba iliwachagua ila wakashindwa kuitumikia mwisho wa siku wanabaki hawana kitu zaidi ya kudanganya watu.
Ndio mkuu
 
Nimesoma koment karibia zote, nikagundua mnajibu kitu msichokijua. Yaani hapa ni sawa mtu ameenda maeneo fulani na kusema "mnasema mbuyu(mti) upo twende mkanioneshe" anafosi aoneshwe wakati hajaeleza/hajaelezwa mbuyu ni nini. Hapa labda ungekuja na kuuliza "uchawi ni nini?" ukielezwa uchawi ni nini, uliza "uchawi upo?" baada ya hapo sema "nioneshe au nithibitishie"

Au ungeelezea kwanza uchawi nini, ndio uulize kama upo kisha uombe kuoneshwa au kuthibitisiwa.

Yaani ni sawa na umeambiwa mti wa maembe(mwembe) upo hivi na hivi, kwahiyo kaangalie sehemu fulani kama upo. Ukienda unawakuta watu, basi unawaambia "kuna mti unaitwa mwembe upo hivi na hivi, je, upo" wakisema upo, waambie wakuoneshe.

Sasa we umekuja bila swali, umekuja huku unabisha. Ulidhani kitapata nini. Afu naona unauliza kitu hukijui. Kama we unaamini uchawi haupo, kwa nini unaomba uthibitisho wa kitu ambacho hakipo.
 
Waganga hao hao walioshindwa kujua ugonjwa wa ukimwi ni nini nakusema watu wamelogwa na kutupiwa majini au waganga wapi mkuu?

Uzuri mmoja hizo experience zote nimezipitia
Kama issue ya cholestrol tu mkuu na wanasayansi walikuwepo.
 
Unataka kuongea au uthibitisho wa kisayansi? Imani ya uchawi ina karne nyingi mzee, sasa usifikiri kipindi chote hicho kumekosekana kuhusishwa na matukio ya ajabu, kilichokosekana ni uthibitisho wa kisayansi hicho ndio kitu pekee cha kumaliza utata.
 
Reactions: Lax
Unajua kuwa Marekani wapo omba omba katika hiyo hiyo jamii iliyoendelea na niwazungu na wanaweza kukuomba mpaka wewe mmatumbi?
Najua hilo mkuu, je wewe unajua kuwa pia wapo wachawi kabisa huko Marekani na wana elimu zao safi kabisa?
 
Sasa mkuu hata tofauti ya mchawi na ghost haujui ila upo hapa kupinga haya mambo, unadhani sisi tunapata ugumu kiasi gani kujadiliana nanyi? Halafu hamtaki tutoe maelezo mnataka tuthibitishe moja kwa moja hayo msiyoyaelewa ila mnayapinga.
mimi mchawi na ghost tofauti yao siifahamu, maana kama ukikumbuka mpaka sasa hatiujapata muafaka mchawi ni nani na anafanya vitu gani.

kuna mdau hao anasisitiza anayafahamu haya mambo ila bado anagoma kueleza
 
Wanapingana wanasayansi kuhusu ukimwi.
Wanasayansi hawapingani kuhusu Ukimwi bali wapo wanasayansi wachache tena wasio expert wa ukimwi wanaopinga HIV kusababisha AIDS kama vile kulivyo na wanasayansi wanaopinga dunia kuwa duara(flat-earthers) au wanaopinga chanjo(anti-vaxxers) hata hivyo mwisho ya yote huwa kuna "scientific consensus" ya experts ambayo huwa ni muongozo wa dunia nzima. Hakuna Witchcraft consensus kuhusu jambo lolote uchawi ingawa binadamu wamekuwa wanaamini uchawi kwa maelfu ya miaka wakati kuna scientific consensus kuhusu Ukimwi uliogundulika miaka 47 tu iliyopita.
 
Mara ichane hela kidogo chuma ulete itashindwa, ukiona 10k zilizochanwa upande mmoja ujue ndio huo ujinga unaendelea
na wanaibandika pale nje wanasema chuma ulete akija akiona ipo pale anajua upo vizuri hapigi tukio, hizi story ni za kijinga sana
 
Oh! Kumbe kuna ujinga na huko? Nilidhani ulisema hakuna imani hizo huko sababu watu wameelimika na wameachana na huo ujinga.

Sasa mkuu una uhakika kweli hao wenye kuamini hayo mambo huko Marekani hawana elimu?
 
mkuu kama unafahamu uchawi ni nini lisaidie jukwaa, maana hii mada hua inafufuka kila baada ya muda na watu tofauti kwa muda mrefu sana humu jamvini.
 
bwenini huko huko kuna wadau walikua wanawanyoa wenzao alafu watu wakiwa wanawacheka asubuhi walionyolewa kwamba wachawi ndo wamefanya hivyo hadi wanyoaji nao wanaunga kwenye tela la kucheka
😄 🤣 😂
Umenikumbusha enzi hizo boarding.

Kuna ka mchezo, ilikua ukilala kizembe watu wanakuchora nyusi, ndevu na miwani kwa kutumia kiwi.

Sasa kuna siku dogo mmoja alichorwa bila kujijua akaenda mpaka assembly watu wamemkaushia
 
Reactions: Lax
Ubishi hauwezi kuisha kwa sababu ya kuhitajika ushahidi wa kisayansi na kinyume na hivyo ni tricks tu au mambo tusiyoyajua tu ila sio uchawi, kwahiyo mnaopinga uchawi mtabaki kuwa washindi milele.
Acha kulazimisha kwamba wachawi mmeambiwa mlete ushahidi wa kisayansi, leteni uthibitisho wa kifilosofia au ushahidi wowote badala ya kusema tu ni experience yenu binafsi. Ukisema umelogwa ndio maana ni magonjwa au masikini leta uthibitisho, ukisema imepoteza pesa kwa chuma ulete leta uthibitisho,.msije na vibes na experience zako binafsi tu ukasema ndio uthibitisho.
 
Oh! Kumbe hao wanasayansi wenye kupinga hiv kusababisha Aids ni kwa sababu sio expert wa ukimwi? Hahaha
 
Yeyote anayebisha kuwa hakuna uchawi aweke majina yake HALISI matatu na ya mama yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…