Je, LBL sio Matapeli kama Matapeli wengine?
Status
Not open for further replies.
Kuna mtu kanirushia link yao ananiambia unajiunga kwa Kiasi fulani cha pesa, mfano 540K halafu wao watakuwa wanakutumia video za matangazo ya biashara Kila siku video tano, unaview sekunde 5 Kila tangazo, halafu wao wanakulipa 18,000 Kila siku, nimekuja kwenu mnisaidie tafadhali kabla sijapigwa.

Utapigwa kitu kinaitwa " cut out"
 
Kuna mtu kanirushia link yao ananiambia unajiunga kwa Kiasi fulani cha pesa, mfano 540K halafu wao watakuwa wanakutumia video za matangazo ya biashara Kila siku video tano, unaview sekunde 5 Kila tangazo, halafu wao wanakulipa 18,000 Kila siku, nimekuja kwenu mnisaidie tafadhali kabla sijapigwa.

Yaani kuangalia tangazo ndio ulipwe?matapeli ,utalipwa siku moja au mbili ili ulete wengine baada ya hpo umepigwa .watakunga telegram
 
Kuna mtu kanirushia link yao ananiambia unajiunga kwa Kiasi fulani cha pesa, mfano 540K halafu wao watakuwa wanakutumia video za matangazo ya biashara Kila siku video tano, unaview sekunde 5 Kila tangazo, halafu wao wanakulipa 18,000 Kila siku, nimekuja kwenu mnisaidie tafadhali kabla sijapigwa.

Wa kwanza kula wa mwisho kuliwa. waliotangulia wamekula na kula na kula tena. sasa hivi lbl ina miezi kama nane, so haijulikani kama itaendelea au lini itakufa. Ni kweli hata mimi nipo nishakula na kula na kula sana. Yani ela niliyoweka ishatoka zaidi ya mara sijui 10. Stake what you are ready to lose. Ni kama kubet
 
Mizengo pinda akiipenda sawa akikunja ule uso ulo kunjika tayari ujue watu wanalizwa,lile jasusi limeua JATU, DECI na ,BBT na nyingine nyingi,lakini maisha yanapita hata mazao yanaanza vizuri mwisho bei inaporomoka,na watanzania pia tukome kila kitu lazima mlete huku Jamii forum,hivi wajua hata DECI ni midomo iliponza kichaa sasa hata blt italima watu sababu ya vibwengo kama nyie,hata bajaji zimepanda bei sababu ya wapenda sifa kama.wewe Tena mnaongelea bar,serikali yenyewe ni ya njaa njaa tuu wakiskia hapa tuu watu wanalizwa,imagine that.
 
kinachoenda kukukuta ni kama ile hadithi ya kale ya mzee Bushele alipiga msele na baiskeli kuleta manjonjo kwa mkewe akamwaga ubwabwa wa kula jioni.

Alikimbizwa na mke wake akarushiwa mwiko wa kisogo 😆😆
Bila shaka familia ililala njaa.. sifa za kijinga😀
 
Asilimia kubwa ya Mitanzania ni kama minyumbu vile mijingamijinga aise .

Wapelekee wakupige ulete mrejesho .Nirudie kusema hakuna hela ya bure jamani fanyeni kazi aise.

Mwandishi mathiasi mnyampala katika kitabu chake cha diwani ya mnyampala aliandika shairi akisema "bure ina sumu kali yafaa kuiepuka."

Sasa kwakuwa wengi wanapenda kitonga acha wapigwe.

