Je, LBL sio Matapeli kama Matapeli wengine?
Status
Not open for further replies.
Dogo baada ya kunifowadia hayo ikabidi nimuulize maswali haya

Ntaomba vithibitisho vifuatavyo ukinipa soon na mimi ntajiunga na wewe
  • HQ za hio kampuni zipo wapi?
  • Leseni za uthibitsho wa kuthibitisha kuwa ni kampuni halali ya kurun bussiness Tanzania kutoka BRELA na mamlaka mengine husika
  • Mawasiliano yao endapo utapata changamoto yoyote
Yangu ni hayo tu
Utakuwa huna ujanja wowote ukijiunga kwa kuona eti imesajiliwa na BRELLA.

Hawa wanaotapeli watu wanakuwa na usajili na vibali vyote.Wanaweza kwenda vyombo vya habari na kupewa muda wa kutosha kutangaza biashara zao mfano Rifaro Africa walipata airtime ya kutosha chanell 10.

Kifupi ni miradi ya baadhi ya wenye mamlaka,kujipatia pesa ya kampeni mwakani.Wakishapata pesa hizo wanajifanya kuzipiga marufuku kampuni hizi

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Ebhana ehe mi niliomba hivi vitu nikapewa Hila naisi ni vya adobe mana sikujishughulisha navyo Toka siku hiyo mana Nina mambo mengi yananiendesha ngoja niweke hapa tushare na wadau kwa faida ya wengine wasitapeliwe
 
Kuna ule wa 'sungura project' mradi huu upo same,watu wameweka pesa zao,Kuna jamaa alinifuata na kunishawishi nijiunge,nikamwambia DECI ilinipa fundisho zuri sana!
Mkuu, Mimi deci hadi inasepa nilikuwa nimepanda 6M zikafiamo, lakini sasa 😃😃 nilikuwa nimevuna 13M. Nami pia ilinipa fundisho, kwa hiyo ikitokea fursa kama hizo huwa nawahi mapemaaa, yaani sie ndo huwa wa kwanza kwanza kabisa 😃😃😃, mchezo unaitwa wa kwanza ndiyo mshindi 😂😂😂😂, deci ikirudi hata leo naingia, kwa hiyo kila mtu anafundisho lake alilopata.
 
Zimekuja kwa wingi ipo nyingine kwenye soka -FIC inalipa vibaya mno! Wemefungua ofisi DSM, Mbeya na Mwz, ni obvious wana leseni na wanatoa misaada sana kwa wasio jiweza ! Huenda ndio CSR/ corporate social responsibility yao! Sio mhsukia wafuatilie kwenye mtandao utawasoma!
 
Ithibati yao niliyotumiwagwa hii sasa kampuni hipo Tanzania nzima hila ithibati ni ya moro TU sikutaka kuumiza ndonga sana mana sikuwa na mpango wa kutapeliwa pesa ngumu aisee
 

Attachments

  • Screenshot_20241222-100409_1.jpg
    Screenshot_20241222-100409_1.jpg
    236.7 KB · Views: 10
IELEWE LBL

💠💠TANZANIA ADVERTISING MEDIA LIMITED
💠💠

✅LBL Imeanza tangu mwaka 1967

✅LBL kirefu chake ni Leo burnett London

♻️Hapa Tanzania imeingia mwaka huu mwezi wa pili baada ya kualikwa na serikali yetu ya jamuhuri ya Muunguano wa Tanzania. Baada ya usajili na kukamilisha taratibu zote ikaanza kufanya kazi rasmi mwezi wa saba mwaka huu.

♻️Hapa manispaa ya Morogoro mtu wa kwanza/muasisi wetu ni Dr David Lugomela ambaye ndiye kiongozi wetu mkuu na kutushirikisha fursa hii.

♻️ LBL inafanyaje kazi.
Kumbuka ni kampuni inayohusiana na utangazaji. Ni kampuni iliyobobevu duniani.
1. Makampuni mengi makubwa ya filamu dunia. Wale wapenzi wa movie mtaelewa hili. Mfano.
🌀 *Paramount,
🌀20th century Fox,
🌀 destiny* ,
🌀Warner Brothers,
🌀DreamWorks picture,
🌀Universal Picture
🌀MGM Picture na mengine mengi
Yameweka ubia na kampuni ya LBL isaidie kutangaza matangazo yao ya movie na filamu ili yawafikie watu wengi duniani.
Hivyo basi ili kampuni ya LBL ifanye jukumu hilo vyema wakaona iajiri watu wengi ambao watatazama matangazo ya movie na hapo idadi ya watu wengi itafikiwa. Ndo mana inasisitiza kualika watu zaidi

🔰 _Baada ya muda wanapeleka kwa makampuni na kuwaonesha mfano:...........
_
🌀*PARAMOUNT * movie yako hii imetazamwa na watu milioni 10.5 mwezi huu.( Utakuta walikubaliana hivi kwamba Kila viewers mmoja( mtu mmoja aliyetazama) Lbl watalipwa Dola 1. Hebu jaribu kuchukua Dola 1 × mil 10.5 LBL wanaingiza. Kwanini wasirudishe fadhira. Hivyo ndivy LBL Inavyofanya kazi.

✅UZOEFU
_Wengi wetu twajua nyakati hizi wengi hupata pesa Kwa mitandao.

_Diamond huingiza fedha YouTube kwa kuwa tu na viewers wengi.

_MiladAyo anaingiza fedha Kwa kuwa tu na viewers wengi

🖊️Note vipi wewe unayetazama kazi zao unalipwa ? Au unagharamika bando lako?

