Je, kwa mshahara wa Shilingi 310,000 unaweza kuishi Dar es Salaam?

unajua hata bodaboda au bajaj huwa wanaingiza pesa kutokana na mahali walipo mkuu.
Bodaboda anaeingia hadi town na anafanya kazi sehemu ambapo watu ni middle income anaingiza pesa nzuri kuliko hawa wanaofanyia kazi sehemu ambazo watu wengi ni kipato cha chini maana kupata route za 5000 - 10000 ni ngumu

kingine mtu mwenye bodaboda yake anaweza akaingiza pesa nzuri tofauti na anaetakiwa kupeleka hesabu kwa boss.. Ndo maana nilisisitiza hapo mkuu
 
Hahahah hesabu za online hizo mambo kwa ground ni mtiti
 
Ni kweli japo kwangu mimi watu wenye kipato cha chini ni biashara yangu na boda boda ndio watu wanaojibu maswali mengi ya kwangu kuhusu kipato kwa kuwa natumia usafiri wao kila siku. hivyo ninachokueleza kwa wao kupata hizo fedha inawezekana haijalishi yuko wapi ili mradi azingatie masharti na hasa wenye umri kati ya miaka 20-35
 
Tatizo msharaha ni fixed ,ukitilea mfano bodaboda ,muuza kandoro unakosea sana.Kuna bodaboda anaishi nyumba ya 150k muuza kandoro anakwambia kwa siku anaondoka na mpk 30k faida sometime inategemea na hali ya hewa (jua).
Kila kitu kinategemea location mkuu

sikatai kuna watu wanaingiza hela nzuri kwa kazi hizihizi za kawaida ila inategemea na lokesheni aliyopo .. Wa kariakoo si sawa na wa temeke au mbagala au makumbusho

kingine mkuu kama hao watu wangekuwa wanaingiza hiyo wastani wa laki 9 kwa mwezi, sidhani kama wangeendelea na hizo biashara maana kama kuna watu wanajua channel ya hela kwa kazi ambazo hazihitaji mtaji mkubwa bhasi ni wa hali ya chini
 
sawa mkuu naheshimu mawazo yako
 

Imebidi nicheke tu
 
Mimi kwa 310K naishi Dar bila zengwe.
 
70K Chakula Cha Mwezi Mzima.

20K Vocha.

40K kwa wazee.

50K nauli ya mizunguko ya mwezi.

Inayobaki ni ya kusave na pocket money.
Kuonga unaonga kiasi gani kwa mwezi?
Bia ngapi kwa wiki unakunywa au wewe msabato??
Mbona umesahau kuweka kwenye bajeti hayo
 
Kuonga unaonga kiasi gani?
Bia ngapi kwa wiki unakunywa au wewe msabato??
Mbona umesahau kuweka kwenye bajeti hayo
Ooh hapo kweli.

Mimi sinywi wala sivuti.

Aina ya wanawake ninaoruka nao kuhonga huja in terms of outing, kuumwa, pesa ya kula n.k nadra kulipishwa kodi. So pesa inayobaki inacover hapo.
 
Habari wadau!

Ebu nisaidieni hivi kweli 310,000/= inatosha mtu kufanya kazi na kuishi DAR au unatakiwa kuwa na miundombinu mingine?
Huwa najiuliza wale mama lishe huwa wanapata Tsh ngapi kwa mwezi.
Ghafla imeniijia sura ya yule mdada mpika vitumbua aliyekuwa na mtoto kapanga nyumba Ubungo, kuna mwamba mlinzi alikuwa analipwa 250k lakini aliufurahia sana ule mshahara ungemwezesha kuishi kwa raha kidogo mjini ana watoto wawili lakini wanaishi bwana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…