Matovu Godfrey
JF-Expert Member
- Oct 5, 2025
- 986
- 693
Asante saaana wananchi 🔥
Way Forward 🫂🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿📍🔥🔥View attachment 3496166
Msisahau leo #MariaSpaces saa 2 usiku tunajadili Way Forward
Mjadala wa kitaifa njoo uchangie 💪🏽
#MO29 #OktobaTunatoka #tanzania #FreeTunduLissu
SsafiKwisha habari yao
Sikuwai kujua kama ni mweupe hiviMpo salama!
Kwa waliopo Dar hii haijawahi kutokea. Hata siku ya jumapili haiwagi hivi. Barabara ni nyeupe sana sijapata kuona. Fikiria Morogoro road unaweza ukavuka barabara ukiwa umefumba macho. Barabara ambayo kwa hapa Tanzania ndio iko busy 24/7 kwa siku zingine kwani ndio barabara lango la mji wa Darisalama.
Daladala zipo moja moja yaani kila baada ya dakika kumi hivi wakati siku nyingine hapakaliki.
Siku ya leo kama Lisu akichukuliwa akawekwa ndani ya gari siri ya nyuma. Ili aonyeshwe hali ilivyo hakika ataumia kuliko alivyopigwa risasi au kuliko alivyowahi kupata maumivu wakati wowote katika maisha yake.
Hata Polisi, Askari na serikali hawajategemea mambo yawe rahisi kiasi hiki. Wenyewe hawaamini kama Watu wangeweza kuwasaliti wengine kwa kiwango hiki. Hii ndio tafsiri ya Usaliti.
Kwenye maisha yako. Hakuna jambo baya kama kutetea watu wajinga na maskini wasiokuwa tayari kutetewa.
Kwa hizi barabara zilivyo unaanzia wapi kuandamana. Ni nyeupe ajabu. Nilitokea Kimara mpaka ubungo kweupe kuna doria za hapa na pale za askari.
Nimeenda njia ya Mwenge, kisha makumbusho, nimerudi Magomeni mpaka mjini, posta kumepoa. Aiseeh!
Yaani hapa ukibeba bango lako hata askari wenyewe watakucheka sana. Barabara zimekumeza. Unakuwa kioja na kituko.
Nimehoji baadhi ya askari huku kwenye doria kutaka maoni yao kuhusu hali ilivyo wenyewe wanashangaa sana. Wanasema hata kama ni uoga sio wa kiwango hiki. Ni uoga uliopitiliza sana.
Zaidi wanasema wanajisikia uchungu kwa taifa kupata aibu kwa wananchi wake kushindwa hata kujitokeza walau pawe busy na vyombo vya kimataifa vipate kazi ya kufanya.
Upande wa wapiga kura hali yao bado ni mapema kueleza situation ilivyo. Ila baadhi ya watu niliokutana nao asubuhi hii ni kama wanategeana.
Hawaelewi kama watapiga kura au hawatapiga.
Kwa ujumla siku ya leo;
1. Serikali imeshinda, vyombo vya usalama, Dola vimeshinda kwenye hii vita.
Inaweza kuonekana ni jambo rahisi lakini wamejitahidi pakubwa.
Ubao unasoma 2-0 dakika bado ni zamapema.
2. Waandamanaji sio tuu wapo nyuma kwa bao moja lakini pia kimchezo wamezidiwa. Uwanja umeinama.
Hawachezi kama timu. Timu yao imevurugwa na kuvunjwa vunjwa.
3. Kuna uwezekano leo asipigwe hata mtu mmoja. Yaani kusiwe na fujo ya aina yoyotem yaani hata rungu moja hutosikia.
4. Wapiga kura watakuwa wachache sana. Kwa hali Ilivyo.
Ingawaje hii haiwathiri upande wa serikali. Wao lengo lao siku ya leo ipite salama. Pili watakaojitokeza hata kama ni elfu moja haohao watatumika kueleza kwa kulikuwa na uchaguzi.
