Je, LBL sio Matapeli kama Matapeli wengine?
Status
Not open for further replies.
Sasa kuna nyingine hiyo ina faida kinoma kama kawaida wa kwanza kula wa mwisho kuliwa nisharuka nayo. hiyo 200k inakupa 28500 kila siku na hufanyi chochote. imeanza tarehe nne nimeiwahi mapema msemo ni ule ule wa kwanza kula wa mwisho kuliwa.
Inaitwaje mkuu
 
Maelezo yao:

I
LEWE LBL

💠💠TANZANIA ADVERTISING MEDIA LIMITED
💠💠

✅LBL Imeanza tangu mwaka 1967

✅LBL
kirefu chake ni Leo burnett London

♻️Hapa Tanzania imeingia mwaka huu mwezi wa pili baada ya kualikwa na serikali yetu ya jamuhuri ya Muunguano wa Tanzania. Baada ya usajili na kukamilisha taratibu zote ikaanza kufanya kazi rasmi mwezi wa saba mwaka huu.

♻️Hapa manispaa ya Morogoro mtu wa kwanza/muasisi wetu ni Dr David Lugomela ambaye ndiye kiongozi wetu mkuu na kutushirikisha fursa hii.

♻️ LBL inafanyaje kazi.
Kumbuka ni kampuni inayohusiana na utangazaji. Ni kampuni iliyobobevu duniani.
1. Makampuni mengi makubwa ya filamu dunia. Wale wapenzi wa movie mtaelewa hili. Mfano.
🌀 *Paramount,
🌀20th century Fox,
🌀 destiny* ,
🌀Warner Brothers,
🌀DreamWorks picture,
🌀Universal Picture
🌀MGM Picture na mengine mengi
Yameweka ubia na kampuni ya LBL isaidie kutangaza matangazo yao ya movie na filamu ili yawafikie watu wengi duniani.
Hivyo basi ili kampuni ya LBL ifanye jukumu hilo vyema wakaona iajiri watu wengi ambao watatazama matangazo ya movie na hapo idadi ya watu wengi itafikiwa. Ndo mana inasisitiza kualika watu zaidi

🔰 _Baada ya muda wanapeleka kwa makampuni na kuwaonesha mfano:...........
_
🌀*PARAMOUNT * movie yako hii imetazamwa na watu milioni 10.5 mwezi huu.( Utakuta walikubaliana hivi kwamba Kila viewers mmoja( mtu mmoja aliyetazama) Lbl watalipwa Dola 1. Hebu jaribu kuchukua Dola 1 × mil 10.5 LBL wanaingiza. Kwanini wasirudishe fadhira. Hivyo ndivy LBL Inavyofanya kazi.

✅UZOEFU
_Wengi wetu twajua nyakati hizi wengi hupata pesa Kwa mitandao.

_Diamond huingiza fedha YouTube kwa kuwa tu na viewers wengi.

_MiladAyo anaingiza fedha Kwa kuwa tu na viewers wengi

🖊️Note vipi wewe unayetazama kazi zao unalipwa ? Au unagharamika bando lako?

♻️LBL UNAPOVIEW video hawakuachi hivihivi. Kwasababu wanajali ikiwa tunawaingizia fedha nyingi sana basi wakaona nasi tupate kifuta jasho. Ambacho kwetu kinathamani Kubwa, kwa level tofauti kama ifuatavyo........... 👇

1️⃣ P1 LEVEL

_💠Ukiweka 50,000
💠Unapewa picha 5 za kuangalia
💠Kila picha unalipwa 335
💠Kwa siku unalipwa 1675
💠Kwa mwezi unalipwa 50250
💠Kwa mwaka 611,375 /=_

2️⃣ P2 LEVEL

💠Ukiweka 150,000
💠Unapewa Picha 10 za kuangalia
💠Kila picha unalipwa 500
💠Kwa siku unalipwa 5000
💠Kwa mwezi 150,000
💠Kwa mwaka 1,825,000
💠Hivyo 150,000 itakuwa imezaa sh 1,675,000

💠Ukiweka 540,000
💠Unapewa picha 15 za kuangalia
💠Kila picha unalipwa 1200
💠Kwa siku unalipwa 18000
💠Kwa mwezi 540,000
💠Kwa mwaka 6,570,000
💠Hivyo 540,000 itakuwa imezaa 6,030,000 /

✳️ILI kujiunga nijulishe nikutumie Link.

✳️Kujiunga na LBL * ni bure kabisaa ila ili uwe mwajiriwa au mfanyakazi rasmi wa LBL unatakiwa kuwa na mtaji wa *50000/= kwa ngazi ya P1 , 150000/= kwa ngazi ya P2, na 540000/= kwa ngazi ya P3 Kumbuka hakuna biashara unayoweza ifanya kama hauna mtaji ni lazima uwe na mtaji. ukikamilisha account yako nitakuadd kwa group la WhatsApp
UTAKUWA TAYARI UANZE KAZI💠💠

🔰MWISHO
.
✳️ LBL MAFANIKIO ni hakika
✳️LBL sio matapeli. Tuwe makini na matapeli watakao jitokeza na kuharibu sifa ya kampuni.

✳️Hii ni kazi sio kamali au bahati nasibu .
✳️Usipoview huwezi pata pesa Kwa sababu nao hawajapata pesa kupitia wewe."
Mwisho wa kunukuu.
_____________________________


Baada ya kupitia maelezo haya nikaanza kuchimba kuhusiana na kampuni ya LBL:

Leo Burnett London (LBL
) ni tawi la Leo Burnett, ambayo ni mojawapo ya makampuni makubwa ya matangazo duniani, iliyoanzishwa na Leo Burnett mwaka 1935 huko Chicago, Marekani. Leo Burnett London ni sehemu ya McDonald's, Procter & Gamble, Coca-Cola, na wateja wengine wakubwa.

