Je, Polisi washitakiwe kusababisha vifo kizembe vya random shootout? RIP Aqulina Akwilini, Baftaha, She is an Angel!

Someone is going to pay the price for these killings; damu za watu huwa hazimwagiki bure bali zina maagano. Kinga ya hirizi kiunoni haiwezi kuzuia mkono wa Mungu usikuadhibu. RIP beatful .
 
Mleta uzi leta habari toka vyanzo vya uhakika sio kutoa kwa akina mange,unajipunguzia heshima,umesema aliuwawa ni mwanachuo wa UDSM wakati ni wa kutoka NIT
Suala anasoma wapi halina mashiko sana.Kilichopo ni kuwa kauwawa kwa uzembe wa watu Fulani tena bila hatia
 
Serikali inayojifunia nguvu ya dola kushinda chaguzi si serikali bali ni kikundi Fulani tu cha watu wanaolinda maslahi yao ya madaraka kwa mabavu.
Damu hiyo iliyomwagika haitawaacha salama.
 
Akili zenu ndivyo zilivyo risasi imepigwa na polisi chadema ndio wawajibishwe hakika CCM ni kizazi cha laana.
 
huyo denti alikua anatafuta nin huko kwenye mikutano ya siasa wakati wenzie wako kwenye maandalizi ya mitihani?
Mdomo sharp kuliko kichwa. Tafuta taarifa kabla hujaropoka kwa kejeli kwa kuwa tu hayajakukuta wewe.

Uliambiwa na nani alikuwa ameandamana?
Maandamano ni kosa?
Kama ni kosa, hukumu yake ni kifo?
Waandamanaji wanakuwa ni watu wa aina gani: wasio na maandalizi ya mitihani au yeyote anayeguswa na kilichosababisha maandamano?
 
Hawa police washtakiwe ili kuwatia adabu mbona wanafanya kazi tofauti na kiapo chao
 
Hakuna dala dala litakalopita katika vurugu
Laana hiyo hakika albadiri inafanya kazi yake
 
NO WAY ASKARI HAWANA MAKOSA NI LAZIMA WAHAKIKISHE AMANI NA UTULIVU VINAPATIKANA!
Tusijiingize katika anga zao jamani!
Rip Aqulina!
Katika sheria zote,ama ziwe za kileberal(kidunia)au za kidini,ni kosa kubwa kudhulumu roho ya mtu,bila ya kuwa na sababu,sababu kama self defence,litataka pawepo na uthibitisho wa kutosha,utakaopelekea kuchukua hatua hiyo,ya kumshambulia mtu hadi kumpotezea maisha,laana hii inawaingiza katika makosa washiriki wote,kuanzia,wachangiaji,wapangaji na watekelezaji.

Mwenyenzi Mungu Muumba mbingu na ardhi,binaadamu,na viumbe wote,ni yeye aliemuba uhai,ameutengeneza uhai,katika ufundi usioelezeka,jukumu la kuuchukua uhai lipo kwake,lakini linakua na sababu,sababu Moja asiyoisamehe,ni kuidhulumu roho,Kwa yule asiyoweza kuimiliki,Alana ya kuidhulumu roho inakwenda mbali na baina msamaha.

Suala mtasema nini mkirudi Kwa muumba.

Watanzania wapo katika mtihani mkubwa katika wakati huu,kumekuwa na mauwaji na utekaji wa watu,unaofanywa na watu wasiojulikani,lakini la kusikitisha zaidi,hawa watu wasiojulikana wanaopotea ama kuuwawa ni kutoka vyama vya upinzani,ni kweli serikali haihusiki???,yupi wakulaumiwa na kujiuzulu.
 
Pascal hapa ukichunguza Polisi waliingizwa kwenye mtego na viongozi wa Chadema, viongozi hawa walijua kuwa wakiandamana watapambana na polisi. Sasa hivi wapinzani wanajaribu kwa kiasi kikubwa kuharibu sifa za serikali ya awamu ya tano International kwa kuifanya ionekane ni ya kidikiteta. Cha msingi vyombo vya usalama viwe very carefully katika kutekeleza kazi kwenye sehemu ya watu wengi, hekima na busara itumike. Kutumia nguvu kama ya jana haikuitajika.
 
Unajua kulikuwa na vibaka wangapi,unajua ni nani alikuwa anaandamana kwa dhati,unajua ni yupi alikuwa chadema na yupi hakuwa chadema......!? Haya mambo lazima uangalie kwa kubalance
kwahiyo kibaka apigwe risasi. CCM bana ni zao la shetani.
 
Duuh hii nchi tunakoelekea n kubaya kupigana risasi huku leo huyu kesho yule tutafika kwel
REST IN PEACE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…