5. Baada ya siku ya leo nini kitatokea?
a) Waandamanaji watakuwa wamekatishwa tamaa na watakuwa wamepata aibu kubwa ambayo sijui kama itaisha hivi karibuni.
b) Waliokuwa vinara mtandaoni watakasakwa wiki za mwanzoni za mwezi November kisha serikali itaachana na mambo ya uchaguzi kwani hang over na tension ya uchaguzi itakuwa imeisha.
So ni vizuri kama ulikuwa mstari wa mbele kuhamasisha maandamano wiki hizi mbili ujitahidi sana kujificha. Ukifanikiwa basi utakuwa umeokoka.
c) Matusi mitandaoni yatarudi tena kutukana sasa waandamanaji kwa kuwa waoga na kunguru. Kenya watatukana Sana watanzania.
d) Maridhiano ya kitaifa kufanyika na wale waliokamatwa kwa sababu za kisiasa na kiuchaguzi kuachiliwa.
e) Kusafisha baadhi ya taasisi za dini na kuunda sheria mpya zitakazobana taasisi za dini kujihusisha na siasa.
f) Influencers wa mitandaoni kubanwa zaidi na kuwekewa sheria za kitaaluma, na kimaudhui na kikodi.
Kwamba bila kiwango fulani cha taaluma kuna mambo haupaswi kuyajadili mitandaoni kama muanzisha maudhui na influencer.
Ila ku-post mambo personal kama picha zako utapewa uhuru.
g) Bado vuguvugu la waliotekwa, kuuawa na kupotezwa litaendelea kusakama huku kelele za wanaharakati mmojammoja wakiwa wanajitahidi kukumbushia.
h) serikali muda huo itafanya jitihada kuwasahaulisha watu habari hizo na mambo ya kukamatana kamatana baada ya mwezi mmoja kuelekea 2026 yatapotea. Jambo ambalo litafanya wale wanaharakati wanaokumbushia utekaji n mauaji kuchokwa na watu kama sio kupuuzwa.
I) mwaka 2026 utakuwa mwaka wa kitofauti sana.
J) Lisu atakuwa ameachiwa lakini atakuwa amekata tamaa. Sio kwa sababu ya kunyoroshwa na Serikali bali kutokana na Wale anaowapigania kumnyorosha, kumsaliti na kumtelekeza.
Poleni wote. Hayo ndio maisha.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Ana ujuaji wa kijinga. Anaijiita taikuni wa fasihi. Hapo ukimuuliza kwa nini usingesubiri hata saa 4 ndio uandike, atakosa jibu.Sikuwai kujua kama ni mweupe hivi
Sikuwai kujua kama ni mweupe hivi
Siku hazigandi!Ila wabongo kwa mikwara hawajambo dada wa watu kaacha kufanya udaku ambao ulikuwa unamuingizia pesa nyingi kwa kupost habari za mastaa wakibongo na wasanii wengine amekosana nae kwa sababu tu ya hili vuguvugu la maandamano yaliandaa the end of the day kaangushwa na wabongo Wewe umeona wapi maandamano yanapangwa. Wale mabingwa wakuongea humu jukwaani mbona hatuoni clip zenu mkiandamana?
Humu tunawaambiaga sana CCM bado ni chama chenye nguvu bado hatujapata chama mbadala tishio huwa ninaonekana Kama Mimi ni CCM hiki chama kimewin nchi Kwanza ukiingia kwenye mpira wanazirun Simba na Yanga na viongozi wao, Wana wahold wasanii karibia wote wa Sanaa, ukienda kwenye majeshi na polisi Kuna wanachama wao, mahakama na kwenye watumishi wa umma vile vile wapo wengi mule na hata ukija kwenye mavyuo ndio usiseme ukienda uko vijijini ndio kabisa na ndio maana wakikwambia Wanawanachama zaidi ya mil 12 usione waongo kwa namna hii hiki chama kinatokaje madarakani?
Chama ambacho mnakitegemea cha upinzani Chadema huwa hakijui Nini kinafanya kinaenda bila muelekeo na shida ya hiki chama Wanaona CCM Kama kidogo in short wa underestimate badala wa kubali ukubwa wao ili ujue unaanzia wapi kukikabili lakini huoni hicho Wala strategy zozote alafu wanadanganya unabeba nchi