Je, kweli ni bora kuamini Mungu yupo halafu siku ya mwisho usimkute, kuliko kutoamini halafu ukamkuta?

Je, kweli ni bora kuamini Mungu yupo halafu siku ya mwisho usimkute, kuliko kutoamini halafu ukamkuta?

Mungu mkuu ni utambulisho wa kila dini katika kuelezea sifa za Mungu wanaye muabudu.

Kwahiyo wanao abudu Ng'ombe husema Ng'ombe ndio Mungu Mkuu ? Au wanao abudu sana husema hilo ? Inaonekana hujui maana ya Mungu Mkuu.
Hata zile dini za kale ambazo ni kongwe kuliko yako kama Sumerian zilikuwa zina amini Mungu zaidi ya mmoja, kwenye hiyo miungu zilikuwa na Mungu mkuu aliyekuwa anaitwa Enki ambaye ni mhusika na maswala hayo ya uumbaji.

Kijana usipate tabu, ndio maana nakwama huna misingi ya kielimu. Hakuna dini kongwe kuzidi Uislamu.

Hizo unazo dai kuwa ni kongwe, weka historia zake na utuambie machimbuko yake.
Kwa hiyo sio kweli kuwa dini zenye kuabudu Mungu zaidi ya mmoja zinaamini nje ya imani yao kuna Mungu muumba wa ulimwengu kwasababu tumeona hata wao pia katika orodha ya Miungu wao wanaye huyo Mungu ambaye ni muumba.

Marejeo yako ni wapi ? Mimi no mekutolea mfano wa makafiri wa Makkah na wasio kuwa wao. Wasome Mayahudi na kufuru zao.
Sio kweli kuwa tamko Mungu ni tamko linalomaanisha ni Mungu pekee anayepaswa kuabudiwa.

Haya umeyapata wapi ? Umesoma kwenye Kamusi gani ? Soma Kamusi za lugha uone zinakwambia nini kuhusu tamko Mungu. Usilete stori za vijiweni hapa. Unatakiwa ujue ya kuwa tunapo wazungumza miungu wengine since kwa maana ya halisi ya Mungu bali katika mlango wa kuwahabarisha na kuwajuza watu.
Hii itabaki kuwa ni maoni yenu binafsi kulingana na lenye mipaka isiyovuka imani yenu hivyo haiwezi kuwa ni tamko lenye kujumuisha imani zingine na ndio maana tumeweza kuona imani zingine zikiwa na Mungu zaidi ya mmoja na wote wakiabudiwa.

Kijana huwa napenda kujadili na watu wenye elimu na kuyajua mambo, leta maana ya Mungu ya Kamusi. Usilete stori za vijiweni.
Kusema imani ya wengine sio sahihi, hauwezi kuwa sahihi. Kwasababu hauwezi kutumia sheria za dini yako kukosoa dini za wengine.

Lazima nitumie dini yangu sababu ndio uhalisia wenyewe, ndio maana hata hizi Imani huwa tunazihakiki. Dini ya kweli ambayo ni marejeo ina sifa zake anuai, kwanza lazima iendane na maumbile.
Hata hizo dini zinaweza kukuambia kuwa dini yako ni ya uongo kwasababu wanazoziona zinahitilafiana na kanuni za dini yao.

Kusema sio hoja, Cha msingi ni kuthibitisha ukweli wa dini yao, sababu haya mambo yanajadilika na vitabu vipo na historia zimedhibitiwa.
 
Kufanya maelezo marefu yawe mafupi

Nipe source ya hiyo tafsiri kwanza nisome nihakikishe kabla hatujafika mbali.

Nataka hiyo ambayo haijatolewa na wazee wako wa zuoni.

Hiki ulichokiandika kwanza umekisoma na kukielewa ?

Sasa ambayo haijatolewa na wanazuoni wangu si usilete wewe mzee ?

Kwahiyo kumbe unajadili jambo huna elimu nalo na bado unabisha ? Acha kupotezea watu muda kijana.
 
Ulisema kuna ya wanazuoni na kiarabu, sasa hiyo tafsiri uliyoweka inatoka kwenye chanzo kipi kati ya hivyo viwili?

Au ni mchanganyiko?
Ya wanazuoni na Kiarabu ndio nini ?

Soma nilichokiandika na nimekitolea ufafanuzi mzuri sana.
 
Kwahiyo wanao abudu Ng'ombe husema Ng'ombe ndio Mungu Mkuu ? Au wanao abudu sana husema hilo ? Inaonekana hujui maana ya Mungu Mkuu.
Kuna mambo mengi huyajui kwasababu ya kutofuatilia.

Umetaja Mungu Ng'ombe ambaye kimsingi ni Mungu wa imani ya Kihindu.

Lakini kitu ambacho umeshindwa kukielewa ni kutonielewa kwenye maelezo yangu niliyoandika hususan pale nilipopinga kauli yako kuwa Mungu mkuu pekee ndio anayepaswa kuabudiwa.

Wahindu wanaamini kwenye Miungu yani Mungu zaidi ya mmoja kama ilivyo tu kwa Sumerian.

Kwenye hiyo Miungu kila Mungu ana department yake ambayo amehusishwa nayo.

Na mmoja wa hiyo Miungu ni pamoja na huyu Mungu Ng'ombe ambaye wewe umemuwekea kama mfano na jina lake anaitwa Kamadhenu au surabhi.
1734558810046.jpeg

Wahindu huamini kuwa Miungu yao au viumbe wa Mungu kwa imani yao huchukua maumbo ya ng'ombe.

Hivyo wao wanawapa heshima hao wanyama kwasababu wanawaona kama ni sehemu ya baraka.

Huyu ni Mungu ambaye department yake inahusika na ishu ya uponyaji na maswala mengine ya kilimo.

Kwenye hiyo hiyo dini ya Kihindu ambayo kuna Mungu Ng'ombe pia wanaye Mungu Brahma ambaye huyu department yake ni maswala ya uumbaji.

1734558857711.jpeg

Kwa hiyo ukisikia kuwa kuna jamii zinaabudu Mungu paka au fisi haina maana hawana backup ya Mungu muumba.

Wala haina maana kama wanaamini Mungu wa dini yako ndio muumba.

Wao wana multiple Gods, na hao wanayama ni wawakilishi tu yani ni kama nyie mnavyosema mitume au manabii.
 
Kijana usipate tabu, ndio maana nakwama huna misingi ya kielimu. Hakuna dini kongwe kuzidi Uislamu.

Hizo unazo dai kuwa ni kongwe, weka historia zake na utuambie machimbuko yake.
Utofauti wa dini yako na za wenzako katika uongo ni kwamba wenzako wameanzia ndani kuongopa

Wakati uongo wa dini yako haujaanzia tu kwenye maandishi ya ndani kuhusu mambo ya Mungu bali hadi kwenye taarifa za lini dini yako imeanza, pia zimepotosha.

Na ujinga wa waumini wanakubali tu.
 
Marejeo yako ni wapi ? Mimi no mekutolea mfano wa makafiri wa Makkah na wasio kuwa wao. Wasome Mayahudi na kufuru zao.
Hao Makafiri sijui Makavel ni maneno yenu ambayo mnayatumia kuwaita wasio waislamu.

Na sometimes nayaona mkitoleana nyinyi kwa nyinyi pale ambapo mnashindwa kukubaliana kwenye mafundisho yenu.

Kwa hiyo kuniambia Makaveli sijui Makafiri wa Makka walifanya hiki na hiki haiwezi kuwa ni point inayoenda kubatilisha ulalali wa dini nyingine ambayo ni independent na ina misingi yake katika uendeshaji.
 
Haya umeyapata wapi ? Umesoma kwenye Kamusi gani ? Soma Kamusi za lugha uone zinakwambia nini kuhusu tamko Mungu. Usilete stori za vijiweni hapa. Unatakiwa ujue ya kuwa tunapo wazungumza miungu wengine since kwa maana ya halisi ya Mungu bali katika mlango wa kuwahabarisha na kuwajuza watu.
Unaulizaje kuwa hayo nimeyatoa wapi ilihali wewe mwenyewe unajua kuwa zipo dini zinazoamini Multiple Gods yani Polytheism??

Unaelewa maana ya Polytheism?
 
Kijana huwa napenda kujadili na watu wenye elimu na kuyajua mambo, leta maana ya Mungu ya Kamusi. Usilete stori za vijiweni.
Najua jinsi ambavyo unafanya jitihada za kujisahaulisha ili kukwepa swali la msingi nililokuuliza kuhusu hatua ya pili ya kuthibitisha uwepo wa Mungu.

Najua nia yako ni kuingizia mada juu ili tuondoke kwenye lengo kuu ambalo linakuwajibisha utoe uthibitisho wa uwepo wa Mungu.

Najua sababu ya kwanini unakwepa hilo swali na mara kadhaa nimeshawahi kusema kuwa huwezi kutoa majibu ya hilo swali kwasababu hauna huo uthibitisho.

Na hiyo inachagizwa na uhalisia dhana ya uwepo wa Mungu kutokuwa na uhalisia.

******************

Narudi sasa kwenye swali lako unalotaka nikupe maana ya Mungu

Maana ya Mungu nimeitoa kwenye Wikipedia najua unafahamu namna ya ku confirm taarifa zinazotoka kwenye vyanzo kama Wikipedia

Screenshot_20241219-012225.png

Sasa hapa kwenye duara lekundu ndio u focus zaidi
Screenshot_20241219-012239.png
 
Lazima nitumie dini yangu sababu ndio uhalisia wenyewe, ndio maana hata hizi Imani huwa tunazihakiki. Dini ya kweli ambayo ni marejeo ina sifa zake anuai, kwanza lazima iendane na maumbile.
Kwani ni dini gani ambayo wahusika wa hiyo dini wanakubali kuwa dini yao sio uhalisia?

Imani yako unaihakiki kupitia references zipi na zenye kufuata misingi gani?

Hizo sifa ulizozitaja ni mitizamo ya imani yenu katika kuitofautisha dini yenu na zingine.

Dini zingine tofauti na yako nazo zina kanuni zake ambazo hutumika kama utambuzi wa kupima uhalasia wa dini. Ambapo dini yao ime qualify hivyo vigezo na yako ime disqualify.
 
Ukipinga tafiti ndio umeipinga Sayansi hivyo.

Halafu kuna shida ya uelewa hapa naiona.

Hivi ukisikia kauli kuwa Bunge linajadili hoja ni ipi tafsiri unayoipata? Kwamba ni jengo linaloitwa Bunge ndio linalofanya mjadala?

Au ni wabunge ndio wanaofanya mjadala?

Mara nyingi tunatumia msemo "Sayansi imesema hivi" au "Sayansi inaonyesha kwamba" kama uwakilishi tu kumaanisha utafiti na data zilizopatikana kupitia mbinu za kisayansi zinazoonesha ushahidi au matokeo fulani.

Ingawa sayansi yenyewe sio mtu au kiumbe cha kutambua, tunatumia msemo huo tu kwa urahisi na niijua haiwezi kuleta shida ya kutoeleweka kwasababu najadiliana na mtu ambaye hivi vitu kwake ni rahisi.

Kwasababu hata makanisani ni kawaida kusikia Pastor katika mahubiri yake akiongea maneno haya "Biblia inasema" japo kuwa wote tunajua Biblia sio mtu mpaka iseme ila kwenye ishu yako maana yake hiyo ni mada nyingine ambayo utaipinga.
Msemo wa sayansi imesema..... unatumika sana na watu hufanya hivyo kupata urahisi wa kuelezea hivyo sio ajabu ila shida yako ni mtazamo wako kuhusu sayansi.

Angalia sentensi yako ya kwanza kwamba unaposema ukipinga tafiti ya sayansi ndio umeipinga sayansi, kuna tafiti ngapi za sayansi ambazo sio sahihi zinapingwa leo hii ukiniambia ukipinga tafiti ndio umepinga sayansi unanishangaza inaonyesha jinsi gani una mtazamo usio sahihi kuhusu sayansi.
 
Kuamini ni kutokuwa na uhakika, ushahidi wala uthibitisho wa jambo au kitu fulani. Ambapo jambo au kitu hicho kinaweza kiwepo ama kisiwepo.

Kujua kwa kudhani, Ni kutokuwa na taarifa sahihi zenye uhakika, ushahidi, ukweli na uthibitisho kuhusu jambo au kitu fulani ambacho tayari kipo in reality.
Sasa hapo utofauti ni upi katika hayo maneno mawili kwa kuangalia tafsiri ulizoweka?
 
Sasa hapo utofauti ni upi katika hayo maneno mawili kwa kuangalia tafsiri ulizoweka?
Imani ni kwa jambo ambalo linatarajiwa kuwepo/kutokea in future
(Yani bado halijatokea)au halipo kabisa. Au kitu ambacho kinatarajiwa kuwepo/kutokea in the future au hakipo.

Mfano mwanafunzi akifanya mtihani anakuwa na imani kwamba atafaulu, kwa sababu bado ufaulu kwake haujatokea.(Ufaulu wake upo in future). Anaweza asifaulu vilevile, Akafeli.

kwa vile alikuwa na imani tu kwa jambo la "kufaulu" ni jambo ambalo lipo in future au linaweza lisiwepo, Akafeli.

