Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Haya ni maneno ya maana sana mkuu. Kama wanadamu tungeyazingatia na kuishi maisha mazuri ya kuwajali wengine, kupendana na kuheshimiana, dunia ingekua sehemu nzuri sana ya kuishi whether kuna Mungu au la.Haya maneno ya Marcus Aurelius ni mazuri sana;
"Live a good life. If there are gods and they are just, then they will not care how devout you have been, but will welcome you based on the virtues you have lived by. If there are gods, but unjust, then you should not want to worship them. If there are no gods, then you will be gone, but will have lived a noble life that will live on in the memories of your loved ones.”
Wa kuthibitisha nini mkuu?Unao uthibitisho?
Mfano wa misimamo gani atheists au agnostics huwa wanakuwa nayo na wanalazimika kuitetea kwa kwa hali yoyote?Sioni tofauti sana ya mtu ambaye anaamini Mungu/dini na mtu ambaye ameacha kuamini Mungu anaenda kuwa atheist au Agnostic, kwa sababu huko pia kuna mitazamo ambayo atajikuta a alazmika kuifuata na kuisimamia.
Watu wa aina hiyo ukijadiliana nao unaona kabisa jinsi wanavyokazana kutetea hiyo misimamo kwa hali yeyote ile yani kuna mambo unaona kabisa wanalazimika kupinga kwa sababu tu yeye ni atheist.
Wafia dini kazi mnayo!Nashuhudia kuwa ; hakuna mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah na Muhammad ni Mtume wake.
Kuna tofauti gani kati ya mola na Allah?Nashuhudia kuwa ; hakuna mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah na Muhammad ni Mtume wake.
Yuko wapi?Mungu yupo
Hizo ni kauli mbiu (motto ) tu za dini zisikuchanganye ukajihisi kana kwamba wewe ndio special sana na kwamba wenzako ni inferior kwasababu wamekosa kauli mbiu kama hizo.Nashuhudia kuwa ; hakuna mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah na Muhammad ni Mtume wake.
Pointi sio kuepuka mitazamo.Sioni tofauti sana ya mtu ambaye anaamini Mungu/dini na mtu ambaye ameacha kuamini Mungu anaenda kuwa atheist au Agnostic, kwa sababu huko pia kuna mitazamo ambayo atajikuta a alazmika kuifuata na kuisimamia.
Watu wa aina hiyo ukijadiliana nao unaona kabisa jinsi wanavyokazana kutetea hiyo misimamo kwa hali yeyote ile yani kuna mambo unaona kabisa wanalazimika kupinga kwa sababu tu yeye ni atheist.
Umeeleza vizuri, hiyo definition ndio aina ya misimamo ambayo nazungumzia kwa maana ukitaka kujitambulisha kama atheist basi utalazimika kufuata hiyo misimamo. Ukiangalia hivyo vitu kwenye hiyo definition utaona ni vitu tofauti tofauti kwa maana mtu anaweza kuamini hiki na asiamini chengine ila atheist analazimika kupinga vyote. Lakini mtu anaweza kuamini Mungu ila asiamini katika miungu, mfano daktari anaweza kuamini Mungu ila akawa haamini katika uchawi na miujiza.Pointi sio kuepuka mitazamo.
Pointi hapa ni kuepuka uongo.
Dhana ya uwepo wa Mungu ni uongo wa wazi.
Atheist ni ukosefu wa imani ya Mungu/Miungu na maswala yote ya supernatural.
Kwa hiyo kama unazungumzia misimamo wala hauhitaji uwe na mambo mengi zaidi ya kuzingatia hiyo definition hapo juu.
Mfano uchawi au miujiza, ni mambo ambayo atheist atapinga kwa hali yeyote hata akiona kwa macho hivi yupo radhi akubali kwamba hana majibu ya kuelezea hicho alichokiona ila ataendelea kukataa kuwa huo si uchawi au miujiza kwa sababu tu anatetea msimamo wa kupinga mambo yote ya supernatural.Mfano wa misimamo gani atheists au agnostics huwa wanakuwa nayo na wanalazimika kuitetea kwa kwa hali yoyote?
Yesu pia Amani iwe juu yake nakiri kuwa ni Nabii wa Allaah.Wafia dini kazi mnayo!
Ngoja waje watu wa Yesu wakwambie habari zake
Wewe ndio huelewi, atheists wanataka uthibitisho.Mfano uchawi au miujiza, ni mambo ambayo atheist atapinga kwa hali yeyote hata akiona kwa macho hivi yupo radhi akubali kwamba hana majibu ya kuelezea hicho alichokiona ila ataendelea kukataa kuwa huo si uchawi au miujiza kwa sababu tu anatetea msimamo wa kupinga mambo yote ya supernatural.
