Basi kama mtu unanyolewa usiku kichwa kizima bila kujifahamu. Mtu kama huyu anaweza kutatuliwa hata marinda usiku kuchabwenini huko huko kuna wadau walikua wanawanyoa wenzao alafu watu wakiwa wanawacheka asubuhi walionyolewa kwamba wachawi ndo wamefanya hivyo hadi wanyoaji nao wanaunga kwenye tela la kucheka
mkuu unataka tuukubali tu uchawi kwa simulizi, licha ya kukueleza kwamba kwenye simulizi hizo zina utata, we unataka tuendelee tu kukubali.Kila mtu ana experience yake mkuu kwenye haya maisha, nakumbuka rafiki yangu mmoja aliniambia yeye hajawahi kumshuhudia shoga(gay) live hivi kwa macho. Nilishangaa yani ukubwa wote huo na mashoga waliyojaa mjini bado tu haujawshi kushuhudia shoga live? Ndio sawa na mwengine ndani ya miaka 40+ katika maisha yake yeye huwa anaishia kusikia tu habari za kuhusishwa na uchawi kama hizo za kupotea kwa nyeti basi.
Mkuu nadhani hujaelewa vizuri, hata hicho unachosema kikafanyika na wewe ukaweza kujionea mwenyewe pesa kupungua bado itakuwa ni ushahidi binafsi na ushahidi binafsi sio tatizo upo sana tu mbona.
Hivi ni nani anayewadanganyaga kwamba mitishamba sio Sayansi?Lakini mtu huyo huyo anaijua mitishamba kukuzidi na pengine, anajua akipata tatizo flani ataenda kwa mganga au kwenye visomo. Atapigwa makombe na atakaa sawa pasipo kutumia dawa za hospitali etc..
Huyu mtu ukimleta kwenye sayansi ataona unazungumza vitu vigumu kwake kwa sababu unatumia lugha ya sayansi kumuelezea lakini pia naye akikuambia yake, ndio hayo utaona pia ya kufirika kwa sababu unataka kutumia njia na maelezo ya kisayansi kuuelezea uchawi ulivyo.
majibu mengine sio lazima yatamkwe moja kwa mojaCha msingi unaamini ipo ama haipo.
Unajua hapa watu wanajaribu kuwa technical and safe ili tu wasiondoe imani walizozishikilia.
Unaweza kuwa na maoni tofauti kuhusu manifestation ya spiritual world. Lakini ukaamini ipo
Ni sawa na uchawi. Watu wengi tu wanaamini upo lakini wana maoni tofauti kuuhusu
Sasa kwa nini iwe ngumu kwa min -me ambaye haamini uchawi clearly. Na wala haofii lakini bado anashindwa kutoa neno moja tu kuwa.
SIAMINI kama spiritual world ipo. Mbona ni simple. Kigugumizi cha nini sasa hapo mkuu
Sasa mbona unajiingiza kwenye ubishani wa vitu usivyovielewa na mbaya zaidi unadai uthibitisho kwa kitu ambacho hukielewi? Inawezekanaje hiyo?mimi mchawi na ghost tofauti yao siifahamu, maana kama ukikumbuka mpaka sasa hatiujapata muafaka mchawi ni nani na anafanya vitu gani.
kuna mdau hao anasisitiza anayafahamu haya mambo ila bado anagoma kueleza
Na wana elimu sio kwamba wanaamini sababu ya uduni wa elimu.Wapo watu wanao amini uchawi
kwani mkuu wewe hivi vitu navielewa? kama ndio tueleze. kama hapana mimi na wewe ni walewaleSasa mbona unajiingiza kwenye ubishani wa vitu usivyovielewa na mbaya zaidi unadai uthibitisho kwa kitu ambacho hukielewi? Inawezekanaje hiyo?
Hebu toa mfano ni kwa namna gani mtu anaweza kuthibitisha uchawi pasina kuwepo utata na uthibitisho huo usiwe wa kisayansi?Acha kulazimisha kwamba wachawi mmeambia mlete ushahidi wa kisayansi, leteni uthibitisho wa kifilosofia au ushahidi wowote badala ya kusema tu ni experience yenu binafsi. Ukisema umelogwa ndio maana ni magonjwa au masikini leta uthibitisho, ukisema imepoteza pesa kwa chuma ulete leta uthibitisho,.msije na vibes na experience zako binafsi tu ukasema ndio uthibitisho.
Hiyo concept naielewa vizuri kwa sababu hata utengenezaji wa gongo ni sayansi kwa sasabu inarandana na kitu ambacho umefundishwa kwenye chemistry.Hivi ni nani anayewadanganyaga kwamba mitishamba sio Sayansi?
Kuna tofauti kubwa mno kati ya Ramli na Mitishamba.
Mkuu, nashauri urejee maana ya Sayansi ni nini. Sabb unachanganya mafaili
Watu wakisikia Sayansi, wanawaza sijui mzungu, sijui miformula mizito mizito. Hii nayo ni wrong perspective.
Hivi unajua kwamba:-
-hata kutengeneza Mkaa tu ile sayansi.?