Kujua kwa kudhani, Ni kwa jambo ambalo tayari lipo, Au kitu ambacho tayari kipo kweli kwenye uhalisia. Sema wewe ndio huna taarifa sahihi za uwepo wake.

Mfano una wazazi wako. Na wewe unaweza kujua kwa kudhani kwamba kweli hao ni wazazi, Kumbe inawezekana kiuhalisia hao sio wazazi wako. Kwa vile huna uthibitisho na taarifa sahihi za kuhakikisha kweli hao ni wazazi wako.

Lakini hata kama hao wazazi kiukweli sio wazazi wako, Bado wazazi wako wa asili waliokuzaa lazima wapo au walikuwepo ndio maana ulizaliwa. Sema huna taarifa sahihi za kuhakikisha uwepo wao.

Unabaki kujua kwa kudhani tu hao wasio wazazi, Ni wazazi wako. Kumbe sio.

Kiuhalisia una wazazi wako wa asili ambao bado huna taarifa sahihi, bado huja hakikisha na kuthibitisha uwepo wao.
 
Mashambulizi ni makali sana, haya mambo ya kiimani yana mkanganyiko sana.
 
Kuna mambo mengi huyajui kwasababu ya kutofuatilia.

Umetaja Mungu Ng'ombe ambaye kimsingi ni Mungu wa imani ya Kihindu.

Lakini kitu ambacho umeshindwa kukielewa ni kutonielewa kwenye maelezo yangu niliyoandika hususan pale nilipopinga kauli yako kuwa Mungu mkuu pekee ndio anayepaswa kuabudiwa.

Wahindu wanaamini kwenye Miungu yani Mungu zaidi ya mmoja kama ilivyo tu kwa Sumerian.

Kwenye hiyo Miungu kila Mungu ana department yake ambayo amehusishwa nayo.

Na mmoja wa hiyo Miungu ni pamoja na huyu Mungu Ng'ombe ambaye wewe umemuwekea kama mfano na jina lake anaitwa Kamadhenu au surabhi.
View attachment 3179940

Wahindu huamini kuwa Miungu yao au viumbe wa Mungu kwa imani yao huchukua maumbo ya ng'ombe.

Hivyo wao wanawapa heshima hao wanyama kwasababu wanawaona kama ni sehemu ya baraka.

Huyu ni Mungu ambaye department yake inahusika na ishu ya uponyaji na maswala mengine ya kilimo.

Kwenye hiyo hiyo dini ya Kihindu ambayo kuna Mungu Ng'ombe pia wanaye Mungu Brahma ambaye huyu department yake ni maswala ya uumbaji.

View attachment 3179941

Kwa hiyo ukisikia kuwa kuna jamii zinaabudu Mungu paka au fisi haina maana hawana backup ya Mungu muumba.

Wala haina maana kama wanaamini Mungu wa dini yako ndio muumba.

Wao wana multiple Gods, na hao wanayama ni wawakilishi tu yani ni kama nyie mnavyosema mitume au manabii.
Nakuuliza kwanini huigusi hoja yangu ?
 
Kwani ni dini gani ambayo wahusika wa hiyo dini wanakubali kuwa dini yao sio uhalisia?

Imani yako unaihakiki kupitia references zipi na zenye kufuata misingi gani?

Hizo sifa ulizozitaja ni mitizamo ya imani yenu katika kuitofautisha dini yenu na zingine.

Dini zingine tofauti na yako nazo zina kanuni zake ambazo hutumika kama utambuzi wa kupima uhalasia wa dini. Ambapo dini yao ime qualify hivyo vigezo na yako ime disqualify.

Sababu kila mtu anaona dini yake ni sahihi, ndio maana tunakuja au kinakuwa na hatua ya kuzihakiki dini husika.

Msingi wa kwanza lazima dini ya kweli iendane na maumbile, hili nimelitaja huko awali.

Pili, lazima tuangalie historia na na chimbuko la dini husika.

Tatu, lazima tuangalie ilikuwaje ikawepo na ilianzishwaje na marejeo ya maandiko yake ni wapi.

Labda nikuulize swali rahisi maana naona unakimbia hoja. Wewe unatumia njia gani kuhakiki habari au unaokoteza okoteza ?
 
Najua jinsi ambavyo unafanya jitihada za kujisahaulisha ili kukwepa swali la msingi nililokuuliza kuhusu hatua ya pili ya kuthibitisha uwepo wa Mungu.

