Li ngunda ngali
JF-Expert Member
- Jun 22, 2023
- 707
- 2,572
Ukiifikiria vizuri kauli ya bwana Mbowe aliyoitamka eti HATA WATU WA USALAMA WA TAIFA NA VIONGOZI NDANI YA CCM wanamtaka alisemee hilo jambo la BANDARI ni wazi unang'amua pengine upo usaliti wa wazi ndaniye.
Binafsi, kama mwana CCM na muumini wa falsafa ya ukweli na uwazi naona upo utata bayana wa kinachoendelea.
Hofu yangu ni usaliti unaotamkwa hadharani tena unaofanywa na wasaidizi wake M/kiti unatoa taswira ya wazi safari si salama huko mbele.
Hata huo MKATABA kuwekwa kwenye mitandao ni wazi pia USALITI WA FAIDA ULIFANYWA.
Shime kwa bi mkubwa tafadhari aichunguze vyema nyumba aishio na kwalo ujitahidi kufanya yaliyo ya kweli na haki.
Uzuri wa jambo jema hujieleza lenyewe bila utetezi uchwara. Na vilevile jambo baya daima hukataliwa na kila awaye tena kwa kupaziwa sauti!
CCM tukiendelea kujipendekeza na kujidanganya eti Watanzania bado ni mbumbumbu na tunaweza kufanya lolote kwa kulazimisha hakika tutakuwa tunaendelea kujidanganya!
Lipo jambo moja nitabilialo-UASI WA MAMBO MABAYA KWA TAIFA KUTOKA KWA MTENDA.
Kidumu Chama cha Mapinduzi!