Je, Rais Samia anasalitiwa?

Je, Rais Samia anasalitiwa?

NilIvyokuwa nikufuatilia " Bunge dhaifu'kwa hisani ya Assad" nilmsikia mkuu wao akisema hata mambo yaweje hakuna wa kujitoa (kuvunja mkataba) ,hii nayo imekaaje mkuu?
Wachambuzi Wengi wanaongea vitu hawajavielewa kabisa ...
Mkataba unasema masuala yote ya security yatatoka Kwa nchi husika
Mchambuzi anakwambia tumekabidhi bandari kuhatarisha usalama..,How??
Ama wanafanya kusudi kupotosha au Wana tatizo na lugha ya kiingereza
 
Wachambuzi Wengi wanaongea vitu hawajavielewa kabisa ...
Mkataba unasema masuala yote ya security yatatoka Kwa nchi husika
Mchambuzi anakwambia tumekabidhi bandari kuhatarisha usalama..,How??
Ama wanafanya kusudi kupotosha au Wana tatizo na lugha ya kiingereza
Mkataba ni wa muda gani? kiasi gani na tutalipwa nini kwa Mwezi/mwaka?
 
Hofu yangu ni usaliti unaotamkwa hadharani tena unaofanywa na wasaidizi wake M/kiti unatoa taswira ya wazi safari si salama huko mbele.

Hata huo MKATABA kuwekwa kwenye mitandao ni wazi pia USALITI WA FAIDA ULIFANYWA.

Shime kwa bi mkubwa tafadhari aichunguze vyema nyumba aishio na kwalo ujitahidi kufanya yaliyo ya kweli na haki.

Uzuri wa jambo jema hujieleza lenyewe bila utetezi uchwara. Na vilevile jambo baya daima hukataliwa na kila awaye tena kwa kupaziwa sauti!
Tulishasema mapema, kuna watu wanamuwekea bomu boss wao ila kamwe hawatajitaja, wanasiasa wa Tz ni watu hatari sana, nimejifunza mengi toka JK astaafu uongozi, akina Makamba na baadhi ya waliojumuika na Mwendazake waliiponda awamu ya JK na kuisifia ya Mwendazake, leo hii hayupo, wanamponda kama hakuwa sehemu yao, hata huyu asipokemea hiyo sifiasifia inayoendelea atakuja kushituka amekosea step dakika muziki unakwisha
 
NilIvyokuwa nikufuatilia " Bunge dhaifu'kwa hisani ya Assad" nilmsikia mkuu wao akisema hata mambo yaweje hakuna wa kujitoa (kuvunja mkataba) ,hii nayo imekaaje mkuu?
Hakuna mkataba usio na njia za kujitoa ..hakuna ndo maana hata huu wametaja Hadi mahakama ya usuluhishi....ina maana wanajua kutoelewana kupo
 
We hukuona threads mbili za poisonous ??
Kasema wazi kuna kikundi kimepanga kumkwamisha Rais ...na mkataba uliosambazwa sio mkataba halisi

..lakini watu wanapinga hata mkataba uliopitishwa na BUNGE.

..Je, kilichopitishwa na BUNGE ni mkataba feki?

NB:

..na tafadhali usiite " makubaliano. "

..mkikubaliana jambo fulani na mkaweka sahihi huo sio mkataba?
 
😅😅😂😂😂
...nje kidogo ya mada...., ipo siku nilibandika bandiko lililogusia kale kajiko ka Mbowe( kabla hapajazibwa dance floor) ili kupima niliyekuwa najibishana nae kuhusu mbowe....hakulijua hilo la mishikaki na mayai pale!.....hatahivyo naweza kusema kalikua ndipo ilipoanza Chipsi Mayai...mchanganyo! Ilikuwa mishikaki na mayai, yaani ukiona, hauna tofauti na zege hili la leo!

Zomba, umerudisha na kuleta siku za nyuma mbele, Mbowe alikuwa na tabia za u Dikteta(ubabe ubabe) wewe umeita Superior complex! toka kitambo nyakati zile vurugu(misheni town) zikifanyika pale alikuwa akizikunja kulia na kushoto. Kifupi, nimekuelewa saaana tu!
Dah, napakumbuka sana. Pale kabla ya kina Mbowe kupanya bar, ndio ma born town tunakwenda kula chips samaki enzi hizo. sekela chicken niliwaonea pale kwa mara ya kwanza. Kijiko hiko unachokikumbuka cha mishkaki ndio wakichomwa kuku hapo.

Dah kumbe wa zamani tupo hapa.

Ndio alikua mgomvi mgomvi kwa ajili ya wapambe aluokua nao.

Kuna siku kuna kijana wa mitaa ya jangwani akamwabia tutoke nje, si akakubali wakatoka pale round about. Mbowe akajidai kukunja ngumi, yule mtoto wa jangwani sijui aliruka vipi kichwa. Maana tunamuona puuu yuko chini anapiga miguu na damu zinamtoka mdomoni, jamaa akakimbizwa na wenzake mbio huku wanasema umeua. Wapambe ikabidi wamuwahi kumoepea Mbowe, maana mob ya jangwani ilikua ya kibabe kweli. Mie naona Mbowe lazima aling'oka jino siku ile. Toka iku hio akawa heshima na adabu.

Tumetoka mbali sana.
 
Kwani haya mambo yanahitaji kuamini?si unafatilia trends na unaona..

Why watu wasamabaze mkataba hauna kikomo??

Wakati mkataba uko so clear kuwa mkataba wa HGA duration yake itakapofika mwisho na IGA itakuwa umefika mwisho..
Na HGA bado haijasainiwa
Weka sasa hiyo Duration hapa tuone.
 
