Je, Polisi washitakiwe kusababisha vifo kizembe vya random shootout? RIP Aqulina Akwilini, Baftaha, She is an Angel!

Je, Polisi washitakiwe kusababisha vifo kizembe vya random shootout? RIP Aqulina Akwilini, Baftaha, She is an Angel!

Magufuli, polisi
Magufuli, mwendesha mashtaka
Magufuli, hakimu
Magufuli, magereza

sasa hivi ni jeshi la mtu mmoja. Kashtaki popote
 
Mimi naona kwa hili tu tusimhukumu Pascal.kwa kuwa nafikiri kuleta tu huu uzi na kusema kwa uwazi bila ya yeye kujificha,ametimiza wajibu wake, kwa kiasi kikubwa,nami nampongeza.

kwa kweli ni wajibu wa serikali kuchukua hatua sasa.
Pole kwa familia na watanzania wote wenye nia njema kwa matukio mabaya kama haya.

Ni wakati waandishi wa Habari kuamka kwa maana kalamu zao ni zaidi ya risasi na Camera zao ni zaidi ya kombora la nuklia.

Simlaumu nimemtahadharisha tu
 
Nimelia sana kwa kweli kwa tukio hili. Maana yake hakuna aliye salama tena Tanzania yetu. Kama mtu anapigwa risasi akiwa ndani/anashuka daladala,maana yake ni kuwa hakuna aliye salama. It pains a lot.
 
Inamaana bila kukusanya watu na kuandamana wasingepewa hizo hati?viongozi wenyewe hawatoshi?mbona watoto wao hawakuwepo kwenye maandamano?

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
Yaani mtu mzima unayemaliza nyembe kunyoa hayo matakataka unauliza swali la kipuuzi eti mbona watoto wao hawakuandamana ?muda mwingine usijionyeshe kama una akili pekee za kuvukia barabara.
 
Sasa hivi polis wapo juu ya Sheria wanafanya chochote kile kitachofanikisha kuhujum upinzani, sasa hivi wapinzan machoni mwa vyombo vya dola in km majambazi
 
RIP. It is so sad. matumizi ya nguvu yasiyo ya lazima ni lazima yapingwe kwa mguvu yote.
Under Recklessness na vicarious liability, inawezekana.
 
Ni kweli, lakini unataka tena kusikia “I wish i could be IGP”? Au unafumbia macho kiini cha tatizo kwasababu katokea kule?
 
Hata mauaji ya arusha si walikufa wasio na hatia?? Leo imekuwa haijawahi kutokea tena?
Haijawahi kutokea awamu kama hii watu wanapotea,mwandishi na saa nane,watu kupigwa risasi mchana kweupeeee kama lisu nk hakuna cha uchunguzu wala majibu.
 
Hawa ni wapinzani wa serikali ya CCM,ambao wakati ule walikuwa watiifu,wakiwa na mapenzi na imani na serikali na nchi yao,je wakikusanyika hivi,na wakadai haki za kibinaadamu zinazovunjwa zikome,itakuwaje ?????.
Mimi nadhani ni wakati wa millions march Dar umefika,kuomboleza mauaji ya watu wanaouawa kama ndege,thamani ya binaadamu,Haipo Tanzania.
Ukawa piga mbiu ya upatu,au mnasubiri mauaji mengine yaendelee???????.
 

Attachments

  • IMG_0878.JPG
    IMG_0878.JPG
    34.8 KB · Views: 47
  • IMG_0879.JPG
    IMG_0879.JPG
    69 KB · Views: 46
  • IMG_0880.JPG
    IMG_0880.JPG
    33.4 KB · Views: 39
  • IMG_0881.JPG
    IMG_0881.JPG
    44.4 KB · Views: 38
Sasa Mwigulu unaona raha gani kula mshahara kwa Damu hizi hasa ya binti kama huyu?


Anajaribu kumu impress maghufuli kwa kutoa order za unwagaji damu, Mwigulu muogopeni mungu hivi Vyeo vinavyowafanya mmwage damu za watu huku duniani hamtaenda navyo mbinguni wala hamtaingia navyo kaburini
 
Moderator umeunganisha uzi wangu na wa Mayara, wote tulikuwa tunaongelea jeshi la polisi lakini katika muktadha tofauti. Msiwe mnaunganisha mada bila kutathmini mara mbilimbili. Mimi nilikuwa naongelea jeshi ilivyopofomoka kitaasisi Mayalla anaongelea kitu kingine
 
NO WAY ASKARI HAWANA MAKOSA NI LAZIMA WAHAKIKISHE AMANI NA UTULIVU VINAPATIKANA!
Tusijiingize katika anga zao jamani!
Rip Aqulina!

Angekuwa dada yako ungeongea hivi....??? Usiombe yakutokee brother. Kwa hiyo Amani haipatikani mpaka waue raia wasio na hatia?? Hii ni serikali ya kidicteta ndugu. Malta nyingi madictator Hutumia nguvu nyingi kusov matatizo ndy maana kila uchao mili ya watu huokotwa sehemu mbalimbali hapa nchini. Tanzania sasa imekuwa nchi isio na amani na isiyotenda haki ingawage kunavyombo vya sheria lakini vyote havina meno. Udhaifu wa vyombo hivyo imefanya Tanzania ifike hapa. Inasikitisha sana. Mungu akulaze mahala pema peponi. Aliyekuua hato ishi milele bali na yeye atakufu tu. Namwomba mungu amwandalie Adhabu kali siku ya kifo chake na huyo aliyemtuma kama rais, IGP yyte yule aliyehusika na mauji haya afikwe na mwisho mbaya siku ya umauti wake.
 
huyo denti alikua anatafuta nin huko kwenye mikutano ya siasa wakati wenzie wako kwenye maandalizi ya mitihani?
Umesoma mada ukamaliza? Umeambiwa alikua kwenye daladala au hujui kusoma??

Hata kama alikua kwenye mkutano, ni kigezo cha kuuliwa!?
 
Pascal hapa ukichunguza Polisi waliingizwa kwenye mtego na viongozi wa Chadema, viongozi hawa walijua kuwa wakiandamana watapambana na polisi. Sasa hivi wapinzani wanajaribu kwa kiasi kikubwa kuharibu sifa za serikali ya awamu ya tano International kwa kuifanya ionekane ni ya kidikiteta. Cha msingi vyombo vya usalama viwe very carefully katika kutekeleza kazi kwenye sehemu ya watu wengi, hekima na busara itumike. Kutumia nguvu kama ya jana haikuitajika.

Umesoma bandiko hili?
Mbowe achunguzwe kwa vifo vya Daniel John na Aquilina
 
R.I.P
Poleni wafiwa

Chadema wanaenda kuwanunua kuwapa chenji ndogo wajaze sehemu wanapita..

Uchunguzi wa polisi ufanyike kwa kifo chake hii ni lazima
Na pia uchunguzi nani anawakusanya wajae kufanya fujo bila kufata sheria na huku wanajitayarisha na mitihani n.k. lazima Chadema wawajibishwe pia.

NA HAWA POLISI NA CCM KWANINI HAWAKUFATA YA JUZI YA NAIROBI, KUWAACHIA TU. WANAJUA CHADEMA WANAPENDA YA KUUANA KUTAFUTA HURUMA.
Kwani huyo mliye muua alikua kwenye mkutano au kwenye dala dala?
 
huyo denti alikua anatafuta nin huko kwenye mikutano ya siasa wakati wenzie wako kwenye maandalizi ya mitihani?
Rip Mwanafunzi,mkuu umenena vyema,ndugu Yangu Pascall,ameandika mengi mkwenye huu uzi na mengi ni ya kweli.Mkuu mwaka 97 nadhani nilikuwa Mombasa,sehemu moja inaitwa ukunda ambapo ni south coast,Kulitokea machafuko ya siasa kipindi kile,mida ya jioni risasi zilirindima sana mimi na ben Mtui,pamoja na watu nisiowafahamu tulienda kuangalia lile tukio,Ben Mtui hakurudi ulirudi mwili wake tu.Mimi ndio nilipeleka ripoti za msiba kwa ndugu na marafiki,alipigwa risasi ambayo haikukusudiwa kwenda kwake.kaka yake Elijah alihangaika na serikali kwa kosa hilo,lakini Ben Never came back to life.Swali nalojiuliza Tulifuata nini pale hadi Ben akauwawa?Tulikuwa na kazi gani pale wakati Polisi wanatekeleza majukumu yao?Aquilina hakupaswa kuwa pale,wazazi wake hawakumtuma kufanya kazi ile.Amewakosea wazazi wake.Risasi hazikupigwa chuoni,Hata kama polisi tutawalaumu lakini tuwe na utaratibu wa kukwepa maandamano yasiyo n VIBALI.
 
Ndio majuha mengine yalikusanywa pale mlimani city na kukatishwa viuno. Let's wake up, vijana tusiposimama kukemea haya ipo siku tutajuta. Tukemee hili kwa nguvu zote, polisi wanatumika vibaya. R.I.P beautful angel Aquilina
 
Back
Top Bottom