Najua itakavyoisha kwa sababu mimi nimeingia vikampuni uchwara vingi vya hivi na mwisho wake naujua. Sasa hivi kwanza siwezi mwalika mtu ajiunge kwasababu ishatimiza miezi kadhaa na muda wowote inaweza kubuma ikasepa na ela ya mtu akakulaumu. ndo maana sialiki mtu. hizo akaunti zangu nimejialika mwenyewe kutokea kwenye akaunti moja.
Yani unajikiona lbl ni kile kile cha kalynda tofauti huko ulikuwa unaambiwa na process orders, lbl unatazama video ambazo unakuta ni zile zile week nzima.
LBL unaambiwa kampuni imesajiliwa sijui london. Hivi kama uwekezaji ungekuwa rahisi hivi, unadhani balkshire wangeenda kuwekaza dollar milioni 260 kwenye kampuni ambayo faida yake itaanza kutengenezwa baada ya miaka 10 na huenda ikafa kwa sababu ni startup?
Nachosema, kama umewekeza huko kula ila kwa kuita watu wakaweka pesa kuna ambao wataweka na itabuma kabla ya hata kurudisha fedha yao na watakulaumu. Mimi ni mtu ambaye sipendi lawama. Na nimeweka fedha nikijua risk zake.
Pia ingelikuwa ni kampuni genuine ela ingekwua inawekwa kwa lipa namba, sio kuituma kama unamtumia mtu na kila wakati jina tofauti ili sever isome msg zilizopokelewa ilinganishe na namba iliyotuma hiyo fedha ndo iupdate.