Je, Polisi washitakiwe kusababisha vifo kizembe vya random shootout? RIP Aqulina Akwilini, Baftaha, She is an Angel!

Ushauri wangu kwa uongozi wa UDSM na Familia ya Mwanafunzi aliyeuawa, utakuwa ni usaliti mkubwa kwa Marehemu kama uongozi wa UDSM utakubali Kupokea mwili wake na kuandaa utaratibu wa kumuaga bila maelezo yoyote kutoka kwa POLISI!

POLISI waeleze, hayo maandamano yalikuwa makubwa kiasi gani cha kufyatua risasi za moto!

Kulikuwa na tishio kubwa kiasi gani la uvunjifu wa amani hadi POLISI wakalazimika kutumia risasi za moto hovyo hovyo kiasi cha kuua abiria kwenye daladala!

Ifikie hatua tuache upuuzi wa kuacha wa kuendekeza haya majinga majinga kwa kigezo cha uzalendo! Nani anatakiwa kuwa mzalendo na nani hatakiwi kuwa mzalendo kwa mwenzake!?! Uzalendo ni nini!?!

Huu upuuzi ukiendelea, hatima yake sio nzuri kwa Taifa!

Kwa nchi za wanaojielewa, HIKI KIFO CHA HUYU BINTI ASIYEKUWA NA HATIA YOYOTE KINGEKUWA MWANZO WA KUPATA HAKI NA POLISI KUHESHIMU HAKI YA RAIA KUISHI! FAMILIA, UONGOZI WA CHUO NA WANAFUNZI WA VYUO VYOTE TANZANIA WAKIONGOZWA NA HAWA WA UDSM HAWATAKIWI KULIACHA HILI JAMBO KIHOLELA NAMNA HII!! DUNIA NZIMA, JUMUIA YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU MICHANGO YAO INAJULIKANA KWENYE JAMII! ACHENI KUKARIRI MAANDISHI TU, KUWA MSOMI NI PAMOJA NA KUKEMEA MAOVU KWENYE JAMII
 
utasikia tz kisiwa cha amani huku matukio ya watu kuuwawa na kupigwa risasi , kutekwa yanatokea kila siku.
 
Kweli kabisa Mkuu,, hawa ni wakuwatenga kabisa,, me kwenye Banda langu nimepangisha JW tu,, huwa polisi siwataki nawaambiaga kabisa madalali
 
shughuli za mcha mungu hizo yule mzee kama Tahira kwa kweli he is very greedy..sijui anatupeleka wapi jaman
 
Kila cku ccm inajinasibu kuwa inakubalika kwa wananchi tena kuwa ina wanachama wengi kuliko vyama vyote sasa kwanini msijiamini mfanye chaguzi za huru na haki na kila mmoja ajitangaze kwa wananchi ili tuone kama kukubalika kwenu huko
 
Habari za asubuhi wadau.

Sio mara ya kwanza kusikia ama kuwa muhanga wa unyanyasaji na mauaji ya polisi nchini kwetu.

Binafsi nina ushauri tu, taasisi zote za kijamii (mashule, makanisa, misikiti, mashule, vyuoni nk) ziwatenge waajiliwa wote katika idara ya usalama (polisi, mgambo) ila si wanajeshi (hawa muda wao haujafika).

Haiwezekani mtu na akili zake timamu kumnyanyasa mwananchi asiye na hatia ama kuvunja haki zake za msingi! Iwe kwa vyovyote vile hata kama ni maagizo kutoka kwa mkuu! Kwani wao hawana akili na ufahamu kuhusu UTU, hata kama hawana ufahamu huo kwani taratibu zao zinaelekeza kunyanyasa na kuvunja sheria/haki za wananchi?

Je, katiba yetu imekataza kuandamana? Je, ni lini katiba imezuia kampeni?

Polisi ndio husimamia sheria zisivunjwe, je taasisi hii inawajibika kwa nani? Je, mahakama zetu zinaweza kuleta suluhu?

Binafsi siamini katika uwajibishwaji wa polisi, hivyo maoni yangu JAMII iwaajibishe kupitia taasisi zake.

Asanteni, haya ni mawazo yangu upo sahihi pia kutokubaliana nayo.
 
Siku mama yako akipigwa risasi ya kwenye mitako yake Ile uje pia uandike ivyo
mnashangaza sana....hivi tatizo ni binti kupigwa risasi au nyie kuzuiliwa kufanya vurugu zenu mitaani?..Hamkujua hayo maandamano haramu hayakuwa na Mwisho mzuri!?Mmepigwa mnaanza kulia lia hapa kama vifaranga vilivyokosa mama....Tena endeleeni kabisa na hayo mafujo yenu mpaka nusu yenu Mmpate vilema vya maisha ndiyo mtajifunza
 
Sura zao zimeonekana kwenye video...
Best revenge lazima ifanyike ili wasirudie kutumwa
Kilichotokea leo ipo siku watu wataandama kiukweli ukweli
 
Wewe nakujua si kaka poa wapale Ohio?
Naona jana wewe na ukoo wako hamkupata tenda mkageuzana wenyewe kwa wenyewe!
Pathetic ignore list yangu inakuhusu wewe hanithi wa nchi kavu!!!!
Malaya wa kiume
Eti hizi ndiyo points za wafuasi wa serikali (CCM) ??!! Mbona AIBU ?
 
Kuna wakati kukaa kimya huwa ni hekima. Lakini kukaa kimya huku mkiangalia kichaa akiwa ameshika panga, anawafyeka mmoja baada ya mwingine ni upumb.avu.

Wameua watu, miili wanatupa kwenye mito na kwenye fukwe za bahari, tupo kimya. Eti tunasema Mungu anajua.

Mungu anachojua ni kuwa ametupatia akili na nguvu za kupambana na vichaa. Yeye alifanya kazi kutuonesha kuwa mafanikio ni kwa kufanya kazi.

Wametaka kumwua TL, tupo kimya. Wameteka watu, tupo kimya. Wanakamata watu na kuwaweka korokoroni kama watakavyo, tupo kimya.

Hakika hata huku mbele ya Mungu, sote tutahukumiwa sawa na wauaji na watesaji. Wakati wao watahukumiwa kwa mauaji na utesaji, sisi tutahukumiwa kwa kushindwa kutekeleza wajibu wetu wa kujilinda na kuwalinda wenzetu. Hakuna ahera wala mbingu ya mtu mwoga na mzembe.
 
Polisi wanajionaga kama Makufuli wakati wana njaa hatari, dawa yao ni kuwarecord tu pindi tukiwapa zile buku 10.
 
Paskal, kumetokea nini mpaka mtanzania huyu akawa katikati ya polisi na risasi zao za moto?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…