Je, Mwanamke ana wajibu wa kuchangia kifedha ndani ya Ndoa?

Kama unajijua hutakiwi kula kwa jasho mbona usikae nyumbani ukalea watoto alafu mmeo akatafuta pesa za kujenga familia?
Si mnasema hamtaki mama wa nyumbani? Na mke akiomba kila kitu unaanza kulalamika, acha auze hata mandazi.
 
Maswala ya nani Kati ya mwanamke na mwanaume anapaswa kuchangia pesa katika familia hayana mpangilio maalumu, hayana kanuni na hayapaswi kabisa kuwekewa kanuni au Sheria kama mnavyotaka.

Binafsi huwa ninakerwa Sana na kauli inayosema "mke akiwa na milioni moja halafu mume ana laki tano familia ina laki tano kwa sababu mwanamke pesa zake anajua atazituamia vipi". Hii kauli ni ya kipuuzi mno, kwangu mimi pesa za mume ni za familia na pesa za mke pia ni za familia.

Nasema hivi kwa sababu siko tayari kuhudumia kiumbe ambacho hakina mchongo wowote zaidi ya kupiga domo. Hata ninyi mnaojaribu kujadiliana kujua nani anapaswa kuchangia acheni mara moja tabia hii, Kila mtu adili na mkewe/mumewe. Kama mtu hataki mke wake asichangie asipotoshe watu wengine humu.

Mke wangu atachangia Sana katika familia labda afiche pesa zake nisizione. Siko tayari kufanya mambo kwa presha ya jamii.

Eti "hamna hela ya mboga" halafu ana hela, NYAMBAFU!!
Al-mukheef Monetary doctor
 
Uhodari mwingi sana kwneye kuelezea hali ilivyokuwa hapo zamani. Ni kwa vile bibi na mama zetu walivumilia sana kunyanyaswa kiuchumi, kila kitu ngoja baba aje. Haufafahamu hili sababu walikuwa hawalalamiki wala kuonesha kwa watoto wao. Lakini walihakikisha binti zao hawapitii waliopitia wao, zaidi wanapofiwa au kutelekezwa na mwanamme, au kipindi mwanamme anafuja mali kwenye jambo lisilo na manufaa kwa familia/watoto. Wamama hawa walibebea 'resentment' juu ya baba zenu, matokeo yake ikawa watoto wanapokuwa wakubwa, masaada mkubwa zaidi anapewa mama au tuseme anakumbukwa zaidi (si tunajionea wenyewe kwenye jamii zetu?) japo baba yupo hai na ndio aliyevuja jasho na damu kuwalea.

Pesa anayopata unaitolea macho ya nini? Kuhudumia familia kifedha narudia ni jukumu la mwanamme. Ukosefu wa wababa wengi wanaoelewa majukumu yao limekuwa jambo la kawaida kwenye jamii ya sasa. matokeo yake tunapata vijana ambao hawaoni umuhimu wa kuhudumia familia zao sababu hawana mfano unaoeleweka wa kiume. Wanaona mama zao walipambana na hivyo wake zao wapambane, hapana kubwa sana
 
Mimi mwanamke wangu ata simama Kama mlezi wa familia, ka ni biashara ata simamia za familia pia.
Kusimamia familia na biashara ni mchango mkubwa, lakini bado naamini kuwa kuchangia kifedha ni jambo la hiari kwa mwanamke, si jukumu lake la lazima. Ikiwa ataamua kusaidia, ni vizuri, lakini haipaswi kuwa sharti la ndoa.
 
Inaonekana una support wanawake golkipa, ila kwa maisha ya sasa ni wanaume wangapi Tanzania wana kipato cha kuweza ku-afford mwanamke golkipa, Yani baba, mama, watoto 3, wa-survive na kufanya maendeleo kwa kutumia single income ya baba Muhimbu
 
Inaeleweka kuwa kila mtu ana mtazamo wake kuhusu suala hili. Muhimu ni makubaliano kati ya wanandoa. Kama unadhani mke wako atachangia sana, hilo ni sawa kwa ndoa yako. Lakini kuna wengine wanaoamini mwanamke asichangie au achangie kwa hiari, na hilo pia linaheshimika.
 
Wabinafsi saana hawa viumbe hata Kwa vichenji vinavyobaki kwenye mahemezi utaskia usiiguse pesa yangu,
Kama kuna tatizo la uwazi wa kifedha kwenye ndoa, linapaswa kushughulikiwa kwa mazungumzo, si kwa ku-generalize kuwa wanawake wote ni wabinafsi.
 
Na pia, yaya yupo kumsaidia huyo mama na kazi za nyumbani. Hata zamani mama/bibi zetu walisaidiwa na ndugu zao wa kike au wifi zao hapo nyumbani kwa vitu vidogo vidogo siku hizi umbali unafanya watu wawe na wadada wa kazi. Hamna ubaya wa kupata msaada unapohitajika. Kipaumbele ni kuhudumia mumeo bila uchovu wa siku nzima kukuelemea.

Isitoshe dada wa kazi sio replacement ya kazi ya kuwa mzazi. Hajaingia leba, nyonyesha watoto wako wala kuwaapa uangalizi makini kama wa mama. Kufua na kudeki isilinganishwe na kulea kwa maana ya kulea
 
mwanamke kama anaamka asubuhi na Kwenda Kibaruani either kajiajiali au Kaajiliwa ni Muhimu sana Kuchangia maendeleo ya Familia kama Anataka Kutunzwa kwa kila Kitu basi akae tu ndani alee watoto na Mumewe apambane
 
Kila familia ina mfumo wake. Kama ilivyo kwa babu na bibi zako, walishirikiana kulingana na mazingira yao. Lakini si lazima kila ndoa ifuate mfumo huo. Kila wanandoa wanaamua kinachofanya kazi kwao.
 
Kama unajiona sio jukumu lako kuhudumia familia kaa nyumbani ulee watoto uhudumiwe kila kitu.
Ukijitia kwenda kutafuta hela hizo hela zitakuwa chini ya familia.
 
Si mnasema hamtaki mama wa nyumbani? Na mke akiomba kila kitu unaanza kulalamika, acha auze hata mandazi.
Hatutaki goli kipa ili na mwana mke achangie kwenye maendeleo ya familia na sio kwenda kutafuta hela ili aende kufanya mambo yake ya kibinafisi.
 
Kusimamia familia na biashara ni mchango mkubwa, lakini bado naamini kuwa kuchangia kifedha ni jambo la hiari kwa mwanamke, si jukumu lake la lazima. Ikiwa ataamua kusaidia, ni vizuri, lakini haipaswi kuwa sharti la ndoa.
Hizo pesa zisizo hudumia familia zinaenda wapi na zinafanya kazi gani?
 
Ikiwa mwanamke ana jukumu la kuchangia kifedha kwa lazima, basi tunapaswa pia kuzungumzia usawa katika majukumu mengine ya familia. Je, mume naye anapaswa kushiriki kwa usawa kwenye kazi za nyumbani na malezi ya watoto?
 
Kama unajiona sio jukumu lako kuhudumia familia kaa nyumbani ulee watoto uhudumiwe kila kitu.
Ukijitia kwenda kutafuta hela hizo hela zitakuwa chini ya familia.
Tuliza jazba ndugu mdau, pingana kwa hoja. Hayo maneno ya kumuambia mkeo muelewane hivyo. Sio kila kiatu ni saizi yako
 
Yeah, ndoto maana sitaki watu wapotoshane, wanandoa wataamua wenyewe bila kusukumwa na kitu chochote. Kumbuka nyinyi kama wanandoa mkikwama hakuna atakaye kuja kuwasaidia.

Mke wangu atachangia Sana!!!
 
Swali linabaki—je, mwanamke akichangia, inamaanisha mume naye anaweza kutarajia kusaidiwa kwenye majukumu mengine ya nyumbani kama kulea watoto na kazi za ndani?
Mtu unaamka saa 12:00 unarudi saa 3 za usiku hayo malezi ya watoto na hizo kazi za ndani unazifanya saa ngapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…