Mungu mkuu ni utambulisho wa kila dini katika kuelezea sifa za Mungu wanaye muabudu.
Kwahiyo wanao abudu Ng'ombe husema Ng'ombe ndio Mungu Mkuu ? Au wanao abudu sana husema hilo ? Inaonekana hujui maana ya Mungu Mkuu.
Hata zile dini za kale ambazo ni kongwe kuliko yako kama Sumerian zilikuwa zina amini Mungu zaidi ya mmoja, kwenye hiyo miungu zilikuwa na Mungu mkuu aliyekuwa anaitwa Enki ambaye ni mhusika na maswala hayo ya uumbaji.
Kijana usipate tabu, ndio maana nakwama huna misingi ya kielimu. Hakuna dini kongwe kuzidi Uislamu.
Hizo unazo dai kuwa ni kongwe, weka historia zake na utuambie machimbuko yake.
Kwa hiyo sio kweli kuwa dini zenye kuabudu Mungu zaidi ya mmoja zinaamini nje ya imani yao kuna Mungu muumba wa ulimwengu kwasababu tumeona hata wao pia katika orodha ya Miungu wao wanaye huyo Mungu ambaye ni muumba.
Marejeo yako ni wapi ? Mimi no mekutolea mfano wa makafiri wa Makkah na wasio kuwa wao. Wasome Mayahudi na kufuru zao.
Sio kweli kuwa tamko Mungu ni tamko linalomaanisha ni Mungu pekee anayepaswa kuabudiwa.
Haya umeyapata wapi ? Umesoma kwenye Kamusi gani ? Soma Kamusi za lugha uone zinakwambia nini kuhusu tamko Mungu. Usilete stori za vijiweni hapa. Unatakiwa ujue ya kuwa tunapo wazungumza miungu wengine since kwa maana ya halisi ya Mungu bali katika mlango wa kuwahabarisha na kuwajuza watu.
Hii itabaki kuwa ni maoni yenu binafsi kulingana na lenye mipaka isiyovuka imani yenu hivyo haiwezi kuwa ni tamko lenye kujumuisha imani zingine na ndio maana tumeweza kuona imani zingine zikiwa na Mungu zaidi ya mmoja na wote wakiabudiwa.
Kijana huwa napenda kujadili na watu wenye elimu na kuyajua mambo, leta maana ya Mungu ya Kamusi. Usilete stori za vijiweni.
Kusema imani ya wengine sio sahihi, hauwezi kuwa sahihi. Kwasababu hauwezi kutumia sheria za dini yako kukosoa dini za wengine.
Lazima nitumie dini yangu sababu ndio uhalisia wenyewe, ndio maana hata hizi Imani huwa tunazihakiki. Dini ya kweli ambayo ni marejeo ina sifa zake anuai, kwanza lazima iendane na maumbile.
Hata hizo dini zinaweza kukuambia kuwa dini yako ni ya uongo kwasababu wanazoziona zinahitilafiana na kanuni za dini yao.
Kusema sio hoja, Cha msingi ni kuthibitisha ukweli wa dini yao, sababu haya mambo yanajadilika na vitabu vipo na historia zimedhibitiwa.