Strong and Fearless
JF-Expert Member
- Apr 24, 2017
- 895
- 2,218
- Thread starter
-
- #121
Inategemea na maelewano ya wanandoa. Kama mke hawezi kuchangia kifedha, lakini anajitolea kwa familia kwa njia nyingine, hiyo ni sawa. Muhimu ni kuwa na ushirikiano na kuelewana, siyo lazima kila mmoja kuchangia kifedha.mwanamke kama anaamka asubuhi na Kwenda Kibaruani either kajiajiali au Kaajiliwa ni Muhimu sana Kuchangia maendeleo ya Familia kama Anataka Kutunzwa kwa kila Kitu basi akae tu ndani alee watoto na Mumewe apambane
Mtu anayeishi na mwanamke kama huyo ndo mjinga kwa sababu yeye ndo karuhusu hivyo.Kweli.
Na vp kama Mwanamke ana kipato na hataki kurudi hata na nyanya, vitunguu, chumvi (viungo). Yupo sahihi?
Kuna jaziba gani kwenye maneno yangu?Tuliza jazba ndugu mdau, pingana kwa hoja. Hayo maneno ya kumuambia mkeo muelewane hivyo. Sio kila kiatu ni saizi yako
Wanaume kamwe tusiruhusu kuwa na wanawake ambao hawana mchongo wowote.1. Anaamka saa 11 asubuhi anaacha watoto anaenda kutafuta pesa.
2. Anarudi home saa mbili usiku, watoto wanalalq hawajamuona mama yao.
3. Malezi amemuachia dada/msaidizi wa nyumbani.
Mtu wa namna hii anachangia kipato chake atake asitake, akiona hawezi akae nyumbani kulea watoto.
Mwanamke mpumbavu tu ndio ataona sio sawa kuhudumia watoto wa tumbo lake, huku anaelekeza kipato chake kwa watoto wa ndugu zake.
Wengi wanapenda kutumia 50/50 ila likija swala la kipato utasikia wanasema mume anawajibika 100% na hela yake ni kwa ajili yake na upande wa kwao.
Hizo kazi na malezi utayafanya saa ngapi hali yakuwa siku nzima kiguna njia eti unatafuta hela?Ikiwa mwanamke ana jukumu la kuchangia kifedha kwa lazima, basi tunapaswa pia kuzungumzia usawa katika majukumu mengine ya familia. Je, mume naye anapaswa kushiriki kwa usawa kwenye kazi za nyumbani na malezi ya watoto?
Maneno gani ya jazba hapo?Tuliza jazba ndugu mdau, pingana kwa hoja. Hayo maneno ya kumuambia mkeo muelewane hivyo. Sio kila kiatu ni saizi yako
Haipo katika haiba ya kike kuacha kaibsa kabsia hata kupitia kitu kidogo, au mtoto anapoomba hela ya kitu kidogo mpaka baba arudi. Anayo, anatoa au anafanya kwa roho nyeupe sababu uwezo anao piaKweli.
Na vp kama Mwanamke ana kipato na hataki kurudi hata na nyanya, vitunguu, chumvi (viungo). Yupo sahihi?
Kwa kizazi hiki hiyo haipo mkuu, atachangia pato la familia na maendeleo. Siku ikitokea bahati mbaya tukashindwana mbona mgao wa mahakama unaenda 50/50, na huenda kuna wakati wanachukua 60/40. Nijitoe mhanga then mwisho wake afaidi yeye, hiyo hapana.Wanaume kamwe tusiruhusu kuwa na wanawake ambao hawana mchongo wowote.
Kitu kinachonikera ni mwanamke kuwa na hela halafu hataki itumike katika maswala yahusuyo familia.Hizo kazi na malezi utayafanya saa ngapi hali yakuwa siku nzima kiguna njia eti unatafuta hela?
Mchango wa mwanamke haukamiliki kwa pesa pekee. Kuna majukumu mengine muhimu, kama kulea watoto, kumtunza mume, na kuleta usawa na amani katika familia. Ingawa mke anafanya kazi, mchango wake katika familia haupimwi tu kwa pesa. Hata na dada wa kazi, bado kuna kazi za kipekee ambazo mwanamke anazifanyaSasa mtoke wote asubuhi muende kazini na mrudi wote jioni huku kazi za nyumbani pamoja na kuangalia watoto zinafanywa na dada wa kazi. Wewe mwanamke unakua na mchango gani kwenye iyo ndoa? Kipato chako unapeleka wapi?
Mkuu Kitu ambacho sikubaliani nacho ni kuona mwanamke kuwa na pesa halafu hataki katika matumizi ya kifamilia, yaani unakuta mwanamke hataki hata kununua mboga kwa hela yake.Kwa kizazi hiki hiyo haipo mkuu, atachangia pato la familia na maendeleo. Siku ikitokea bahati mbaya tukashindwana mbona mgao wa mahakama unaenda 50/50, na huenda kuna wakati wanachukua 60/40. Nijitoe mhanga then mwisho wake afaidi yeye, hiyo hapana.
Hata hivyo, uchumi umekuwa mgumu sana, kipato cha mume pekee hakitoshi kusomesha, kujenga, kulisha na kuvisha watoto...ni wanaume wachache sana wanaweza kumudu kwa 100%
Siyo wajibu wake kivipi.Sio wajibu wake ila ni kwa hiari. Lakini inapendeza akifanya hivyo kama anao huo uwezo.
Kazi kama zipi ebu tutajie.Mchango wa mwanamke haukamiliki kwa pesa pekee. Kuna majukumu mengine muhimu, kama kulea watoto, kumtunza mume, na kuleta usawa na amani katika familia. Ingawa mke anafanya kazi, mchango wake katika familia haupimwi tu kwa pesa. Hata na dada wa kazi, bado kuna kazi za kipekee ambazo mwanamke anazifanya
Sidhani kama pesa za mke zinapaswa kuwa tu kwa ajili ya matumizi ya kifamilia. Kuna nafasi ya ushirikiano, na maelewano mapema ni muhimu. Ni muhimu kujua kwamba kila mtu katika ndoa ana majukumu yake, na si lazima michango yote iwe ya kifedha. Ikiwa mmoja ni mama wa nyumbani, bado ana mchango mkubwa katika familia.Kama ni mama wa nyumbani jukumu lote la ustawi wa kiuchumi ni la mwanaume kama una kipato unawajibika kuchangia kulingana na scale ya kipato(sio hiyari, unawajibika).
Ila yote kwa yote ni vyema mkajadiliana ilo suala kabla ya kuishi pamoja. Kama unafikiri mwanamke hauwajibiki kwa bill za nyumbani mwambie mwenzako mapema kabla hamjafunga ndoa au kuanza kuishi pamoja.
Kipindi cha uhumba au mahusiano ya boyfriend and girlfriend mwanaume anaweza akamaliza tu bill za hapa na pale bila kuulizia hela yako lakini mkifunga ndoa katika hali ya kawaida anajua na wewe pia unatakiwa kuchangia kwenye masuala ya kifamilia.
Kwaiyo kama unafikiri pesa yako sio kwa ajiri ya matumizi ya kifamilia au unafikiri kuchangia bill za nyumbani kwako ni hiyari na sio wajibu, mwambie mwenzako msimamo wako mapema kabla ya kuanza kuishi pamoja.
Ya kwamba kuhudumia watoto wako ulio wazaa sio wajubu wako ?Sio wajibu wake ila ni kwa hiari. Lakini inapendeza akifanya hivyo kama anao huo uwezo.
50/50 ni kuhusu ushirikiano na msaada. Huwezi kupima mchango wa ndoa kwa kiwango cha kifedha tu. Usawa wa ndoa unahusisha kujitolea, kuelewana na kusaidiana kwa njia nyingi, na siyo tu kwa michango ya pesa.Mnang'ang'ania 50/50... Ila linapokuja suala la uchumi, mnajitoa. Sasa hiyo 50 kwa 50 inakuwa na maana gani?
Basi hakuna mlinganyo, kila familia itategemea background yake.Kila familia ina mfumo wake. Kama ilivyo kwa babu na bibi zako, walishirikiana kulingana na mazingira yao. Lakini si lazima kila ndoa ifuate mfumo huo. Kila wanandoa wanaamua kinachofanya kazi kwao.