Je, LBL sio Matapeli kama Matapeli wengine?
Status
Not open for further replies.
Kumeibuka utapeli mwingine hivi karibu wa upatu (ponzi scheme) ijulikanayo kama LBL ambako wananchi wengi wanaweka fedha zao ili kuvuna. Huu ni mwendelezo wa yale yaliyotokea awali kama Deci, QNet, ClubD9, Kalinda na Kuku.

Kabla wananchi wengi hawajawa wahanga wa uhalifu,tunaviomba vyombo vya usalama viwachukulie hatua za kisheria wahusika wote wa uhalifu huu.
haya mambo yanatabu sana imagine kituo cha habari kikubwa kama ITV kimewapa promo hawa watu, kama ilivokua kwa ile "kaylinda" nilitegemea hadi sasa wawe wametoa tamko lolote maana wakiwa kimya inakua kama endorsement fulani.

na ikumbukwe hizi kampuni siku hizi zinajisajili ila wanachoenda kujisajili sio wanachokuja kukifanya huku ground. kwahiyo ukiishia kuangalia usajili tu unapotea.

kila la kheri
 
Dogo baada ya kunifowadia hayo ikabidi nimuulize maswali haya

Ntaomba vithibitisho vifuatavyo ukinipa soon na mimi ntajiunga na wewe
  • HQ za hio kampuni zipo wapi?
  • Leseni za uthibitsho wa kuthibitisha kuwa ni kampuni halali ya kurun bussiness Tanzania kutoka BRELA na mamlaka mengine husika
  • Mawasiliano yao endapo utapata changamoto yoyote
Yangu ni hayo tu
Hivi huwezi kuvipata kila mmoja atakwambia ana meneja wake na chain itakwenda itakurusha Kenya na Nigeria na ukienda kwa huyo meneja wa Kenya au Nigeria atakwambia meneja wake yuko Marekani
 
Jukumu la serikali ni kuhakikisha ulinzi wa raia na mali zao,na kuhakikisha sheria zinafuatwa. Sheria zinakataza ponzi scheme. Ujinga wa raia hauondoi jukumu hilo
Ila usisahau kwamba polisi na mahakama hawawezi kumkamata au kumfunga mtu bila kuletewa mashitaka.
Sasa ni kazi ya raia kwenda kutoa malalamiko polisi halafu ndio uchunguzi uanze kufanywa.
Sifurahii vitendo vya utapeli lakini kwa hili nakiri kweli wajinga bado ni wengi
 
Sasa kuna nyingine hiyo ina faida kinoma kama kawaida wa kwanza kula wa mwisho kuliwa nisharuka nayo. hiyo 200k inakupa 28500 kila siku na hufanyi chochote. imeanza tarehe nne nimeiwahi mapema msemo ni ule ule wa kwanza kula wa mwisho kuliwa.
Naoba link ndugu
 
Kwa wale watu wanaopenda Side hustle kuna hii issue ya LBL hii kampuni Ina deal na matangazo ya movie Zinazotoka na zile zilizowahi ku trend kazi yako wew ni kuwa una view Yale matangazo kwa 10 sec then mpunga unaingia ku withdraw pesa yako ni anytime

Note: kuna kiingilio Cha kupanda level
Level zipo tofauti ila nzuri ni level 2 na 3
Level 2 mtaji ni 150,000/= unaingiza 30,000 kwa week.
Level 3 mtaji ni 540,000/= unaingiza 125,000 kwa week
Pia ukialika ama kualikwa unapewa bonasi.

Kazi kwako
 
Mnaenda kupigwa shitukeni watu walishapigwa uko kitambo, ni mtu anaandaa system yake na pesa zake kama million 4-7 inakuwa mtaji.
Alafu mnaaminishwa kwa kutoa faida kwa level fulani, ikifikia mda watakuja na ofa kuwa level fulani kama unatakiwa kuingia na kiasi fulani basi leo ni offer utakiwi kuingiza watu upande level wewe weka kiasi cha level yako utapandishwa ndio siku ya kupigwa hiyo, au mtu anazima tu system yake akishaona kuwa pesa aliyoweka imeshaingiza faida yake, watu wanaofaidika na michezo hii ni wa mwanzoni tu.... kinachofata ni maumivu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom