Maelezo yao:
ILEWE LBL
💠💠TANZANIA ADVERTISING MEDIA LIMITED 💠💠
✅LBL Imeanza tangu mwaka
1967
✅LBL kirefu chake ni
Leo burnett London
♻️Hapa Tanzania imeingia mwaka huu mwezi wa pili baada ya kualikwa na serikali yetu ya jamuhuri ya Muunguano wa Tanzania. Baada ya usajili na kukamilisha taratibu zote ikaanza kufanya kazi rasmi mwezi wa saba mwaka huu.
♻️Hapa manispaa ya Morogoro mtu wa kwanza/muasisi wetu ni
Dr David Lugomela ambaye ndiye
kiongozi wetu mkuu na kutushirikisha fursa hii.
♻️
LBL inafanyaje kazi.
Kumbuka ni kampuni inayohusiana na utangazaji. Ni kampuni iliyobobevu duniani.
1. Makampuni mengi makubwa ya filamu dunia.
Wale wapenzi wa movie mtaelewa hili. Mfano.
🌀 *Paramount,
🌀20th century Fox,
🌀 destiny* ,
🌀Warner Brothers,
🌀DreamWorks picture,
🌀Universal Picture
🌀MGM Picture na mengine mengi
Yameweka ubia na kampuni ya LBL isaidie kutangaza matangazo yao ya movie na filamu ili yawafikie watu wengi duniani.
Hivyo basi ili kampuni ya LBL
ifanye jukumu hilo vyema wakaona iajiri watu wengi ambao watatazama matangazo ya movie na hapo idadi ya watu wengi itafikiwa.
Ndo mana inasisitiza kualika watu zaidi
🔰 _Baada ya muda wanapeleka kwa makampuni na kuwaonesha mfano:...........
_
🌀*PARAMOUNT * movie yako hii imetazamwa na watu milioni 10.5 mwezi huu.( Utakuta walikubaliana hivi kwamba Kila viewers mmoja( mtu mmoja aliyetazama) Lbl watalipwa Dola 1. Hebu jaribu kuchukua Dola 1 × mil 10.5 LBL wanaingiza. Kwanini wasirudishe fadhira. Hivyo ndivy LBL Inavyofanya kazi.
✅UZOEFU
_Wengi wetu twajua nyakati hizi wengi hupata pesa Kwa mitandao.
_Diamond huingiza fedha YouTube kwa kuwa tu na viewers wengi.
_MiladAyo anaingiza fedha Kwa kuwa tu na viewers wengi
🖊️Note vipi wewe unayetazama kazi zao unalipwa ? Au unagharamika bando lako?
♻️LBL
UNAPOVIEW video hawakuachi hivihivi. Kwasababu wanajali ikiwa tunawaingizia fedha nyingi sana basi wakaona nasi tupate kifuta jasho. Ambacho kwetu kinathamani Kubwa, kwa level tofauti kama ifuatavyo........... 👇
1️⃣ P1 LEVEL
_💠Ukiweka
50,000
💠Unapewa picha
5 za kuangalia
💠Kila picha unalipwa
335
💠Kwa siku unalipwa
1675
💠Kwa mwezi unalipwa
50250
💠Kwa mwaka
611,375 /=_
2️⃣ P2 LEVEL
💠Ukiweka
150,000
💠Unapewa Picha
10 za kuangalia
💠Kila picha unalipwa
500
💠Kwa siku unalipwa
5000
💠Kwa mwezi
150,000
💠Kwa mwaka
1,825,000
💠Hivyo
150,000 itakuwa imezaa sh
1,675,000
💠Ukiweka
540,000
💠Unapewa picha
15 za kuangalia
💠Kila picha unalipwa
1200
💠Kwa siku unalipwa
18000
💠Kwa mwezi
540,000
💠Kwa mwaka
6,570,000
💠Hivyo 540,000 itakuwa imezaa
6,030,000 /
✳️ILI kujiunga nijulishe nikutumie Link.
✳️Kujiunga na
LBL * ni bure kabisaa ila ili uwe mwajiriwa au mfanyakazi rasmi wa LBL unatakiwa kuwa na mtaji wa *50000/= kwa ngazi ya
P1 ,
150000/= kwa ngazi ya
P2, na
540000/= kwa ngazi ya
P3 Kumbuka hakuna biashara unayoweza ifanya kama hauna mtaji ni lazima uwe na mtaji. ukikamilisha account yako nitakuadd kwa group la WhatsApp
UTAKUWA TAYARI UANZE KAZI💠💠
🔰MWISHO .
✳️ LBL MAFANIKIO ni hakika
✳️LBL sio matapeli. Tuwe makini na matapeli watakao jitokeza na kuharibu sifa ya kampuni.
✳️Hii ni kazi sio kamali au bahati nasibu .
✳️Usipoview huwezi pata pesa Kwa sababu nao hawajapata pesa kupitia wewe."
Mwisho wa kunukuu.
_____________________________
Baada ya kupitia maelezo haya nikaanza kuchimba kuhusiana na kampuni ya LBL:
Leo Burnett London (LBL) ni tawi la Leo Burnett, ambayo ni mojawapo ya makampuni makubwa ya matangazo duniani, iliyoanzishwa na Leo Burnett mwaka 1935 huko Chicago, Marekani. Leo Burnett London ni sehemu ya McDonald's, Procter & Gamble, Coca-Cola, na wateja wengine wakubwa.
Historia ya LBL: Leo Burnett London imejizolea umaarufu kwa kutoa ubunifu wa matangazo na mikakati ya uuzaji kwa wateja wake. Kampuni imejulikana kwa kuunda kampeni maarufu na za ufanisi. Kwa mfano, wameunda matangazo maarufu kama ya "Proud to be a Coke" kwa Coca-Cola na "Because You're Worth It" kwa L'Oréal.
Kazi ya Leo Burnett London: Leo Burnett London inajivunia kuwa na timu ya wabunifu na wataalamu wa mikakati ambao huunda matangazo ya kuvutia na yenye athari kubwa. Kampuni ina mchanganyiko wa ubunifu na utafiti wa soko ambao husaidia wateja kufikia malengo yao ya biashara.
Pesa Wanazopata: Leo Burnett London inapata pesa kupitia huduma za utangazaji, mikakati ya uuzaji, ubunifu wa matangazo, na huduma nyingine za ushauri wa biashara kwa wateja wao. Hii inajumuisha:
1.
Malipo ya Kampeni za Matangazo: Wanapofanya kampeni kwa wateja, kampuni hulipwa kulingana na ukubwa na aina ya kampeni.
2.
Konsati na Ushauri: Wanatoa ushauri wa kimkakati na huduma za ubunifu kwa wateja kwa malipo ya huduma hizi.
3.
Kuuza Huduma za Utafiti: Wateja wanalipa kwa tafiti za soko na uchambuzi wa maoni ya walaji.
Kwa hiyo, mapato yao yanatokana na huduma zao za utangazaji na mikakati, siyo kutoka kwa malipo ya views au kitu kingine cha moja kwa moja kutoka kwa watumiaji wa media.
Hivyo: Leo barnet london wao ndiyo hulipwa na kampuni tofauti kwa kufanya ubunifu wa matangazo tofauti tofauti kwenye Radio, channel za Tv, mitandaoni n.k ikiwemo movie Trailors.
Zingatia kitu kimoja hapo wao ndiyo wanalipwa hawalipi.
Nikaona niulizie zaidi kupata uhakika, wote tunajua chatGPT inakusanya taharifa kila sehemu ya mtandao, majibu yakawa hivi;View attachment 3190403
Ieleweke LBL sio matapeli wala hawahusiki na kulipa kwa namna yeyote ile.
Ila hao jamaa wanaotoa matangazo haya nfiyo matapeli, wanachafua jina la kampuni hiyo.
Cc:
NoncChalant