-kutengeneza pombe hata hizo unazoziona za kienyeji, hiyo ni Sayansi.
-kutengeneza sabuni, that is science.
Kama ukitulia na ukirejea definition ya sayansi, utanielewa.
ila uchawi ni upuuzi, ni lame excuse inayotumiwa na watu pindi mtu akishindwa kuking'amua kitu, kukielezea, kukielewa, pale ambapo critical thinking na reasoning zikiisha anajifichia humo kwa kusoma ni uchawi, Finding a scapegoat
Mkifikia muafaka mtaniita nione uchawiNa wana elimu sio kwamba wanaamini sababu ya uduni wa elimu.
na mtu yupo serious na anachokitype. Hahah!Duh tuishie hapa
Mfano wako uko kichwa chini miguu juu. Binadamu wengi huko zamani walikuwa wanaamini uchawi lakini kadri muda unavyoenda Sayansi na teknolojia vikizidi kukua wengi wanazidi kuachana na imani za uchawi. Kwa upande mwingine binadamu wengi zamani walikuwa hawakubaliani na sayansi na reasoning ila kadri muda unavyoenda wengi wanahamia kuukubali Sayansi na Rational thinking.
Mkuu huo mtazamo wa kwamba uchawi ni issue ya kurogana tu huo ni mtazamo wako wewe, mimi naposema wazungu wanaamini hayo mambo naelewa vizuri kwamba kule hakuna sana hayo madai kurogana au imani potofu zakuhusishwa na uchawi. Ila bado wanaamini mambo mengi sana sio uchawi tu pamoja na kuelimika kwao.Wakati mwingine huwa nasahau kama tunajadiliana na watu wenye uelewa haba/duni wa fikra. Nikisema Waislamu hawali kitimoto naongelea kwa ujumla wa dini ya Kiislamu, sasa usianze kusema mbona rafiki zako Waislamu Rashidi na Mwajuma huwa mnajumuika nao kula kitimoto, jiongeze. Uchawi umekuwepo Marekani na Ulaya kwa mamia ya miaka haiwezekani ukaisha kabisa wakakosekana hata watu wawili au watatu wanaomini hayo mauzauza yenu ya kichawi.
Tunaposema hukuna uchawi Magharibi tunamaanisha uchawi sio kitu mainstream tena bali ni fringe ideas/beliefs(Imani za ajabu) kwa watu wengi, sio kitu unachoweza kuzungumza comfortable mbele ya watu wengi mfano useme umelogwa usionekane una matatizo ya akili, kitu cha ajabu au kituko na watu wengi. Uchawi bongo ni jambo la kawaida (mainstream), mtu kukuambia amelogwa, amepata mafanikio kwa mganga, pete za majini, matambiko, limbwata na ujinga mwingine mwingi ni mambo ya kawaida kabisa na sehemu ya maisha yetu ya kila siku, uchawi unazungumziwa kuanzia ngazi ya urais, mawaziri, bunge mpaka serikali za mitaa, ni mjadala wa kawaida wa kila siku kwenye redio, tv, vijiweni, kwenye muziki unaimbwa n.k
Mkuu kwa unavyoelewa wewe watu huwa wanaenda kwa waganga kufanya nini?Sasa kama hakujawahi kuwa na ushahidi au uthibitisho wa aina yoyote Ile wa uchawi kwa nini mtu mwenye akili ujisumbue na huo ujinga wa hearsay, vibes na experience binafsi za watu?!
Sipo hapa kukufanya ukubali uchawi na kama wewe upo ili kutufanya tupinge uchawi basi mngekuwa mnatupa elimu ili nasi tuelewe kuwa hayo tuliyoyaona sie kama uchawi si uchawi bali ni kitu gani. Mada imeletwa na nyie wenyewe ila tukijadili tunaonekana tunawalazimisha kuwa wachawi wengine wanakasirika hadi wanatamani kutupiga ngumi kama tungekuwa karibu yao, sasa sijaelewa huwa mnaleta hizi mada ili iweje?mkuu unataka tuukubali tu uchawi kwa simulizi, licha ya kukueleza kwamba kwenye simulizi hizo zina utata, we unataka tuendelee tu kukubali.
Muafaka ni kwamba hakuna uchawi kwa sababu hakuna uthibitisho wa kisayansi, ushahidi binafsi hausaidii kuondoa utata wa uwepo wa uchawi ndio maana uchawi hadi leo unaonekana hauna ukweli kwa sababu hakuna ushahidi wa kisayansi.Mkifikia muafaka mtaniita nione uchawi
Ushirikina hauna formula wala principles zake, coz vitu vyenye formula na principles vinathibitishika beyond reasonable doubt.Kama ilivyo chemistry, unachanganya A, B na C Kupata product flani.. Ndivyo ushirikina ulivyo una formular na principles zake
So, unatuaminisha wewe ulitumia ufahamu wako? Wakati kwenye post hapo chini umekiri kwamba ndo ulikuzwa hivyo kwenye kuamini uchawi na ushirikina.Kiufupi wewe unaamini kile unachoaminishwa na unakataa kile ambacho hujaaminishwa. Kiufupi, hutumii ufahamu wako binafsi ila unasubiri ufahamu wa mtu mwingine ukuthibitishie, na mbaya zaidi asipoweza na hutoweza...
Hiyo ndio tofauti yangu mimi na wewe.. wewe unaamini sayansi ni perfect kwenye kuthibitisha kila kitu ila mimi naamini kuna vitu haiwezi kuthibitishwa kwa sababu yenyewe ni evolving thing.
As you said, "kwa makuzi yako, utaendelea kuamini uchawi na ushirikina"Mimi kwa makuzi na experience yangu nitaendelea kamini uchawi na ushirikina vipo.
Sijui.Hebu toa mfano ni kwa namna gani mtu anaweza kuthibitisha uchawi pasina kuwepo utata na uthibitisho huo usiwe wa kisayansi?
Baada ya maendeleo makubwa ya sayansi binadamu wengi wameachana na imani za kishirikina, uchawi na hata dini kwa upana na kwa ujumla katika jamii. Kwa sasa kuna watu wengi kwenye dini za Ukristo na Uislamu ambao hawaamini uchawi(which is a contradiction), hata hivyo wapo. Dunia ya leo Kuna binadamu wengi zaidi ambao ni atheists na agnostics kuliko kipindi chochote na hii ni kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia. Binadamu wengi wanaoamini uchawi, ushirikina na dini wanapunguza zaidi, hii ni fact, hii ndio hoja kuu, mengine ni gumzo tu baada ya habari.Again "general assumptions"...
Uchawi versus Science
Sayansi nyingi zilizokataliwa si hata kwa bases za uchawi bali pale zinapokuwa contradicted na imani za watu binafsi. Hususani za kidini . . Rejea Galileo incident
Lakini ukiangalia jamii za Misri, kigiriki na hata Asia ambapo gunduzi za mwanzo zilifanyika. Hiyo sayansi haikupingwa bali kuwa adapted kirahisi.
By the way. Sioni kama unanijibu zaidi ya kuchukua kipande kidogo cha explanations zangu na kuonesha nachofikiria sicho na kuongezea maneno ya kunidogosha ili nijione nafikiria upumbavu.
I respect you mkuu na huwa sifanyi argument ila discussions. Ukiweza discuss vitu kama descently, nitajibu
Again najua kitu cha kwanza kitakuwa ni kuattack hiyo paragraph ya nyuma kwa sababu hiyo ndio escape yako. Good day🙏🏽🙏🏽
Tiba za Mitishimba ni dawa za Sayansi(iliyo duni). Miarobaini, Mikaratusi, Quinine na majani mengine mengi ni ingredients za dawa mbalimbali, watu wa zamani waliokuwa wanatumia bila uelewa wa Sayansi haibadilishi na kuvifanya hivi vitu hivyo kuwa ni uchawi. Kama ilivyo jambo lolote lenye maslahi halikosi utapeli au ujanja ndani yake pamoja na religious/beliefs influence, waliibuka watu wakijidai wanatamka maneno fulani wakati wanawapa watu mitishimba wakajipatia nafasi katika jamii kama waganga wa kienyeji(wa kiroho) lakini hakuna chochote wanachoongeza katika hayo matibabu zaidi ya 'Placebo effect"Lakini mtu huyo huyo anaijua mitishamba kukuzidi na pengine, anajua akipata tatizo flani ataenda kwa mganga au kwenye visomo. Atapigwa makombe na atakaa sawa pasipo kutumia dawa za hospitali etc..
Huyu mtu ukimleta kwenye sayansi ataona unazungumza vitu vigumu kwake kwa sababu unatumia lugha ya sayansi kumuelezea lakini pia naye akikuambia yake, ndio hayo utaona pia ya kufirika kwa sababu unataka kutumia njia na maelezo ya kisayansi kuuelezea uchawi ulivyo.
Hawa watu wawili wakikaa sehemu moja si rahisi kukaa sawa..
Na unavyosema vitu kuwa tofauti kutokana na maeneo tofauti.
Je, kwani lazma kuwe na uniformity,
Kwani kuwepo kwa diversity katika kitu flani kilichopo katika sehemu tofauti na kuendeshwa na watu tofauti. Ni conclusion kuwa hiyo inconsistency inaonesha kuwa hicho kitu hakipo...
Kama dunia ilianza na gunpowder huko Asia, je ni sawa na teknolojia iliyotumika kutengeneza silaha za nyuklia
So kama teknolojia inaweza kutofautiana sehemu moja na nyingine. Japo principles na foundation yake inaweza kuwa sawa. Je kwa nini utegemee uchawi wa Wasukuma ufanane na uchawi wa wahausa ijapokuwa nia na msingi wake ni mmoja
Kwa nini unataka explanations za ushirikina ziwe sawa ilhali hata sayansi haipo sawa dunia nzima. Ndio maana kuna mataifa yanavumbua na mengine yanatumua tu