Je, Polisi washitakiwe kusababisha vifo kizembe vya random shootout? RIP Aqulina Akwilini, Baftaha, She is an Angel!

Je, Polisi washitakiwe kusababisha vifo kizembe vya random shootout? RIP Aqulina Akwilini, Baftaha, She is an Angel!

Hivi kulikuwa na ulazima wa kufanya maandamano hayo?yalifanyika muda gani?wakati wa saa za kazi au baada ya ofisi kufungwa?kwa nini wanasiasa hawaleti watoto wao kwenye maandamano?nionavyomimi wote wanapaswa kulaumiwa!
Ilibidi ujiulize kwanza swali kuwa ni haki kutumia silaha za moto ilihali kuna maandamano ya amani? kisha uulize hayo maswali yako
 
Wanatumiwa n.a. mapepo binadamu wa kawaida huwezi fanya unyama huu labda uwe mchawi
Bomu za machozi hazikufaa Rubber bullet hazikufaa mawashawasha mlionunua 2015 yayakufaa.naona mnafaidika n.a. hivi vifo
Muumiani nyie n.a. mlaaniwe
 
Hivi kwa akili yako kwenye vurugu kama hilo kuna dala dala litapita?
Kwa hiyo dala dala walijua chadema wataandamana na kwa hiyo hawakupita huko?Acheni uhuni mnaumiza sana hisia za watu.Fikiria huyu binti angekuwa anatoka katika familia yako..je hata kama alikuwa kwenye maandamano,alistahili hukumu hii?
 
Wanabodi,
Kwanza nitoe pole kwa kifo hiki cha malaika huyu
454a637916def479540d0fc946e0cc85.jpg


Jee mnajua Jeshi la Polisi Linaweza kushitakiwa kwa kifo hiki cha uzembe na wahusika kuhukumiwa kama kifo cha Mwangosi, lakini pia serikali ikashitakiwa kwa kesi ya madai na kuhukumiwa kulipa fidia kwa familia ya marehemu?.

Kuna mazingira ambayo polisi wanaweza kumuua raia wa kawaida katika polisi shootout na polisi wasiwe na criminal liability kama tukio hilo linahusisha matumizi halali ya risasi za moto kwa mujibu wa miongozo yao, lakini tukio lile ni kuthibiti riots, hivyo tangu lini jeshi la polisi linatumia risasi za moto kuthibiti riots za watu wasio na silaha zozote badala ya kutumia rubber bullets?!.

Tena kuna ushahidi wa kutosha na usiotia shaka, mara nyingi uvunjifu wa amani unasababishwa na polisi wanaodhibiti maandamano hayo!. Kama polisi wangesimamia na kuwapa ulinzi Chadema katika kufuata viapo vyao ili wakiona vurugu ndipo waungilie, what did they stand to loose?. Kilichotokea ni uzembe tuu wa polisi wetu na hakuna excuse yoyote itakayo weza kutolewa ku justify uzembe huu wa jeshi letu la polisi kupoteza maisha ya an innocent civilian just like that!.

Poleni sana, wazazi, wanafunzi wenzake, ndugu, jamaa, marafiki, wana Kinondoni wote na wote walioguswa na kifo hiki.

Hii ndio gharama ya demokrasia ambayo Watanzania wanalazimishwa kuilipa ili tuu fulani ashinde!.
Mungu yupo na haya anayaona!.

Rip, mwanafunzi wa Mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM),Aqulina Akwilini Baftaha
Kwa roho mbaya ya Mwigulu wakati akiwa mbunge tu sio waziri jinsi chadema walivyokuwa wanapata misukosuko hadi kufikia kusema ana ushahidi wakutoa hata mbinguni kuwa Lwakatare gaidi, na akawa anatembea na kijana mmoja amemwagiwa tindikali usoni, ,Leo yeye ndio waziri,, na hapo Dar Huyo Makonda alivyo na roho mbaya ukijumlisha na tukio la jana,

Kwa kifupi ilipofikia nchi yetu kuna haja ICC waje wafanye uchunguzi juu ya haya matukio .... kuna siku police watawamiminia risasi hata kundi la watu kumi kwa pamoja,, hii awamu kuna mtu anafurahi sana damu za watanzania zikimwagika,, rest in peace binti yetu//
Halafu utasikia sasa leo jioni watakavyokuja na Maneno mepesi na ya kipuuzi juu ya kifo cha huyo mwanafunzi asiye na hatia, Kikwete katuletea balaa sana, bora angemuacha Lowasa awe Rais tu au MEMBE, inafikia wakati ni bora kuongozwa na mtu mwenye kashfa kuliko anaefurahia damu zenu zimwagike
 
NO WAY ASKARI HAWANA MAKOSA NI LAZIMA WAHAKIKISHE AMANI NA UTULIVU VINAPATIKANA!
Tusijiingize katika anga zao jamani!
Rip Aqulina!
Ingekuwa ni Mdogo wako ungeandika hivyo,inasemekana marehemu alikuwa abiria ndani ya daladala,je kosa lake ni kuwa ndani ya daladala,au hakupaswa asafiri,au ulifikiri na yeye alikuwa anandamana?.Hata kama unatetea chama chako unapaswa ujue all in all uzembe aukustahili kuwa chanzo cha kukatisha ndoto zake,hata kama angekuwa ni mwanachama wa chama cha upinzani,sina chama lakini kuna mambo yanatokea unajiuliza maswali mengi ya yasiyo na majibu
 
Tumetofautiana baada ya kusema Mtulia ni chanzo......all in all Matumizi ya silaha za Moto hayakubaliki lkn nini unadhani kifanyike!?....Je Chadema wafanye wanavyotaka kufanya!?Je serikali iwape kila wanachotaka?!....
Serikali inafahamu njia sahihi na halali za kukabiliana na kuzuia uvunjwaji wa sheria na maandamano yasiyo halali. Wazitumie hizo njia. Matumizi ya risasi za moto yaepukwe. Hatutaki kuzika watu wasio na hatia kwa sababu chadema wanasumbua. Njia sahihi zitumike.
 
Sasa huyo binti kaingiaje katika anga zao?

I wish angekuwa dada yako ndipo ungeelewa vizuri.
Unalaana ya kufa wewe mse... wa head
Soma post za juu zezekuu!
Ignore list yangu inakuhusu maana wewe ni taira hatuwezi kuelewana hata
Ukinijibu sitasoma maana nimekuzika kwenye ignore list!
 
So sad to loose you my beloved great thinker. Ulikuwa great thinker kweli na umeridhihirisha hilo. Nenda dada yangu tangulia nasi twaja duniani tunapita tu . Ipo cku damu yako na sauti yako itainuka na kuviingia vizazi vya taifa hili kudai haki. Pumzika dada pumzika ila umetuacha na majonzi
 
Baada ya kuona picha hio nimepata hasira..
Hivi binadamu wa kawaida unapataje ujasiri wa kumuua binti kama huyo.
Huu unyama nadhani hata wakoloni hawakufanya..
Shenz sana polisi wa tz.
Hukumu yenu mtaikuta mbinguni
Halafu yakipata matatizo yakuuliwa na majambazi eti yanataka tuwaonee huruma,, pumbav
 
Polisi wengi ni watu waliofeli maisha, hawawezi kuwa na uelewa mpana zaidi ya kutumia silaha kiholela. Wajue siku wakianza kutafutwa wao hayo magwanda watayaona mazito.
 
Wewe kiazi mbatata kweli sasa ulitaka Chadema wabaki nyumbani kwao wakiwa hawana hizo fomu ili kesho wakasindikize wenzao,cha ajabu ni kuwa hujui hata kuwa ni kosa kwa polisi kutumia silaha za moto kwenye maandamano ya kawaida ilihali virungu vipo na mabomu ya machozi,acha unafiki.
Wht if waliopiga risasi daladala ni Hao waliokuwa kwenye kundi la waandamanaji?!!....Tunawajua na chama chenu siku hizi viongozi wenu wanatumia Umafia Kutengeneza sababu.....Haya sababu mmepata!Pigeni domo sasa
 
Back
Top Bottom