Historia ya LBL: Leo Burnett London imejizolea umaarufu kwa kutoa ubunifu wa matangazo na mikakati ya uuzaji kwa wateja wake. Kampuni imejulikana kwa kuunda kampeni maarufu na za ufanisi. Kwa mfano, wameunda matangazo maarufu kama ya "Proud to be a Coke" kwa Coca-Cola na "Because You're Worth It" kwa L'Oréal.

Kazi ya Leo Burnett London: Leo Burnett London inajivunia kuwa na timu ya wabunifu na wataalamu wa mikakati ambao huunda matangazo ya kuvutia na yenye athari kubwa. Kampuni ina mchanganyiko wa ubunifu na utafiti wa soko ambao husaidia wateja kufikia malengo yao ya biashara.

Pesa Wanazopata: Leo Burnett London inapata pesa kupitia huduma za utangazaji, mikakati ya uuzaji, ubunifu wa matangazo, na huduma nyingine za ushauri wa biashara kwa wateja wao. Hii inajumuisha:

1. Malipo ya Kampeni za Matangazo: Wanapofanya kampeni kwa wateja, kampuni hulipwa kulingana na ukubwa na aina ya kampeni.

2. Konsati na Ushauri: Wanatoa ushauri wa kimkakati na huduma za ubunifu kwa wateja kwa malipo ya huduma hizi.

3. Kuuza Huduma za Utafiti: Wateja wanalipa kwa tafiti za soko na uchambuzi wa maoni ya walaji.

Kwa hiyo, mapato yao yanatokana na huduma zao za utangazaji na mikakati, siyo kutoka kwa malipo ya views au kitu kingine cha moja kwa moja kutoka kwa watumiaji wa media.

Hivyo: Leo barnet london wao ndiyo hulipwa na kampuni tofauti kwa kufanya ubunifu wa matangazo tofauti tofauti kwenye Radio, channel za Tv, mitandaoni n.k ikiwemo movie Trailors.

Zingatia kitu kimoja hapo wao ndiyo wanalipwa hawalipi.

Nikaona niulizie zaidi kupata uhakika, wote tunajua chatGPT inakusanya taharifa kila sehemu ya mtandao, majibu yakawa hivi;View attachment 3190403

Ieleweke LBL sio matapeli wala hawahusiki na kulipa kwa namna yeyote ile.

Ila hao jamaa wanaotoa matangazo haya nfiyo matapeli, wanachafua jina la kampuni hiyo.

Cc: NoncChalant
Nakushukuru kwa utafiti na kushare na sisi.
 
Yaani wewe unamawazo kama yangu, Mimi mwenyewe ni member na ninalipwa 18,000 kila siku kwa kutizama movies 15 kwa sekunde kumi kumi tu, Hadi waamue kuchochola mie nitakuwa nimepiga zangu nyingi sana 😂😂
Safi kabisa hiyo ndo akili,na kila wiki unatakiwa uinyofoe hiyo pesa hata siku wakipotea unakuwa umeshawapiga vya kutosha
 
Sasa kuna nyingine hiyo ina faida kinoma kama kawaida wa kwanza kula wa mwisho kuliwa nisharuka nayo. hiyo 200k inakupa 28500 kila siku na hufanyi chochote. imeanza tarehe nne nimeiwahi mapema msemo ni ule ule wa kwanza kula wa mwisho kuliwa.
Tupe code mkuu tujilipue.
 
Niko na Account tatu hapo za P3 nimeshapata nusu ya hela niloweka bado nusu namm niongoke na majeraha ya kupoteza fedha in case mtambo ukizimwa
 
Niko na Account tatu hapo za P3 nimeshapata nusu ya hela niloweka bado nusu namm niongoke na majeraha ya kupoteza fedha in case mtambo ukizimwa
Mkuu sio wajinga wale wana hesabu zao walishazipiga muda sanaaa ambapo wanaweza asilimia tano wakanufaika kisha tisini na tano waliobaki ikawa mbona wewoooooo
 
Dogo baada ya kunifowadia hayo ikabidi nimuulize maswali haya

Ntaomba vithibitisho vifuatavyo ukinipa soon na mimi ntajiunga na wewe
  • HQ za hio kampuni zipo wapi?
  • Leseni za uthibitsho wa kuthibitisha kuwa ni kampuni halali ya kurun bussiness Tanzania kutoka BRELA na mamlaka mengine husika
  • Mawasiliano yao endapo utapata changamoto yoyote
Yangu ni hayo tu
Kaka kwema, nimeona hii LBL inazidi kumea na imekua registered brela.. wamefungua ofisi hapa Tanzania moja ikiwepo koani morogoro na baraka inapata toka kwa waziri wetu wa fedha.. nini maoni yako kabla sijajiunga maana tayar nimeshawishika.
 
Kaka kwema, nimeona hii LBL inazidi kumea na imekua registered brela.. wamefungua ofisi hapa Tanzania moja ikiwepo koani morogoro na baraka inapata toka kwa waziri wetu wa fedha.. nini maoni yako kabla sijajiunga maana tayar nimeshawishika.
Waziri wa fedha kabariki lini? Ukipata mda ingia fb then andika "Kalynda Tanzania" hope utajifunza kitu then baada ya kujifunza naamini utaamua ujiunge au uache
 
Sasa kuna nyingine hiyo ina faida kinoma kama kawaida wa kwanza kula wa mwisho kuliwa nisharuka nayo. hiyo 200k inakupa 28500 kila siku na hufanyi chochote. imeanza tarehe nne nimeiwahi mapema msemo ni ule ule wa kwanza kula wa mwisho kuliwa.
Mkuu naitaka hii nijilipue!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom