Je, tofauti na kuishi milele ni kitu gani kingine sisi wakristo tutapewa?

Je, tofauti na kuishi milele ni kitu gani kingine sisi wakristo tutapewa?

Hizi ni tishatisha za jamii ya kale tu ambazo jamii ya watu walioelimika wa leo haitakiwi kuzifuata.

Tatizo kuna watu wengi wa jamii ya leo hawajaelimika bado.
Kuna siku mwaka fulani hivi nilikua huko nyumbani kwenye kikao cha ukoo kwa heshima tu wakaniomba nifungue kwa sala , nikaanza mambo za logic na hakika ya sala nitimuliwa ikabidi nisepe siku hiyo hiyo kwa sababu niliwauzi mapka viongozi wa kidini walio alikwa🤔🤔
 
Hakika, hapa kuna baadhi ya maandiko yanayounga mkono wazo kwamba watu wataishi milele duniani katika paradiso:


  1. Zaburi 37:10, 11
    “Na bado kitambo kidogo mtu mwovu hatakuwako tena... Bali wapole watairithi nchi, Nao watapata furaha tele katika wingi wa amani.”
    — Hii inaonyesha kwamba wapole, au waadilifu, wataishi duniani kwa amani.
  2. Zaburi 37:29
    “Wenye haki watairithi nchi, Nao watakaa humo milele.”
    — Andiko hili linasisitiza kwamba waadilifu wataishi duniani milele, si kwa muda tu.
  3. Isaya 65:21-23
    “Nao watajenga nyumba na kukaa ndani yake; watapanda mashamba ya mizabibu na kula matunda yake... kazi ya mikono yao wataifurahia kabisa.”
    — Hii ni picha ya maisha ya amani, afya, na furaha duniani, si mbinguni.
  4. Mathayo 5:5
    “Heri wapole, kwa kuwa wao watairithi nchi.”
    — Yesu alithibitisha tena kusudi hilo la Mungu la wanadamu kuishi duniani.
  5. Ufunuo 21:3-4
    “Tazama, hema ya Mungu iko pamoja na wanadamu... wala mauti haitakuwapo tena, wala maombolezo wala kilio wala maumivu hayatakuwapo tena.”
    — Maisha haya ya furaha na kutokuwa na mateso yanaahidiwa kwa wanadamu, na si tu walioko mbinguni.

Maandiko haya yanaweza kutia moyo sana, hasa tunapotamani dunia iwe mahali bora pa kuishi. Unapenda wazo la dunia ya namna hiyo?

Vizuri sana! Tuanze na msingi wa mpango wa Mungu kwa wanadamu, tukitumia Biblia hatua kwa hatua.


Hatua ya 1: Kusudi la Mungu la awali kwa dunia na wanadamu


Soma: Mwanzo 1:27-28


“Mungu akaumba mtu kwa mfano wake... kisha Mungu akawabariki Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze dunia, na kuitiisha…”

Hoja kuu:
Mungu aliwaumba wanadamu waishi duniani, waijaze na kuitunza — si kwenda mbinguni. Kusudi lake halikubadilika.


Swali la kutafakari:
Kwa nini unadhani Mungu aliwapa wanadamu dunia badala ya kuwaweka moja kwa moja mbinguni?


Tukimaliza hatua hii, tunaweza kwenda kwenye hatua ya pili kuhusu sababu ya mateso na jinsi Mungu atakavyorejesha paradiso. Ungependa kuendelea sasa au baadae?
 
Kuna siku mwaka fulani hivi nilikua huko nyumbani kwenye kikao cha ukoo kwa heshima tu wakaniomba nifungue kwa sala , nikaanza mambo za logic na hakika ya sala nitimuliwa ikabidi nisepe siku hiyo hiyo kwa sababu niliwauzi mapka viongozi wa kidini walio alikwa🤔🤔
Sehemu kama zile inabidi utafute excuse tu mkuu.
 
Nitapewa jina jipya asilolijua mtu isipokua anayelipokea pamoja na ile Mana waliyopewa baba zetu jangwani, Kuna zawadi ya kula matunda ya Mti wa uzima uliopo kwenye bustani ya Mungu, sitapatikana na madhara ya mauti ya pili, nitapewa mamlaka ya kuchunga mataifa kwa fimbo ya chuma pamoja na nyota ya asubuhi pia Kuna ahadi ya kufanywa kuwa nguzo kwenye hekalu la Mungu pamoja na jina la Mungu, Mji wake Mtakatifu na Jina la Yesu jipya atakalopewa na mwisho kabisa nitapewa kuketi pamoja na Yesu kwenye Kiti Cha Enzi kama mshindi. Hizo ni ahadi za Yesu kwetu.
 
peponi ni huko kwenye majini na mapepo aka akhera kwenye mito ya pombe na mabikira 72 wenye macho kama gololi.
Wakati Mbinguni ni kWa Mungu mkuu Jehova aliyeumba mbingu na dunia.
MKuu Nakusogezea Maandiko Ya Biblia yanayoonyesha Sehemu Inaitwa Peponi..
Ambayo wanaisifia Kwa Uzuri Ikiwa inamaanisha Ni Mbinguni..

Paulo Alipotembelea Peponi..

2 Wakorintho 12:2-4

Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu.

Nami namjua mtu huyo, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua);
ya kuwa alinyakuliwa mpaka Peponi, akasikia maneno yasiyotamkika, ambayo haijuzu mwanadamu ayanene.


Au Mkuu Umesahau kwamba Ufalme Wa Mungu Uko Peponi?

Luka 23:42-43
Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi.
 
Kama hazina zetu zipo mbinguni, hazina za duniani zipo kwa ajili ya nani?

Kama mabikra wapo mbinguni, mabikra wa duniani waliwekwa kwa ajili gani na kwa ajili ya nani?
Mmeekewa nyie wanaume wa duniani, yani mnatutafuna mabikra wa duniani wenye yutiayi na bado wa mbinguni wasio na yutiayi.
Huoni km deal hilo Info 😹😹😹
 
Tendo la Ndoa Si kitu Bora kwangu Na sio kipaumbele, Vipi kwa wale ambao kwao ni Kipaumbele..
Zawadi zitakuwa Tofauti?
Mungu aliyekuumba anajua kitu gani akikuba kwako ndio bora zaidi. Kuna watu wanapenda vitu kwa sababu ya movie, western brainwshing etc.
Pia ubora wa tendo la ndoa ni subjective.
Inategemea na mtu na mtu.
Linakuzwa sana na wafanyabiashara zinazotegemea ngono kama mtaji.

Mimi naamini kuna bora mbadala wa bora zote ambazo tuznaiona bora sasa mkuu wangu.
 
Ukishaona kuna utata wa tafsiri, muktadha, lugha, utamaduni, etc, katika kutafsiri neno la Nungu, huo nao ni ushahidi Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upwndo wote hayupo.

Angekuwapo, kila mtu angejua ukweli bila kuwa na utata wowote.
Hakuna utata hapo ila kuna upana wa tafsiri. Kuna utajiri mkubwa wa tafsiri zinazoonyesha upana wa maelezo ya Mungu ili yaguse kila angle. Usugu wa moyo ndio utaona huu ni udhaifu.
 
Mungu aliyekuumba anajua kitu gani akikuba kwako ndio bora zaidi. Kuna watu wanapenda vitu kwa sababu ya movie, western brainwshing etc.
Pia ubora wa tendo la ndoa ni subjective.
Inategemea na mtu na mtu.
Linakuzwa sana na wafanyabiashara zinazotegemea ngono kama mtaji.

Mimi naamini kuna bora mbadala wa bora zote ambazo tuznaiona bora sasa mkuu wangu.
Mkuu hii nguvu ya kutaja Mungu unapata wapi wakati umeshindwa kuthibitisha?
 
Back
Top Bottom