♻️LBL UNAPOVIEW video hawakuachi hivihivi. Kwasababu wanajali ikiwa tunawaingizia fedha nyingi sana basi wakaona nasi tupate kifuta jasho. Ambacho kwetu kinathamani Kubwa, kwa level tofauti kama ifuatavyo........... 👇

1️⃣ P1 LEVEL

_💠Ukiweka 50,000
💠Unapewa picha 5 za kuangalia
💠Kila picha unalipwa 335
💠Kwa siku unalipwa 1675
💠Kwa mwezi unalipwa 50250
💠Kwa mwaka 611,375 /=_

2️⃣ P2 LEVEL

💠Ukiweka 150,000
💠Unapewa Picha 10 za kuangalia
💠Kila picha unalipwa 500
💠Kwa siku unalipwa 5000
💠Kwa mwezi 150,000
💠Kwa mwaka 1,825,000
💠Hivyo 150,000 itakuwa imezaa sh 1,675,000

💠Ukiweka 540,000
💠Unapewa picha 15 za kuangalia
💠Kila picha unalipwa 1200
💠Kwa siku unalipwa 18000
💠Kwa mwezi 540,000
💠Kwa mwaka 6,570,000
💠Hivyo 540,000 itakuwa imezaa 6,030,000 /

✳️ILI kujiunga nijulishe nikutumie Link.

✳️Kujiunga na LBL * ni bure kabisaa ila ili uwe mwajiriwa au mfanyakazi rasmi wa LBL unatakiwa kuwa na mtaji wa *50000/= kwa ngazi ya P1 , 150000/= kwa ngazi ya P2, na 540000/= kwa ngazi ya P3 Kumbuka hakuna biashara unayoweza ifanya kama hauna mtaji ni lazima uwe na mtaji. ukikamilisha account yako nitakuadd kwa group la WhatsApp
UTAKUWA TAYARI UANZE KAZI💠💠

🔰MWISHO .
✳️ LBL MAFANIKIO ni hakika
✳️LBL sio matapeli. Tuwe makini na matapeli watakao jitokeza na kuharibu sifa ya kampuni.

✳️Hii ni kazi sio kamali au bahati nasibu .
✳️Usipoview huwezi pata pesa Kwa sababu nao hawajapata pesa kupitia wewe.



Matangazo yao sasa yalivyokaa kitapeli , kuna dogo hapa namwambia ni utapeli lakini anabisha kinoma yani , sijui huwa wanawapa roho gani ya kuwa wabishi
Duh, na watu wanajiunga kabisa kwenye huu uharo? Watanzania acha tu wapigwe.
 
Ifike wakati mtu akitapeliwa kama mtumishi wa umma afukuzwe kazi, kama kijana tu anyang'anywe vyeti vyote isipokuwa cha drs la 7 na kuzaliwa.
Haiingii akilini mtu mwenye elimu ya kuanzia kidato cha 4 atapeliwe kijinga
Mi naongezea hao wananchi wanaocheza sijui LBL na nyinginezo wakienda kulalamikia wameliwa, wakamatwe na washtakiwe kwa uhujumu uchumi na kesi zao zisiwe na dhamana.
 
Mimi huwa sioni tofauti ya hayo yanayofanyika na kamari (betting),kwenda kwa kina Mwamposa au Waganga wa Kienyeji n.k.Watu wetu ni kama wale Nyumbu wa Serengeti wakishaamini kule wanakoenda ndio sahihi ukijaribu kuwazuia watakuua wewe. Serikali iendeleze tu ule utaratibu wake wa kukaa pembeni zikijaa au malengo yakifikiwa wanafunga dirisha lao wanasepa,tunasubiri "desi"nyingine maisha yasonge.Kama hatuwabugudhi kina Mwamposa kwa kuuzia Watu maji na mafuta au hao kamari za mchongo pesa n.k basi tuache double standard.
 
Zimekuja kwa wingi ipo nyingine kwenye soka -FIC inalipa vibaya mno! Wemefungua ofisi DSM, Mbeya na Mwz, ni obvious wana leseni na wanatoa misaada sana kwa wasio jiweza ! Huenda ndio CSR/ corporate social responsibility yao! Sio mhsukia wafuatilie kwenye mtandao utawasoma!
Hii nimo ni nzuri kabisa 😄 🤣 😂
 
Kumeibuka utapeli mwingine hivi karibu wa upatu (ponzi scheme) ijulikanayo kama LBL ambako wananchi wengi wanaweka fedha zao ili kuvuna. Huu ni mwendelezo wa yale yaliyotokea awali kama Deci, QNet, ClubD9, Kalinda na Kuku.

Kabla wananchi wengi hawajawa wahanga wa uhalifu,tunaviomba vyombo vya usalama viwachukulie hatua za kisheria wahusika wote wa uhalifu huu.
Wananchi hawajifunzi times and times again? Even serikal itaona mzigo sana kama wananchi vichwa vigumu
 
Wa kwanza kula wa mwisho kuliwa. waliotangulia wamekula na kula na kula tena. sasa hivi lbl ina miezi kama nane, so haijulikani kama itaendelea au lini itakufa. Ni kweli hata mimi nipo nishakula na kula na kula sana. Yani ela niliyoweka ishatoka zaidi ya mara sijui 10. Stake what you are ready to lose. Ni kama kubet
Dm zangu mbona haujibu.
 
unabonyeza withdraw, unaandika kiasi na withdraw password then unasubmit, mpunga unaingia kwenye mpesa yako
Kiasi cha kuanza kutoa ni ngapi na ni lazima uwe na m pesa ndo utoe hela
Lain nyingine azikubali kwani?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom