Venus Star nadhani umesoma au unasoma China, ndio maana unawafagilia zaidi ya uhalisia. Thread umeweka kama swali, lakini ndani umejaza mambo yako yote. China imeendelea sana, hilo halina ubishi. Kwenye teknolojia China soon atakuwa giant, ila hadi sasa si kiongozi. Mimi natoa maoni kama layperson.
Kwa wafanyabiashara, kama unataka mashine ya uzalisha fulani, ukitafuta nzuri China basi itakuwa na components ambazo ziko outsourced nje ya China au kampuni ya nje iliyopo China. Ukitaka mashine ya uhakika, basi utapata nje ya China, shida huwa bei kuwa juu ukilinganisha na China.
Katika ulimwengu teknolojia nyingi ziko wazi (vilishawahi kuwa discovered na watu) ila shida ni kufanya kifanye matumizi unayotaka kwa ufanisi zaidi (invention).
Hadi sasa China yupo vizuri kwenye mass production either ikawa ni kwa high quality items ambazo ni nadra kuwa superior kwa wapinzani wenzake globally au ni zile low-quality products.
Pia China ananufaika sana na contract manufacturing, kwa sababu ya gharama ndogo za nishati, mishahara na kodi. Kuna kiwanda fulani cha matairi kilichopo Taiwan, bei za Tairi kiwanda kikuu ni ndogo, ila ukiwaambia wachukua kiwanda chao cha China rate kwa kila tairi inapungua zaidi ya dolla 15 na kwa ubora uleule.
China ananufaika sana na soko lake kubwa la ndani ambalo lina sheria ngumu katika kulilisha products zitengenezwazo nje.
Tuna matukio mengi ya serikali ya China kutuma vijana wake sehemu nyeti mataifa ya magharibi kama kwenye taasisi za elimu, utafiti, kijeshi n.k ili kunufaika kwa vyovyote vile kwa kuchukua teknolojia ya wenzao. Hii inaonesha China ina struggle bado sehemu nyingi za teknolojia.
Ila uvumbuzi na ubunifu wa vitu huwa nadra sana kufanywa na mtu wa taifa moja. Mtengano wa China na mataifa mengine ya Ulaya unalifanya China isikue haraka katika teknolojia. Adui zake wengi ni giants kwenye teknolojia, hivyo ku share taarifa inakuwa ngumu. Ingewatymia muda mfupi China kukua kana wasingekuwa na strained relationship na US, Japan, Taiwan, Germany, UK, Australia, n.k
Sidhani kama matokeo ya China kuwa banned na Trump kwenye vitu vingi yataonekana ndani ya muda mfupi. Labda miaka 10 ijayo. Huawei pamoja na oS yao bado haifanyi vizuri nje ya China. Unahitaji vichwa vingi kufanikisha hayo mambo. Pia China iendelee kuajiri vichwa vya watu makini vilivyotapakaa globally kama US ilivyokuwa ikifanya kwa muda mrefu.
Ila naamini ndani ya miaka 20 ijayo, China atakuwa giant kwenye teknolojia, na yamkini goods zake zitaanza kuwa ghali pia.