Kuwa Atheist sio mpaka ujue Atheist ni nini.Umeeleza vizuri, hiyo definition ndio aina ya misimamo ambayo nazungumzia kwa maana ukitaka kujitambulisha kama atheist basi utalazimika kufuata hiyo misimamo. Ukiangalia hivyo vitu kwenye hiyo definition utaona ni vitu tofauti tofauti kwa maana mtu anaweza kuamini hiki na asiamini chengine ila atheist analazimika kupinga vyote. Lakini mtu anaweza kuamini Mungu ila asiamini katika miungu, mfano daktari anaweza kuamini Mungu ila akawa haamini katika uchawi na miujiza.
Sasa unakuta mtu alikuwa anaamini katika Mungu ila ikatokea kuja kuona kuwa imani ya Mungu si ya kweli tena unaweza kukuta shida ilikuwa ni mafundisho ya hiyo dini kuhusu Mungu ndio yamemfanya aone habari za Mungu si za kweli, ila sasa mtu huyo anafanya uamuzi kujiingiza kwenye atheism ambapo ghafla anakuwa na ukosefu kabisa wa imani si ya Mungu tu bali pamoja na supernatural.
Na kibaya mtu kuwa atheist basi anaamini ana akili sana kuliko wenye kuamini Mungu na supernatural na kwamba huchukulia atheism ndio ukweli japo kuna watu hutoka huko.
Usituwekee fikra zako potofu vichwani mwetu kwasababu tu ya inferior yakoNa kibaya mtu kuwa atheist basi anaamini ana akili sana kuliko wenye kuamini Mungu na supernatural na kwamba huchukulia atheism ndio ukweli japo kuna watu hutoka huko.
Uchawi ni nini?Mfano uchawi au miujiza, ni mambo ambayo atheist atapinga kwa hali yeyote hata akiona kwa macho hivi yupo radhi akubali kwamba hana majibu ya kuelezea hicho alichokiona ila ataendelea kukataa kuwa huo si uchawi au miujiza kwa sababu tu anatetea msimamo wa kupinga mambo yote ya supernatural.
Hata huko kusema atheists wanataka uthibitisho ukianglia vizuri ni kwamba wanajizuia kwa kutokukubali au kutaka kujifunza chochote kwa kigezo hakuna uthibitisho, ukiangalia hata hiyo mifano uliyoiweka na jinsi ulivyoeleza ni wazi ni mambo ambayo unapinga kwa sababu ya kusimamia huo msimamo wa kwamba hakuna uthibitisho ila si kwamba unapinga kwa sababu unaelewa ukweli wa hayo mambo.Wewe ndio huelewi, atheists wanataka uthibitisho.
Kwa mfano hakuna hata mtu mmoja amewahi kuona mtu mchawi ameanguka na ungo kutoka angani au hata video moja inonyesha mtu akianguka kwa ungo. Kila mara ukisikia story ya mtu kuanguka na ungo ni kwamba mtu tayari amekutwa yuko chini na majivu na ungo wake. Sasa mtu mwenye akili hawezi kuamini tu kirahisi hivyo.
Mfano Mtu akiugua, au akipata ajali akafa huwa kuna uthibitisho ambao utonyesha kama ni bacteria, virusi, cancer cells, jeraha n.k ambavyo vitakuwa vimesababisha kifo na maelezo yanaeleweka. Sasa utakuta mtu anasema alikufa akafufuliwa, au alikuwa anaumwa ukimwi akaponywa ukimuuliza cheti cha daktari kuonyesha alikufa au alikuwa unaumwa ukimwi kiko wapi hana.
Mtu anasema alienda kwa mganga akapewa dawa akawa tajiri, unamuuliza ulila ukaamka ukawa tajiri anakuambia hapana anaanza kukupa story jinsi alivyofanya kazi kwa bidii na muda mrefu alipotoka kwa mganga. Sasa hapo unathibitishaje ni dawa ya mganga na sio juhudi zake za kazi ja bahati nyingine?!
Nachoeleza ndio uhalisi kwa ushahidi wa aina ya majadiliano yenu yanavyokuwa huwa mnajionyesha wazi, mnawachukulia wanaoamini Mungu ni kama watu wasio na maarifa ya kutosha na wasiofuata sayansi. Mbona lipo wazi hili halifichiki naeleza ukweli kama ambavyo nawe unaeleza unachoona ni ukweli.Usituwekee fikra zako potofu vichwani mwetu kwasababu tu ya inferior yako
Hata waislamu wengi wanaamini kuwa wakristo wanawaona waislamu hawana akili kwasababu wamewekeza nguvu kwenye madrasa kuliko ku focus na elimu dunia.
Kwa hiyo usijaribu kuweka mipaka ya kuzuia ukosoaji pale ambapo mambo ya kijinga yanafanyika kwa kufikiri tutafumbia macho ujinga kuofia tutaonekana tuna akili kuliko nyie.