Je, kuna mtu yeyote aliyewahi kushuhudia na kuthibitisha uchawi? Njoo tuongee hapa!

Oh! Kumbe kuna ujinga na huko? Nilidhani ulisema hakuna imani hizo huko sababu watu wameelimika na wameachana na huo ujinga.

Sasa mkuu una uhakika kweli hao wenye kuamini hayo mambo huko Marekani hawana elimu?
Wakati mwingine huwa nasahau kama tunajadiliana na watu wenye uelewa haba/duni wa fikra. Nikisema Waislamu hawali kitimoto naongelea kwa ujumla wa dini ya Kiislamu, sasa usianze kusema mbona rafiki zako Waislamu Rashidi na Mwajuma huwa mnajumuika nao kula kitimoto, jiongeze. Uchawi umekuwepo Marekani na Ulaya kwa mamia ya miaka haiwezekani ukaisha kabisa wakakosekana hata watu wawili au watatu wanaomini hayo mauzauza yenu ya kichawi.

Tunaposema hukuna uchawi Magharibi tunamaanisha uchawi sio kitu mainstream tena bali ni fringe ideas/beliefs(Imani za ajabu) kwa watu wengi, sio kitu unachoweza kuzungumza comfortable mbele ya watu wengi mfano useme umelogwa usionekane una matatizo ya akili, kitu cha ajabu au kituko na watu wengi. Uchawi bongo ni jambo la kawaida (mainstream), mtu kukuambia amelogwa, amepata mafanikio kwa mganga, pete za majini, matambiko, limbwata na ujinga mwingine mwingi ni mambo ya kawaida kabisa na sehemu ya maisha yetu ya kila siku, uchawi unazungumziwa kuanzia ngazi ya urais, mawaziri, bunge mpaka serikali za mitaa, ni mjadala wa kawaida wa kila siku kwenye redio, tv, vijiweni, kwenye muziki unaimbwa n.k
 
Kwani Tanzania hakuna watu wanaoamini kuongea na wafu??
Huku wanaamini sana Mizimu(ancestors) ila wazungu wanaamini hata rafiki yako aliyefariki unaweza kufanya nae mawasiliano na hata mbwa wako sio binaadamu tu, ni imani za kitambo sana ila wazungu wanazifundisha hadi sasa.
 
naam wadau wanapanga kabisa alafu baadae inakua gumzo lisilo na maana
 
Hizi porojo zako za kijinga , sina mda wa kurudia kuzijibu , thibitisha uchawi upo, hauwezi sijakulazimisha
Raha sana mkuu, wewe wimbo wako huo huo "thibitisha" upo vizuri mtafiti.
 
Kwahiyo ukiwa mmarekani hauwezi kuwa mjinga
Sizungumzii wajinga, nazungumzia watu waliyoenda shule wakaelimika kama wewe au zaidi yako tena waliyozaliwa na kukulia katika jamii iliyoelimika.
 
Uthibitisho sio lazima uwe kisayansi, hata kwa philosophy unaweza thibitisha.
Ni lazima mkuu, hivi unajua mkuu imani ya uchawi haijaanza juzi ipo miaka mingi sana duniani ila hadi leo hakuna ushahidi wa uchawi?

Hivyo hakuna ushahidi mwengine ambao utaondoa utata zaidi ya ushahidi wa kisayansi. Mbona rahisi kueleweka hili mkuu.
 
Sasa kama hakujawahi kuwa na ushahidi au uthibitisho wa aina yoyote Ile wa uchawi kwa nini mtu mwenye akili ujisumbue na huo ujinga wa hearsay, vibes na experience binafsi za watu?!
 
Kila mtu ana experience yake mkuu kwenye haya maisha, nakumbuka rafiki yangu mmoja aliniambia yeye hajawahi kumshuhudia shoga(gay) live hivi kwa macho. Nilishangaa yani ukubwa wote huo na mashoga waliyojaa mjini bado tu haujawshi kushuhudia shoga live? Ndio sawa na mwengine ndani ya miaka 40+ katika maisha yake yeye huwa anaishia kusikia tu habari za kuhusishwa na uchawi kama hizo za kupotea kwa nyeti basi.

Mkuu nadhani hujaelewa vizuri, hata hicho unachosema kikafanyika na wewe ukaweza kujionea mwenyewe pesa kupungua bado itakuwa ni ushahidi binafsi na ushahidi binafsi sio tatizo upo sana tu mbona.
 
Reactions: Lax
Wewe umewahi kumshuhudia mtu asiye shoga (straight) live hivi kwa macho?
 
Reactions: Lax
Ili isiwe, ajitokeze mchawi afanye demo moja , uchawi kama upo sifikiri atakosekana humu , na kama upo wanaoufanya wanashindwa vipi kuthibitisha hapa
Unarudia yaleyale tu mkuu mimi nakueleza kwanini ila naona hunielewi.
 

Hizo story za Satellite, gravity, internet, micro organisms ni vitu vipo widely accepted kwa sababu vimekuwa normalized kwa sasa. Ila kuna kipindi hazokuwepo duniani

Mtu wa karne ya 5 ungemuambia kuhusu umeme, ndege kupaa angani ama satellite, angeona unamuambia vitu vya kufirika kwa sababu havipo katika uwepo wake.