Juzi mwamposa amepiga hela za manyumbu watu laki nne wamehudhuria mkesha mfano kila mtu alitoa sadaka ya bukubuku au buku mbili piga hesabu ni shingapi kaingiza.
Hata haomanabii yameshajua mitanzania inataka hela za miujiza sasa wanajipigia hela balla

Mwanza napo nasikia mchungaji mmoja nimemsahau jina nae anamkesha wa wiki nzima watu kamq laki wehudhuria sasa piga hesabu nishingapi kakusanya za sadaka.
Acha Yesu aabudiwe wewee
 
Kuna mtu kanirushia link yao ananiambia unajiunga kwa Kiasi fulani cha pesa, mfano 540K halafu wao watakuwa wanakutumia video za matangazo ya biashara Kila siku video tano, unaview sekunde 5 Kila tangazo, halafu wao wanakulipa 18,000 Kila siku, nimekuja kwenu mnisaidie tafadhali kabla sijapigwa.

Watumie haraka sana izo hela, bila shaka unazo nyingi
 
Wa kwanza kula wa mwisho kuliwa. waliotangulia wamekula na kula na kula tena. sasa hivi lbl ina miezi kama nane, so haijulikani kama itaendelea au lini itakufa. Ni kweli hata mimi nipo nishakula na kula na kula sana. Yani ela niliyoweka ishatoka zaidi ya mara sijui 10. Stake what you are ready to lose. Ni kama kubet
Upo sahihi mkuu Kuna raia wamepiga Sana pesa hizi ishu za pyramid scheme ukiwahi unapiga pesa,wajinga ndio waliwao
 
Najua itakavyoisha kwa sababu mimi nimeingia vikampuni uchwara vingi vya hivi na mwisho wake naujua. Sasa hivi kwanza siwezi mwalika mtu ajiunge kwasababu ishatimiza miezi kadhaa na muda wowote inaweza kubuma ikasepa na ela ya mtu akakulaumu. ndo maana sialiki mtu. hizo akaunti zangu nimejialika mwenyewe kutokea kwenye akaunti moja.
Yani unajikiona lbl ni kile kile cha kalynda tofauti huko ulikuwa unaambiwa na process orders, lbl unatazama video ambazo unakuta ni zile zile week nzima.
LBL unaambiwa kampuni imesajiliwa sijui london. Hivi kama uwekezaji ungekuwa rahisi hivi, unadhani balkshire wangeenda kuwekaza dollar milioni 260 kwenye kampuni ambayo faida yake itaanza kutengenezwa baada ya miaka 10 na huenda ikafa kwa sababu ni startup?
Nachosema, kama umewekeza huko kula ila kwa kuita watu wakaweka pesa kuna ambao wataweka na itabuma kabla ya hata kurudisha fedha yao na watakulaumu. Mimi ni mtu ambaye sipendi lawama. Na nimeweka fedha nikijua risk zake.
Pia ingelikuwa ni kampuni genuine ela ingekwua inawekwa kwa lipa namba, sio kuituma kama unamtumia mtu na kila wakati jina tofauti ili sever isome msg zilizopokelewa ilinganishe na namba iliyotuma hiyo fedha ndo iupdate.
Umeongea maneno ya uchungu me nimekopa pesa nimejiunga level 3 nataka pesa irudi chap Ila nipo tayari kuipoteza hiyo pesa naombea Hawa jamaa wadumu hata miezi sita ijayo,Ila Kuna harufu ya kupigwa hasa kwenye uwekezaji wa muda mrefu

Ishu ya malipo kutoka namba binafsi ni Jambo lakufikirisha Sana na video kujirudia ni Jambo lingine la kufikirisha

All in all waliowahi wanapiga pesa sana
 
Kuna jamaa yangu anapata pesa ila mimi siingii kamwe.. niaaacheee kuna mahalii watu wata jamaaa .. hakuna marefu yasikuwa na nchaa
 
Nikampuni ambayo ukiweka pesa kidogo kuna pesa unalipwa mwaka mzima kilasiku. Kuna video ukazaa unatakiwa uzi view. Ila sijaielewa vizuri. Naomba maelezo kwa mwenye kuijua
Wewe.niambie biashara ngapi zinafunguliwa na kufa,jaribu kinachowezekana,ikibuma poa tuu,infact hata maisha ya binadamu yana mwisho.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom