Je, Ndoto Zinazoonyesha Mambo Yajayo Ni Kazi ya Ubongo au Ulimwengu wa Roho?

Sawa mkuu ila kuna watu wana maono ,kuna watu wamebarikiwa kuona mambo ya mbele....zamani tulikuwa tunawaita manabii ,walikuwa wanatokewa live na kuambiwa ila kwasasa wanatokewa kupitia ndoto.

Sasa mtu aongope ili iweje kuhusu kuota ndoto ya ndugu yake kufa au kupata ajali? Mbona ajali au vifo vimetokea kwenye hiyo familia lakini hakusema hii nilioteshwa?


Mambo ya kiroho yanahitaji imani ,kama hauna imani hauwezi kuamini mpaka ushuhudie wewe na wewe uliyoshuhudia ukija kutuadithie siye hatutakuamini pia tutaona uongo.
 
Kujenga hoja na mtu ambae hana imani hizo za kiroho mtakesha maana wewe na yeye ni mbingu na ardhi
 
Mkuu,nashangaa unashiriki mada ambayo huwezi kuthibitisha kama ipo kwa wengine maana kila kitu unahitaji uthibitisho. Wewe una uhakika gani kama watu wanaota? Wanavyoota huwa upo nao ndotoni? Mada kama hizi usije mkuu. Halafu kuhusu uwepo wa Mungu, mkuu mimi nimeona uwepo wa Mungu na nina uhakika kwa asilimia 100 YUPO, bila mashaka, mimi binafsi nimeshuhudia uwepo wa Mungu, hayo maneno kwamba" mmeshindwa kuthibitisha yupo" nitoe, mimi nimethibitisha bila kutoa shaka, ongelea wengine, sio mimi.
 
Mkuu,nashangaa unashiriki mada ambayo huwezi kuthibitisha kama ipo kwa wengine maana kila kitu unahitaji uthibitisho. Wewe una uhakika gani kama watu wanaota?
Mimi ni binadamu pia kama wengine.

Kama wao wanaota na mimi naota pia.

Kuota kila mtu anaota.
Wanavyoota huwa upo nao ndotoni?
Kuota kupo.

ila wewe kusimulia ndoto aliyoota mwingine kama vile ulikuwepo naye ndotoni kunatia mashaka.

Maana huwezi kuthibitisha kwamba kweli ndoto hiyo iliotwa na huyo mtu anayekusimulia au mtu huyo anakudanganya tu.

Ni kama wale manabii kanisani, wanawaambia waumini wao, Nilioteshwa na Mungu.

Kumbe ni danganya toto za kushika maboya.
Mada kama hizi usije mkuu.
Hapa ni public forum.

Mtu yeyote anaweza kuja kuchangia chochote.
Halafu kuhusu uwepo wa Mungu, mkuu mimi nimeona uwepo wa Mungu na nina uhakika kwa asilimia 100 YUPO,
Yupo wapi?
bila mashaka, mimi binafsi nimeshuhudia uwepo wa Mungu, hayo maneno kwamba" mmeshindwa kuthibitisha yupo" nitoe, mimi nimethibitisha bila kutoa shaka, ongelea wengine, sio mimi.
Umemshuhudia huyo Mungu wapi?

Lini?
 
Mkuu, kama kuota kupo kwanini watu wanaposimulia ndoto ambazo kwa akili zetu tunashindwa kuelewa unaomba uthibitisho? Lakini zinaposimuliwa ndoto nyingine hauombi? Yaani unachagua kipi ch kuhoji ( ambacho upo comfortable kukielezea) ambacho unashindwa kutolea maelezo unahoji kama hiyo ndoto ni ya ukweli? That's double standard. Kama unaamini watu wanaota ilihali wewe huwa haupo nao ndotoni basi wanapokusimulia ndoto ambazo hauzielewi usihoji, tafuta reason behind.
Halafu kuhusu uwepo wa Mungu, mimi nimeshuhudia maishani mwangu,ila haukuwepo kwahiyo Sina namna ya kuweza kuthibitishia maana hakuna namna wewe utajua kama ni uongo au ni ukweli. Sitajichosha kufanya hivyo maana hata nikikesha bado hakuna namna utaniamini. Nimefunga ,sitareply tena kwenye comments zako.
 
Kama hapa nimesoma huu uzi.

Nimeota nipo katika msiba wa rafiki yangu mmoja daktari, napanga maua, nachota maji nje na kuingiza ndani, nakaribisha watu, naufikiria wasifu wake na mambo tuliyofanya pamoja.

Sasa hiyo ni ndoto tu.

Most likely jamaa ataendelea kuwapo tu. Ikiwa hivyo hatusemi kuwa ndoto hazitabiri matokeo yajayo.

Na ikitokea akafariki hapa karibuni, inaweza kuwa coincidence tu, ambayo hata kama ina nafasi ndogo sana ya kutokea, inaweza kutokea.

Ikitokea kweli, kwa coincidence tu, kwa imani zetu, natakiwa kuamini ndoto zinatabiri yajayo.
 
Shukran kaka 🙏🙏
 
Ni matokeo ya ulimwengu wa Roho anakuwa amejaliwa na Mungu karama hiyo.Sisi kwetu tuna hii karama hususan Mama.Mfano naweza kuwa katika shida nikamwambia aniombee huku na mimi nikisali pia.Baada ya muda huniambia nimeota jambo hili limekuwa hivi na inakuwa kama alivyosema.Mfano kuna kipindi nilikuwa naombea kazi kwa kusali na kufunga nikawa sioni dalili nikamuomba Mungu anisaidie nijue hii kazi itatokea wapi .Baada ya siku kadhaa mama aliniambia nimeota umepata kazi na boss wako ni mtu kutoka kanda Fulani kweli nilipata kazi na bosi nilimkuta yuko kama mama alivyosema.Siku moja aliniambia nimeota ndugu yako amerudi nikawa nagombana nae kwa nini karudi wakati shule bado hazijafungwa.Kesho yake nipo ndani nasikia watu wanazozana kutoka kweli ndugu yangu amerudi na mama alikuwa anamgombeza(Kuna makosa alifanya shule akapewa suspension alikuw anasoma boarding).
 
Ooh aisee inastajabisha hongereni
 
Watu hutofautiana experience zao kwenye maisha na ndio maana hata symbols tunazoziona kwenye ndoto huwa tunatofautiana tafsiri zake kati ya mtu na mtu. Na ndio maana watu wawili wanaweza kuota ndoto sawa sawa ila tafsiri zikawa tofauti kwa kila mtu.

Sasa ndoto za matukio yajayo wapo ambao wakiona symbol fulani basi wanajua ni tukio gani litatokea kama tafsiri ya hiyo ndoto japo hiyo symbol haiendani na hilo tukio, wapo ambao wanaota jambo katika ndoto ambalo huja kufanana na tukio lijalo na wapo ambao wanaota ndoto ila wanashindwa kujua kama inahusu tukio lijalo hadi linapotokea hilo tukio ndipo anakuja kuona uhusiano wa ndoto na hilo tukio.
 
Mkuu tunawezaje kutofautisha tafsiri sahihi na retrospective interpretation?
 
dhamira huu keep record ( ndicho ambacho watu hukisoma ) ndani ya dhamira kuna taarifa zote za mtu ( mwenye uwezo wa kupenya hapo anasoma vizuri kabisa maisha ya mtu na hata mawazo ya mtu hata ) lakini hii pata inampa kujua mambo yaliyopo na yaliyopita na sio mambo yajayo.

Ndoto zimegawanyika na zina makundi yake mengi, kwa ufupi kuna kuota na kuna kuona na vyote hivyo vina chanzo mbali mbali na chanzo ndio kinaamua iwe kweli au uwongo, lakini mwisho wa siku ndoto zote ni kweli ila sasa kuna ukweli wa ukweli na ukweli wa uwongo
 
Shukran
huu muandiko na mambo unayo andika selfika hufanani

karibu tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…