Mkuu kwanza hongera sana kwa andiko lako zuri,umeandika vyema na kwa utulivu kiasi,ingiwa mwishoni umehitimisha kwa namna ambayo haina afya sana kwa msomaji wako,kuhusiana na kumshutumu mtoa taarifa juu ya kutoonekana kwa rais (Tundu Lisu).
Kwanza inapaswa utambue kuwa kutoa taarifa(baada ya kupata tetesi) haimfanyi mtoa taarifa kuhusika na tukio moja kwa moja.
Pili,kwa kiwango cha upinzani juu ya serikali,umaarufu na madhila aliyokutana nayo mtoa taarifa,ni wazi kuwa lazima atakuwa na vyanzo vya kuaminika kutoka kwenye system juu ya mambo mengi yanayoendelea humo,unaweza kujiuliza kwanini,lakini jibu la hakika ni kuwa,sio wote waliopendezwa na yaliyotokea juu yake mchana ule kule Dodoma,kumbuka ana marafiki wengi ndani na nje ya utumishi wa umma aliokuwa amehudumu kwa kipindi kirefu,hivyo kuleak kwa taarifa na kuzipata ni jambo rahisi.
Tatu,kumhususisha mtoa taarifa na majasusi ambao walitaka sijui Magufuli ashindwe uchaguzi sio sahihi,sote tulikuwa hapa nchini ,kilichotokea kwenye uchaguzi huo kinajulikana kabisa bila mashaka kwamba haukuwa na credibility yoyote ya kuitwa uchaguzi huru na wa haki(Rejea tamko la Election Observers kutoka East Africa). Upinzani wa Lissu sio wa kutiliwa mashaka kuwa anatumika sijui na mabeberu,amekuwa ni mwanaharakati long ago,kabla hata hajaingia kwenye siasa(Rejea Issue ya North Mara - Nyamongo).
Nne,taarifa za kuchafuliwa kwa mtu huyu zimepigiwa debe na watu wasio na creadibility ya kutoa taarifa kama Cyprian Musiba mara baada ya kwenda ughaibuni kwa ajili ya matibabu zaidi,hapo ndipo ilipanza kusikika oooh anatumiwa na mababeru,sijui wanadhamini matibabu yake ili aje kupinga maendeleo yanayoletwa na Mh hayati Magufuli nk,kwa mtu mwenye akili hapa atajiuliza maswali matatu kama sio matano.
1.Je,kutibiwa nje ya nchi ni kosa,na nini kilipelekea yeye kupigania uhai wake ndani na nje ya nchi,kuna uchunguzi wowote juu ya tukio la kutaka kuuwawa kwa risasi nyingi mchana kweupe katika very monitored area?
2.Serikali iligharamia matibabu yake akagoma?.
3.Hapa nchini kuna hospital ambayo ingeweza kumtibu kwa kiwango cha majeraha yake?.
4.Je,ni mwanasiasa wa kwanza kutibiwa nje?
5.Mtoa taarifa (Cyprian Musiba na wenzake) ni watu wa mlengo gani?
Mwisho,upo ushahidi wa kisayansi kuwa ni kweli pacemaker inaweza kuwa hacked, LAKINI hakuna hata mtu mmoja amewahi ku be hacked, zaidi sana anayefanya hacking sharti awe mita chache kutoka alipo mgonjwa(within 20 feet),hili linaondoa uwezekano wa watu kutoka nje kumonitor pacemaker ya rais,swali fikirishi ikiwa kweli imehakiwa na kupelekea kifo cha rais,ni nani huyo?(maana lazima awe mtu aliye kwenye compaund ya victim,na uhusika wa Lissu unatokea wapi?.
NB.Chochote kinawezekana katika ulimwengu wa ujasusi,visasi na madaraka(siasa).
View attachment 1733034View attachment 1733035