Je, LBL sio Matapeli kama Matapeli wengine?
Status
Not open for further replies.
Sasa kuna nyingine hiyo ina faida kinoma kama kawaida wa kwanza kula wa mwisho kuliwa nisharuka nayo. hiyo 200k inakupa 28500 kila siku na hufanyi chochote. imeanza tarehe nne nimeiwahi mapema msemo ni ule ule wa kwanza kula wa mwisho kuliwa.
Hii nishirikishe , miezi sita haijafika bado hapa Kati Kati lazima tumake pesa
 
Narudia tena, mtu aingie akijua kuwa huu ni utapeli muda wowote utaisha. Mimi nimeingia nikijua kuwa ni utapeli muda wowote unaweza kupoteza ela yote na hiyo ni lazima. Ipo siku tutarudi kwenye thread hii wakishasepa na kijiji.
So, mimi sialiki watu kwa sababu najua muda wowote inaweza kuisha na mtu akanilaumu. mtu kama anaingia aingie mwenyewe kwa mapenzi yake.
Niliona kipindi cha kalynda watu hadi wakakimbia jiji kwa kudaiwa na waliowaingiza.
Jamaa hawana website yyte ila Wana blog moja ya kihuni kinyama, imejaa virus wameandika imeanza mwez wa 7 -2024 to April 2025
 
Kumeibuka utapeli mwingine hivi karibu wa upatu (ponzi scheme) ijulikanayo kama LBL ambako wananchi wengi wanaweka fedha zao ili kuvuna. Huu ni mwendelezo wa yale yaliyotokea awali kama Deci, QNet, ClubD9, Kalinda na Kuku.

Kabla wananchi wengi hawajawa wahanga wa uhalifu,tunaviomba vyombo vya usalama viwachukulie hatua za kisheria wahusika wote wa uhalifu huu.
 
Kumeibuka utapeli mwingine hivi karibu wa upatu (ponzi scheme) ijulikanayo kama LBL ambako wananchi wengi wanaweka fedha zao ili kuvuna. Huu ni mwendelezo wa yale yaliyotokea awali kama Deci,QNet,ClubD9,Kalinda na Kuku. Kabla wananchi wengi hawajawa wahanga wa uhalifu,tunaviomba vyombo vya usalama viwachukulie hatua za kisheria wahusika wote wa uhalifu huu.

Serikali itawaelimisha wananchi mara ngapi?. Waache wapigwe wajifunze in a hard way.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom