Je, Mwanamke ana wajibu wa kuchangia kifedha ndani ya Ndoa?

Hawataki hiyo Nina wasiwasi hawana ndoa hawa Bado vijana, mwenzao huko wiki mbili anataka kuvunja ndoa.
 
umenena vyemaa
 
Kinacho watesa nyinyi wanawake wa sasa ni ubinafsi, ww umeolewa kwa lengo la kwenda kujenga familia moja iweje ufike kwenye ndoa utake kutafuta mafanikio nje ya familia unayo ijenga?
 
Hizo tabia za kisukuma bwana wewe, familia masikini alaumie mke mvivu? Kwetu hakuna mfumo dime wakunyanyasa mke, kama umasikini wa familia ataulizwa baba kashindwa kuongoza familia, baba mbele mke nyuma , sio mke kumfañya kama mfugo wako hapana!
 
Sasa hapo si tiyari kipato chako kimechangia majukumu ya kufamilia?

Sisi tunaongelea wanawake wasio taka pesa yake kuguswa.
Ndio sio lazima ni hiari. Hata wasipotaka hakuna kosa lolote. Mwanaume pambana..ndoa umeitaka mwenyewe
 
Oa kwanza baada ya miaka 5 uje hapa
 
Kulea watoto unamaanisha nini? maana naona mmeshikiria sana hicho kipengere kama justification ya nyie kutojumuishwa kwenye bill za familia.

Embu fafanua unamaanisha kulea watoto kiaje. Kwamba wapate mahitaji yao ya chakula, mavazi, malezi na out za hapa na pale au unamaanisha na sisi wanaume tuwabebe watoto mgongoni twende nao kwenye mizunguko yetu
 
Mwanaume ndiye mwenye majukumu ya kugharamia mahitaji ya mke,watoto na familia kwa ujumla.
Majukumu ya mke ni kumtii mumewe na kumheshimu katika mambo halali,kumpa mapenzi na msaada wa kihisia pamoja na kulea watoto.
Hayo yote atayafanyaje wakati kutwa kiguna njia kutafuta hela?
Mwanamke ana amka 11:00 asubuhi ana rudi ndani saa 4 za usiku huo muda wa kuhudumia watoto na kukuonesha mapenzi anautoa wapi?
 
Hizo tabia za kisukuma bwana wewe, familia masikini alaumie mke mvivu? Kwetu hakuna mfumo dime wakunyanyasa mke, kama umasikini wa familia ataulizwa baba kashindwa kuongoza familia, baba mbele mke nyuma , sio mke kumfañya kama mfugo wako hapana!
Umezungumza hisia zako sio uhalisia. Nenda kafatilie watangulizi wa ukoo wako waliishije. Tanzania hii zaidi ya 90% walikuwa wakulima na wafugaji na waliishi kwenye hiyo misingi niliyoizungumza.
 
Binti kamaliza form four huo uchumi anaipata wapi halafu baadaye mnataka bikira zenye miaka kuanzia 25! Kweli?
Kwahiyo wewe unaoa watoto? Anatakiwa apate muda wa kutosha wa kujiendeleza kielimu na kiuchumi pia
 
Samahani, lakini siungi mkono mtazamo huu. Nadhani ndoa inapaswa kuwa ni ushirikiano wa pande zote mbili, na kila mmoja akichangia kwa njia yake, iwe ni kifedha, kihemko, au katika malezi ya familia. Kutoa ni hiari, lakini inapaswa kutokana na mapenzi, heshima, na kuelewana, siyo kwa kulazimishwa. Sidhani kama kumwambia mwanamke afanye kazi ili kuchangia kwa lazima ndiyo suluhisho la changamoto yoyote inayojitokeza. Ndoa inahitaji ushirikiano na siyo kutoza au kutoa, bali kuelewana na kusaidiana.
 
Hayo yote atayafanyaje wakati kutwa kiguna njia kutafuta hela?
Mwanamke ana amka 11:00 asubuhi ana rudi ndani saa 4 za usiku huo muda wa kuhudumia watoto na kukuonesha mapenzi anautoa wapi?
Hehehe!!!
 
Kwa kifupi, mwanaume ndiye anayeongoza kifedha, lakini mke anaweza kusaidia kwa hiari kulingana na hali ya familia
Hakuna hiari, kama anaingiza pesa ni lazima pesa yake iwe na mchango kwenye familia yake.

Hizi ni fikra za kimasikini, kama mke anakipato unganisheni nguvu mjenge uchumi mzuri wa familia yenu.

Watu wanazeekea kwenye upangaji kwa mambo ya kijinga kama haya, eti anaogopa jamii itamcheka mke kashiriki ujenzi. Huu ujinga kwangu hauna nafasi.

Huu ujinga ndio unazalisha taifa masikini, kwasababu watafutaji ni wachache ila wategemezi ni wengi sana na hakuna uwiano. Yani ni wastani wa mtu mmoja kuwa na wategemezi zaidi ya 10, kipato chako chote kinakombwa na mahitaji ya wategemezi.
 
Basi hapa hatuongelei familia moja moja tunaongelea kwa ujumla. Katika hali ya kawaida kabisa kitendo cha kuwa na kipato maana yake unaondoka kwenye kundi la watu tegemezi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…