Ukiwasikiliza wanaharakati unaweza kudhani kuwa muda wowote ule huko mtaani watu wataanza kuchinjana.
Diamond ni mtafutaji wa riziki kupitia muziki, anayo haki ya kuipamba CCM kama wanamlipa pesa nzuri.
Sasa kama kuna unyama umefanyika wenye kuihusu CCM Diamond kama mwanamuziki hata asingeimba nyimbo za siasa bado angekuwa hana ubavu wa kuufanya unyama huo usifanywe popote ulipofanyika.
Hao watu 15,000 ni wachache sana kulinganisha na mamilioni ya watu waliosimama barabarani kumuaga JPM na wengine wakatandika kanga zao ili matairi yazikanyage.
Diamond anaweza kushinda hiyo tuzo na akaendelea kuimba nyimbo za CCM na bado hizi harakati za wanaharakati zisiathiri muziki wake.
Nongwa za kipuuzi kama hizi za activists ni sawa sawa na zile za miaka ya 1980 mwanzoni wakati Nico Njohole alipotakiwa kufanya majaribio Arsenal halafu viongozi wa FAT wakamuwekea mizengwe.
Nongwa kama hizi zilimnyima Mwameja nafasi ya kucheza timu ya ligi daraja la kwanza Uingereza.