Najua nia yako ni kuingizia mada juu ili tuondoke kwenye lengo kuu ambalo linakuwajibisha utoe uthibitisho wa uwepo wa Mungu.

Najua sababu ya kwanini unakwepa hilo swali na mara kadhaa nimeshawahi kusema kuwa huwezi kutoa majibu ya hilo swali kwasababu hauna huo uthibitisho.

Na hiyo inachagizwa na uhalisia dhana ya uwepo wa Mungu kutokuwa na uhalisia.

******************

Narudi sasa kwenye swali lako unalotaka nikupe maana ya Mungu

Maana ya Mungu nimeitoa kwenye Wikipedia najua unafahamu namna ya ku confirm taarifa zinazotoka kwenye vyanzo kama Wikipedia

View attachment 3179944

Sasa hapa kwenye duara lekundu ndio u focus zaidiView attachment 3179945
Hili tatizo lingine, ulichokiweka bado kinahitaji marejeo, inabidi usome pia namna ya kurejea na kunukuu jambo.

Hapa nakuuliza tena, huyu aliweka haya huku Wikipedia marejeo yake ni wapi ?

Kingine hoja ya dini nyingine kukubali kuwepo kwa miungu msingi, nimeielezea huko juu kwa kuashiria mfano wa makafiri wa Makkah, Hawa walikuwa Wana miungu 360 na kila Mungu alikuwa na jukumu lake, lakini walikuwa wanajua na kuamini ya kuwa Mungu Mkuu ni yule ambaye ameumbwa mbingu na ardhi na ndio muendesha mambo na ndio anayepaswa kuabudiwa, lakini katika ibada zao walikuwa Wana waabudu hao miungu wao.
 
Najua jinsi ambavyo unafanya jitihada za kujisahaulisha ili kukwepa swali la msingi nililokuuliza kuhusu hatua ya pili ya kuthibitisha uwepo wa Mungu.

Najua nia yako ni kuingizia mada juu ili tuondoke kwenye lengo kuu ambalo linakuwajibisha utoe uthibitisho wa uwepo wa Mungu.

Najua sababu ya kwanini unakwepa hilo swali na mara kadhaa nimeshawahi kusema kuwa huwezi kutoa majibu ya hilo swali kwasababu hauna huo uthibitisho.

Na hiyo inachagizwa na uhalisia dhana ya uwepo wa Mungu kutokuwa na uhalisia.

Mpaka tunafikia hapa ni wewe kutokujibu hoja zangu. Hii inaondoa maana ya mjadala.

Msingi wangu Mimi ni lazima tujue ukweli wa kila tubalo lijadili ili isiwe tunapoteza muda. Huwezi kujengea hoja mambo ambayo huyajui na huna elimu nayo.

Suala la uthibitisho juu ya uwepo wa Mungu, tumeshathibitisha sana na hili ni rahisi sana kwetu. Shida inakuja kwenu ambao hamna na hamtoweza kuja kuthibitisha ya kuwa hakuna Mungu. Sababu akili iliyo salimika haikatai hilo. Kwahiyo hili ni jambo dogo sana kwetu.
 
Unaulizaje kuwa hayo nimeyatoa wapi ilihali wewe mwenyewe unajua kuwa zipo dini zinazoamini Multiple Gods yani Polytheism??

Unaelewa maana ya Polytheism?

Huu ni utoto mwingine, maana kitu kinachojulikana ni rahisi kukiletea marejeo, au wewe umeyaota haya ? Inakuwaje tunapoteza muda kwenye hakuna ?

Wewe weka umeyaota wapi ? Tatizo la kujibu maswali mnayo ulizwa kunawafanya mzidi kuonekana ni madhaifu sana.
 
Scars
Kiranga
min -me
Infropreneur
Nyani Ngabu

Mmekua mnapinga uwepo wa Mungu kila siku kwa kuuliza maswali yale yale bila kuja na kitu kipya
Sasa naomba niwaulize kama mmeweza kujua kuwa hakuna Mungu, pia kuna uwezekano mmeshajua Chanzo cha huu uliwengu na viumbe vyake
Naomba mje kutueleza chanzo cha huu ulimwengu na viumbe vyake ni nini?

Nafkiri sisi wenye imani ya uwepo wa Mungu tuanze kuwa challenge hawa Atheist kwa kuwahoji maswali fikirishi sio kila siku kubishana Mungu yupo au hayupo
Kwa hiyo wewe ni nyani/sokwe au uliumbwa binadamu!??
 
Back
Top Bottom