Halafu tukisema humu mwanamke mwenye kazi/kipato hana faida yoyote kwenye ndoa ni mara mia ya mama wa nyumbani, tunaonekana ni watu wa ajabu...!!Tupo kwenye ulimwengu ambao tuna fursa sawa za elimu, biashara, uongozi n.k. Kwa nyakati hizi mwanamke mwenye kipato sio hiari tena kushiriki kujenga uchumi wa familia yake.
Nimeshuhudia huu ujinga mtaani kwangu, mume uchumi umeyumba ikabidi watoto warudi shule za kayumba kutoka shule binafsi walikokuwa wanasoma tokea wakiwa wadogo, ili kukabiliana na ukata.
Mke anafanya biashara ya nafaka na kukopesha ela za riba, anakipato ambacho kama wangeunganisha nguvu wale watoto wasingerudi kayumba. Inasemekana mama alinukuliwa kwenye vyama vya kinamama akisema hawezi kusomesha watoto hilo sio jukumu lake.
Mwanaume wangu kwenye ndoa atafanya majukumu yake ya kifedha kama inavyotakiwa, na mimi nitamsaidia kwa hiari na upendo. Kuwa strong and fearless haimaanishi kutokuheshimu mfumo wa ndoa au kusaidiana. Ni kuhusu kujitegemea kihisia na kifedha, lakini bado kushirikiana kwa upendo na mwenzako.😀😀😀 strong and fearless woman anataka kulipiwa bill zake na mwanaume
Wewe hauna ndoa na mawazo ulioyonayo ni simp tu ndio anaweza kukuoaMwanaume wangu kwenye ndoa atafanya majukumu yake ya kifedha kama inavyotakiwa, na mimi nitamsaidia kwa hiari na upendo. Kuwa strong and fearless haimaanishi kutokuheshimu mfumo wa ndoa au kusaidiana. Ni kuhusu kujitegemea kihisia na kifedha, lakini bado kushirikiana kwa upendo na mwenzako.
Sasa mbona mie sijakulia wala kuzaliwa uswahilini kama wewe na mkeo mnakoishi, sema hivi ukiwa na pesa ya kuunga unga lazima ujue kila kinachoingia kwa mkeo, ila pesa ikiwepo hakunaga maswali ya hivyo mme anakamilisha sehemu yake na mke akikuta mambo hayajakaa sawa anakamilisha, tafuta pesa, sasa ikitokewa elf 10 lazima aulize change iko wapi! Usifikiri wanawake wote humu wanaochangia wapi uswazi!Hapana mke wangu ni mwanamke mwelevu sana na anajua ninafanya mambo kwa logic hivyo basi hata siku moja hawezi kuniona mimi nina roho mbaya.
Nyie wanawake wenye akili ndogo hasa mliokulia uswahilini ambao mkiingia ndoani mnakuwa parasite, mnataka kutumia hela za mwanaume kuholela holela kisa tu ni mumeo, mara nyingi ndio mnapenda kuitumia hii kauli ya "una roho mbaya" hasa pale mume asipokubalina na wewe kwenye jambo fulani la kifedha.
Wanawake wenye parasitic mentality kama wewe ni hasara kubwa sana kwa mwanaume.
Hayo majukumu mengine yanapatikana kukiwa kwanza na uhakika wa kipato.Ndoa si biashara ya kugawana mizigo kwa usawa wa asilimia. Kila mmoja anatoa kulingana na uwezo wake, na mchango wa mwanamke si lazima uwe wa kifedha. Kama mke anahakikisha nyumba iko sawa, watoto wanalelewa vyema, na familia inapata utulivu, huo tayari ni mchango mkubwa kuliko pesa. Familia ni ushirikiano, si hesabu za kugawana bili.
Bongo hii hii na wengi wanaotumia nguvu kupika,kufua kudeki na kazi ndogo ndogo ni vile eidha hawajui uwepo wa vitendea kazi au basi wanapenda maana hawana kazi ya kufanya.Kazi zipi zakumalizwa na machine? Kwa bongo hii au nchi nyingine? Hapa hapa mkuranga watu wapo wangapi wanamaliza kazi Kwa machine! Simu zinapotisha hizi
Hawana uwezo wakuzinunua, mtu kapanga chumba kimoja au chumba na ukumbi umeme tu kulipa ni ugomvi hizo machine vipi, siku zile mbili watu walizuiwa kwenda katikati ya mji, angalia watu walivyolalamika hizo machine wapi na wapi!Bongo hii hii na wengi wanaotumia nguvu kupika,kufua kudeki na kazi ndogo ndogo ni vile eidha hawajui uwepo wa vitendea kazi au basi wanapenda maana hawana kazi ya kufanya.
Kama hawana uwezo washirikiane tu, mwenye uwezo wa hiki afanye.Hawana uwezo wakuzinunua, mtu kapanga chumba kimoja au chumba na ukumbi umeme tu kulipa ni ugomvi hizo machine vipi, siku zile mbili watu walizuiwa kwenda katikati ya mji, angalia watu walivyolalamika hizo machine wapi na wapi!
Zamani jukumu la kuhudumia familia lilikua ni la Mwanaume kabla ya 50/50 mabibi zetu walikua nyumbani Wakulea familia na kutimiza majukumu mengine ya NyumbaniUhodari mwingi sana kwneye kuelezea hali ilivyokuwa hapo zamani. Ni kwa vile bibi na mama zetu walivumilia sana kunyanyaswa kiuchumi, kila kitu ngoja baba aje. Haufafahamu hili sababu walikuwa hawalalamiki wala kuonesha kwa watoto wao. Lakini walihakikisha binti zao hawapitii waliopitia wao, zaidi wanapofiwa au kutelekezwa na mwanamme, au kipindi mwanamme anafuja mali kwenye jambo lisilo na manufaa kwa familia/watoto. Wamama hawa walibebea 'resentment' juu ya baba zenu, matokeo yake ikawa watoto wanapokuwa wakubwa, masaada mkubwa zaidi anapewa mama au tuseme anakumbukwa zaidi (si tunajionea wenyewe kwenye jamii zetu?) japo baba yupo hai na ndio aliyevuja jasho na damu kuwalea.
Pesa anayopata unaitolea macho ya nini? Kuhudumia familia kifedha narudia ni jukumu la mwanamme. Ukosefu wa wababa wengi wanaoelewa majukumu yao limekuwa jambo la kawaida kwenye jamii ya sasa. matokeo yake tunapata vijana ambao hawaoni umuhimu wa kuhudumia familia zao sababu hawana mfano unaoeleweka wa kiume. Wanaona mama zao walipambana na hivyo wake zao wapambane, hapana kubwa sana
Hukuwahi kukaa na bibi zako wakusimulie maisha ya zamani? Hawakuwa na pakusemea waliumizwa walilia vifuani, na wababa watesa wake zao hawanaga maisha marefu sana , wengi wake zao walibakia na kuishi muda mrefu sanaZamani jukumu la kuhudumia familia lilikua ni la Mwanaume kabla ya 50/50 mabibi zetu walikua nyumbani Wakulea familia na kutimiza majukumu mengine ya Nyumbani
Sasa katika Dunia ya sasa Wanawake wengi mnadai haki Sawa 50/50 na mmepewa hizo haki tena mmependelewa kwasababu now ukienda kuomba kazi ni bora ukutane na mwanaume mwenzako mtashindana ukikutana na mwanamke jua lazima apendelewe, ukicheki kwenye elimu mtoto wa kiume na wakike wakipata Div 3 jua mtoto wa kike ataenda A level wakiume atatafutiwa uelekeo mwengine, Yan imekuwa sio gender equality tena bali gender equity kumpendelea mmoja badlaa ya mwengine.
Mbaya zaidi mkiambiwa kuwa haki sawa ni lazima iendane na usawa wa kimajukumu still Hamtaki, yan mnataka mpewe fursa sawa na Wanaume na bado mmepndelewe lakini kwenye kutimiza Wajibu mnataka Mwanaume akae mbele kwa kisingizio kuwa ni jukumu lake OK kama pesa yako haina mchango kwa familia yako nini maana ya wewe kufanya kazi,,, Yan unaishi na mwanamke hata kukiwa na shida ya 50K hawezi kuitoa kisa eti yeye ni mwanamke na hela unapata, Huo ni ubinafsi, Mkiulizwa kwanini mnataka haki sawa mnajibu ili muwe financial independent mkishakuwa financial independent mkiambiwa haya saidia familia yako unasema sio jukumu lako bali ni la mwanaume, sasa nini maana ya wewe kuwa independent kama uhuru wako haumsaidii mtu yeyote,,
Huo ni ubinafsi hakuna Excuse hapo na ndo maana wazee wetu hawakuwapa fursa wanawake kwasababu waliona mbali walijua Mwanamke akifanikiwa huwa anajiwaza yeye tu (Ubinafsi) mwanaume akifanikiwa anaiangalia familia yake
Huwa kuna sababu hupelekea watu kuwa hivyoKama kwenye ndoa hamuwezi kuweka mipango sawa mkashirikiana basi hiyo ndoa haifikii popote.
Sasa kama huwezi kichangia chochote si bora uache kazi ijulikane moja.
Kwani hata sasa Wanaume na wanawake ni kina nani wanaowahi kufa😂 Wanaume wanakufa kutokana na majukumu stress, kutumika kwa muda mrefu na mwisho mwili kudhoofu tangu Dunia kuumbwa trend ya wanaowahi kufa ni Wanaume wanawake wanabakiHukuwahi kukaa na bibi zako wakusimulie maisha ya zamani? Hawakuwa na pakusemea waliumizwa walilia vifuani, na wababa watesa wake zao hawanaga maisha marefu sana , wengi wake zao walibakia na kuishi muda mrefu sana