Ndio ilikuwa point yangu hapo. Sio ACCEPTANCE ila EXISTENCE

Wewe umeiweka kwenye ACCEPTANCE and ADAPTION.

Kiufupi, hata katika business kuna innovators, hawa ni watu wanaoichukua na kuitumia bidhaa mwanzoni kabisaa, na kuna laggards, hawa wanatumia bidhaa ikishakuwa imetumika na watu wengi na mara nyingine imeshakuwa sehemu ya culture flani.

Wewe ni innovator kwa upande wa sayansi na unaviona vyote ni rahisi na umevikubali. Lakini kuna mtu madongo kuinama, ukimuambia kuna infrastructure ya umeme ambayo itatokea kwenye satellite. Atakushangaa kwa sababu pengine hata smartphone hajawahi kuitumia

Lakini mtu huyo huyo anaijua mitishamba kukuzidi na pengine, anajua akipata tatizo flani ataenda kwa mganga au kwenye visomo. Atapigwa makombe na atakaa sawa pasipo kutumia dawa za hospitali etc..

Huyu mtu ukimleta kwenye sayansi ataona unazungumza vitu vigumu kwake kwa sababu unatumia lugha ya sayansi kumuelezea lakini pia naye akikuambia yake, ndio hayo utaona pia ya kufirika kwa sababu unataka kutumia njia na maelezo ya kisayansi kuuelezea uchawi ulivyo.

Hawa watu wawili wakikaa sehemu moja si rahisi kukaa sawa..

Na unavyosema vitu kuwa tofauti kutokana na maeneo tofauti.

Je, kwani lazma kuwe na uniformity,

Kwani kuwepo kwa diversity katika kitu flani kilichopo katika sehemu tofauti na kuendeshwa na watu tofauti. Ni conclusion kuwa hiyo inconsistency inaonesha kuwa hicho kitu hakipo...

Kama dunia ilianza na gunpowder huko Asia, je ni sawa na teknolojia iliyotumika kutengeneza silaha za nyuklia

So kama teknolojia inaweza kutofautiana sehemu moja na nyingine. Japo principles na foundation yake inaweza kuwa sawa. Je kwa nini utegemee uchawi wa Wasukuma ufanane na uchawi wa wahausa ijapokuwa nia na msingi wake ni mmoja

Kwa nini unataka explanations za ushirikina ziwe sawa ilhali hata sayansi haipo sawa dunia nzima. Ndio maana kuna mataifa yanavumbua na mengine yanatumua tu
 
Mkuu tunaenda nao hivyo hivyo tu maana wenyewe wanaamini ni waerevu kuliko sisi, mtu hata hajui tofauti ya mchawi na ghost ila kakaza mishipa ya shingo anapinga nae uchawi hakuna, mwengine yeye anajua uchawi unafanyika na wachawi tu ila ni kinara wa kupinga na kutuona wengine wote wajinga na yeye ndio kafanya utafiti.
 
Sitaki kuamini nataka kujua kwa sababu na weza amini hata uongo tu, ndio maana yangu.
Kwa hiyo wewe huwa Unaamini tu unachokijua..

Je, wewe unakijua kila kitu kinachoaminiwa dunia hii?...
 
spiritual nayo kila mtu anamtazamo wake
Cha msingi unaamini ipo ama haipo.

Unajua hapa watu wanajaribu kuwa technical and safe ili tu wasiondoe imani walizozishikilia.

Unaweza kuwa na maoni tofauti kuhusu manifestation ya spiritual world. Lakini ukaamini ipo

Ni sawa na uchawi. Watu wengi tu wanaamini upo lakini wana maoni tofauti kuuhusu

Sasa kwa nini iwe ngumu kwa min -me ambaye haamini uchawi clearly. Na wala haofii lakini bado anashindwa kutoa neno moja tu kuwa.

SIAMINI kama spiritual world ipo. Mbona ni simple. Kigugumizi cha nini sasa hapo mkuu
 
Sayansi kujisahisha kwenye issue ya cholestrol ndio uthibitisho wa uchawi?
Sayansi haijisahishi, lakini nadharia za watu (na makosa ya mwanadamu) husawazishwa na kusahihishwa na sayansi yenyewe.

Wakati huo upotoshaji unafanyika wapo waliyopinga kama sasa hivi ambako wapo wenye kupinga hiv kusababisha Aids.
 
Mfano wako uko kichwa chini miguu juu. Binadamu wengi huko zamani walikuwa wanaamini uchawi lakini kadri muda unavyoenda Sayansi na teknolojia vikizidi kukua wengi wanazidi kuachana na imani za uchawi. Kwa upande mwingine binadamu wengi zamani walikuwa hawakubaliani na sayansi na reasoning ila kadri muda unavyoenda wengi wanahamia kuukubali Sayansi na Rational thinking.
 
So sad!
Binafsi nikiona mtu anashupalia na kukaza shingo kwamba kuna uchawi, huwa namwangaliaaaaaa yaani natamani hata nimtwishe gizo la miba.
 
Kwa hiyo wewe huwa Unaamini tu unachokijua..

Je, wewe unakijua kila kitu kinachoaminiwa dunia hii?...
Nitarudi mkuu, muda wa kulegeza ubongo na mvinyo kidogo sasa😅
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…