Status
Not open for further replies.
Na
Ifike wakati mtu akitapeliwa kama mtumishi wa umma afukuzwe kazi, kama kijana tu anyang'anywe vyeti vyote isipokuwa cha drs la 7 na kuzaliwa.
Haiingii akilini mtu mwenye elimu ya kuanzia kidato cha 4 atapeliwe kijinga
Naomba, koment yako iprintiwe na copies zake zibandikwe makao makuu ya nchi dodoma, bungeni pale, dar iwekwe posta na kariakoo. Mikoani iwekwe kwenye kila roundabout ya mjini.

Na kwenye kila bango laMAMA ANATOSHA litolewe, iwekwe koment yako.
 
IELEWE LBL

πŸ’ πŸ’ TANZANIA ADVERTISING MEDIA LIMITED πŸ’ πŸ’ 

βœ…LBL Imeanza tangu mwaka 1967

βœ…LBL kirefu chake ni Leo burnett London

♻️Hapa Tanzania imeingia mwaka huu mwezi wa pili baada ya kualikwa na serikali yetu ya jamuhuri ya Muunguano wa Tanzania. Baada ya usajili na kukamilisha taratibu zote ikaanza kufanya kazi rasmi mwezi wa saba mwaka huu.

♻️Hapa manispaa ya Morogoro mtu wa kwanza/muasisi wetu ni Dr David Lugomela ambaye ndiye kiongozi wetu mkuu na kutushirikisha fursa hii.

♻️ LBL inafanyaje kazi.
Kumbuka ni kampuni inayohusiana na utangazaji. Ni kampuni iliyobobevu duniani.
1. Makampuni mengi makubwa ya filamu dunia. Wale wapenzi wa movie mtaelewa hili. Mfano.
πŸŒ€ *Paramount,
πŸŒ€20th century Fox,
πŸŒ€ destiny* ,
πŸŒ€Warner Brothers,
πŸŒ€DreamWorks picture,
πŸŒ€Universal Picture
πŸŒ€MGM Picture na mengine mengi
Yameweka ubia na kampuni ya LBL isaidie kutangaza matangazo yao ya movie na filamu ili yawafikie watu wengi duniani.
Hivyo basi ili kampuni ya LBL ifanye jukumu hilo vyema wakaona iajiri watu wengi ambao watatazama matangazo ya movie na hapo idadi ya watu wengi itafikiwa. Ndo mana inasisitiza kualika watu zaidi

πŸ”° _Baada ya muda wanapeleka kwa makampuni na kuwaonesha mfano:...........
_
πŸŒ€*PARAMOUNT * movie yako hii imetazamwa na watu milioni 10.5 mwezi huu.( Utakuta walikubaliana hivi kwamba Kila viewers mmoja( mtu mmoja aliyetazama) Lbl watalipwa Dola 1. Hebu jaribu kuchukua Dola 1 Γ— mil 10.5 LBL wanaingiza. Kwanini wasirudishe fadhira. Hivyo ndivy LBL Inavyofanya kazi.

βœ…UZOEFU
_Wengi wetu twajua nyakati hizi wengi hupata pesa Kwa mitandao.

_Diamond huingiza fedha YouTube kwa kuwa tu na viewers wengi.

_MiladAyo anaingiza fedha Kwa kuwa tu na viewers wengi

πŸ–ŠοΈNote vipi wewe unayetazama kazi zao unalipwa ? Au unagharamika bando lako?

♻️LBL UNAPOVIEW video hawakuachi hivihivi. Kwasababu wanajali ikiwa tunawaingizia fedha nyingi sana basi wakaona nasi tupate kifuta jasho. Ambacho kwetu kinathamani Kubwa, kwa level tofauti kama ifuatavyo........... πŸ‘‡

1️⃣ P1 LEVEL

_πŸ’ Ukiweka 50,000
πŸ’ Unapewa picha 5 za kuangalia
πŸ’ Kila picha unalipwa 335
πŸ’ Kwa siku unalipwa 1675
πŸ’ Kwa mwezi unalipwa 50250
πŸ’ Kwa mwaka 611,375 /=_

2️⃣ P2 LEVEL

πŸ’ Ukiweka 150,000
πŸ’ Unapewa Picha 10 za kuangalia
πŸ’ Kila picha unalipwa 500
πŸ’ Kwa siku unalipwa 5000
πŸ’ Kwa mwezi 150,000
πŸ’ Kwa mwaka 1,825,000
πŸ’ Hivyo 150,000 itakuwa imezaa sh 1,675,000

πŸ’ Ukiweka 540,000
πŸ’ Unapewa picha 15 za kuangalia
πŸ’ Kila picha unalipwa 1200
πŸ’ Kwa siku unalipwa 18000
πŸ’ Kwa mwezi 540,000
πŸ’ Kwa mwaka 6,570,000
πŸ’ Hivyo 540,000 itakuwa imezaa 6,030,000 /

✳️ILI kujiunga nijulishe nikutumie Link.

✳️Kujiunga na LBL * ni bure kabisaa ila ili uwe mwajiriwa au mfanyakazi rasmi wa LBL unatakiwa kuwa na mtaji wa *50000/= kwa ngazi ya P1 , 150000/= kwa ngazi ya P2, na 540000/= kwa ngazi ya P3 Kumbuka hakuna biashara unayoweza ifanya kama hauna mtaji ni lazima uwe na mtaji. ukikamilisha account yako nitakuadd kwa group la WhatsApp
UTAKUWA TAYARI UANZE KAZIπŸ’ πŸ’ 

πŸ”°MWISHO .
✳️ LBL MAFANIKIO ni hakika
✳️LBL sio matapeli. Tuwe makini na matapeli watakao jitokeza na kuharibu sifa ya kampuni.

✳️Hii ni kazi sio kamali au bahati nasibu .
✳️Usipoview huwezi pata pesa Kwa sababu nao hawajapata pesa kupitia wewe.



Matangazo yao sasa yalivyokaa kitapeli , kuna dogo hapa namwambia ni utapeli lakini anabisha kinoma yani , sijui huwa wanawapa roho gani ya kuwa wabishi
 
Mijini wajinga hawaishi
Halafu wanajifanyaga wajanja
 
Dogo baada ya kunifowadia hayo ikabidi nimuulize maswali haya

Ntaomba vithibitisho vifuatavyo ukinipa soon na mimi ntajiunga na wewe
  • HQ za hio kampuni zipo wapi?
  • Leseni za uthibitsho wa kuthibitisha kuwa ni kampuni halali ya kurun bussiness Tanzania kutoka BRELA na mamlaka mengine husika
  • Mawasiliano yao endapo utapata changamoto yoyote
Yangu ni hayo tu
 
hiyo mbona kawaida, hata wakulima kuna wanaopata na wanaokosa, wafanyabiashara kuna wanaofaidika na wanaofilisika, wasafiri kuna wanaofika na ambao hawafiki. Kila kitu ni betting ukijua hilo huumizi kichwa.
Maneno ya kujifariji. Utapeli tu
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…