Mbowe anatumiwa katika vit ya kibiashara kwa tama yake ya pesaa.

Ashakum si matusi, Ikiwa yupo tayari kuuza utu wake kwa mali. Vipi kuhusu mwili wake?

Asiyemjua Mbowe labda siyo mtu wa Dar. Watu wa Dar tunamfahamu vizuri sana tena sana. Wakuulizwa ni DJ Seydou aliyemwingiza Mbowe katika mambo ya Disco, wakati huo bado anasoma na bar ya Mbowe (baba) ilikuwa ni ya kawaida tu, tena aliipata kiharamu baada ya kuwadhulumu Wahindi waliokuwa na restaurant ya mwanzo ya fisha and chips, enzi hizo ikiitwa Mermaids.Mzee Aikaeli Mbowe Aliwadhulumu kwa kuwa alikuwa bosi wa National Housing.

Aulizwe pia kijana wa Kiarabu, sasa si kijana tena, aliyekuwa ndiye mwenye hivyo vyombo vya disco enzi hizo anaitwa Sudi, wakati huo alikuwa mgeni Dar kutokea Mwanza, walikuwa marafiki sana na Seydou, wote hao walitokea Mwanza.

DJ Seydou, Sudi na Marehemu Khalifa shemeji yake Sudi,wenye vyombo vya disko, na kijana mmoja wa zamani wa mitaa ya Kariakoo anaitwa Fahmi, huyu mtoto wa Kariakoo ndiye walijuana nae mwanzo mwanzo walipotokea Mwanza, ndiye aliwapa connection ya pale ilipokua Bar ili wakapige disko. Fahmi alikuwa ni mpenda kujirusha na toto la kariakoo maarufu.

Ikabidi Fahmi awe kiunganishi wao kwa Mbowe (baba), na DJ maarufu wa Dar. Meb ndiye alimfundisha Seydou u DJ.

Na mbowe huyu tumjuwae kwa kuwa alikuwa kijana mdogo akajikuta kaingia kuipenda kampani ya kina Seydou ya disko. Ndiyo chanzo chanzo cha mbowe kuitw DJ, kwa kuw DJ Seydou na Fahmy waikuwa nae kijana mwenzao.


Nimeweka hayo ili muelewe kua namjua sana Mbowe toka enzi hizi.

Mbowe hata umfanyie wema vipi ni lazima akugeuke linapokuja jambo la pesa na umaarufu. Ana kitu kinaitwa "superior complex" Kwa kua alikulia ushuani na ni toto la kudekezwa nyumbani basi imejijenga kwenye ubongo wake kuwa hakuna zaidi yake.

Huyo kununuliwaa utu wake kuwa msaliti wala hafikiri mbali, hana uwezo wa kufikiri deep. Huyo na Alex Masawe hawana tofauti hulka zao. Yypical wachaga.


Na hayo kayarithi kwa baba'ke, nae kuuza utu wake ili apate mali na ukubwa ulikuw ni kawaida tu kwake (Like father like son). Abishae waulize watu wa zamani, mpaka kuna uvumi kua mkewe alikuwa analala na kiongozi wetu wa kwanza na Mzee Aikaeli Mbowe akilijua hilo lakini akimezea ili muradi wake uende, yaani ficha kombe mwanaharamu apite.


Msaliti wa kwanza ni Mbowe, Magufuli alishamstukia huyo, akmminya. Mbowe anatumikakwenye siasa toka zamani kama "double agent". Ni mtu hatari sana huyo. Nchi zingine huyo angeshakuwa silenced zamani sana.

Inaonekana unajua mengi.
 
Ukiifikiria vizuri kauli ya bwana Mbowe aliyoitamka eti HATA WATU WA USALAMA WA TAIFA NA VIONGOZI NDANI YA CCM wanamtaka alisemee hilo jambo la BANDARI ni wazi unang'amua pengine upo usaliti wa wazi ndaniye.

Binafsi, kama mwana CCM na muumini wa falsafa ya ukweli na uwazi naona upo utata bayana wa kinachoendelea.

Hofu yangu ni usaliti unaotamkwa hadharani tena unaofanywa na wasaidizi wake M/kiti unatoa taswira ya wazi safari si salama huko mbele.

Hata huo MKATABA kuwekwa kwenye mitandao ni wazi pia USALITI WA FAIDA ULIFANYWA.

Shime kwa bi mkubwa tafadhari aichunguze vyema nyumba aishio na kwalo ujitahidi kufanya yaliyo ya kweli na haki.

Uzuri wa jambo jema hujieleza lenyewe bila utetezi uchwara. Na vilevile jambo baya daima hukataliwa na kila awaye tena kwa kupaziwa sauti!

CCM tukiendelea kujipendekeza na kujidanganya eti Watanzania bado ni mbumbumbu na tunaweza kufanya lolote kwa kulazimisha hakika tutakuwa tunaendelea kujidanganya!

Lipo jambo moja nitabilialo-UASI WA MAMBO MABAYA KWA TAIFA KUTOKA KWA MTENDA.

Kidumu Chama cha Mapinduzi!
Nimefurahi umetumia alama ya kuuliza katika kichwa cha habari. Binafsi siamini maneno ya Mbowe, kwa sababu naviona vyombo vya ulinzi na usalama vinamtii pasi chembe ya shaka Rais, Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu. Pili, kuhusu madai ya 'kuvuja mkataba' pia si kweli, kwani hakuna mkataba uliosainiwa! Kwa hiyo hoja hiyo ni sawa na kusema daraja limebomoka kabla ya kujengwa..🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom