Je, Tundu Lissu anazo sifa za kuwa Rais wa Tanzania?

Urais ni zao la wakati.. Na sio kutaja majina kabla ya wakati..Wakati utakapofika ni vyema matatizo ya nchi yakaainishwa.. Kisha tukachagua mwenye uwezo wa kuyatatua matatizo hayo kati ya wale watakaokuwa wamejitokeza..
 

..kilichowazuia Ccm 2014 kutuletea katiba yenye mambo mzuri isipokuwa serikali 3 ni nini?

..au kitu gani kinawazuia Ccm kutupatia katiba nzuri sasa hivi wakati wameshikilia mihimili yote?
 
Urais ni zao la wakati.. Na sio kutaja majina kabla ya wakati..Wakati utakapofika ni vyema matatizo ya nchi yakaainishwa.. Kisha tukachagua mwenye uwezo wa kuyatatua matatizo hayo kati ya wale watakaokuwa wamejitokeza..
Hapata, baba wa taifa (RIP) aliwahi kusema, wale wote wanaotaka kuwa wagombea lazima wajulikane mapema ili watu wapate muda mrefu wa kuwajadili. Alisema kuwa kama CCM ikishamtangaza mgombea wao itakuwa tayari imeshamtangaza Rais wa nchi hii kwa 99.99%. Bahati nzuri CCM tayari wameshamtangaza mgombea wao 2025 mapemaa kuwa ni Rais Mama Samia, hivyo ni vema na wagombea wa upinzani wakajulikana mapemaa ili wananchi tupate muda wa kuwafahamu na kuwachambua vya kutosha kama hivi tunavyofanya kwa mama Samia na Lissu. Hii ni afya kwa wapiga kura, wagombea na taifa pia, wasichukie watu wanapowadadavua mapema madhaifu na mazuri Yao.

Uchaguzi wa Marekani ni 2024, mchAkato rasmi wa wagombea bado lakini watu tayari wanawadadavua Trump na Biden kwakuwa Trump kaonyesha Nia ya kuhombea tena kupitia Chama chake Cha republican.
 

..Samia hana uwezo wa kushindana na Lissu kwa hoja.

..Lissu ni msomi mzuri kuliko Samia na ana uelewa mpana wa masuala mengi ya kiuongozi na kiutawala.

..Lissu pia ana historia ya kutetea wanyonge wa nchi yetu na ni mwanasiasa ambaye hajachafuka kwa rushwa.

..Samia amemzidi Lissu kwasababu yuko ndani ya serikali hivyo dola na mifumo yote inambeba.
 
Hata hiyo 'democracy' huko kwao imegota.
 
Bwana Mayalla, kwamba TL akishindwa na mwanamke itakuwa ni aibu??? Hii comment yako imeniacha na maswali mengi Sana....kwamba:

Kama ni aibu kwa Tundu Lisu, je, ni aibu kwa Watanzania wote wanaume kuongozwa na mwanamke?

Je, mwanamke ni kiumbe thaifu dhidi ya mwanaume, au una maana gani?

Je, una lengo la kudharirisha wanawake?
 

..hii tuliyonayo Tz ni demokrasia yetu pekee, sio demokrasia ya magharibi.

..demokrasia ya Tz tume ya uchaguzi inateuliwa na mwenyekiti wa chama tawala.

..demokrasia ya Tz wasimamizi wa uchaguzi ni makada wa chama tawala.

..demokrasia yetu haifanani hata kidogo na demokrasia ya magharibi.

..Watz tuache kutafuta visingizio huko nje mambo yanapotuharibikia.
 
Watu wanataka maji, hospital, barabara, umeme, chakula, mkongo, ajira na amani hawataki maneno na uelewa wa Ulaya sijui sheria. Sheria zote muhimu sana kwetu ziko kwenye Katiba ya nchi.
 
Bwana Mayalla, kwamba TL akishindwa na mwanamke itakuwa ni aibu??? Hii comment yako imeniacha na maswali mengi Sana....kwamba
Hakunaga mashindano yoyote kati ya mwanaume na mwanamke, wanaume wanatakiwa kushindana na wanaume wenzao, wanawake na wanawake wenzao. Mwanaume ukishindana na mwanaume mwenzio ukashindwa, its normal umezidiwa, lakini mwanaume ukishindana na mwanamke ukashindwa kiukweli ni aibu!. Hii sio mara yangu ya kwanza kushauri mtu asigombee kuepuka aibu ya kushindwa!. Uchaguzi wa 2015 kwa Zanzibar, nilishauri hivi, Kumuepushia aibu ya Kushindwa, CCM isimsimamishe Dr. Shein hawakusikia wakamsimamisha na kweli ali... ilibidi Jecha kuokoa jahazi kwa kupindua meza!. Mwanaume rijali uneyesimama kushindwa na mwanamke anayechuchumaa ni aibu!. Sometimes bora kufa kishujaa huku umesimama kuliko kuishi huku umepiga magoti!. Lissu ni shujaa msimuaibishe!
Kama ni aibu kwa Tundu Lisu, je, ni aibu kwa Watanzania wote wanaume kuongozwa na mwanamke?
It's the other way round, yaani kitendo cha Mwanamke kuongoza nchi ni credits kubwa sana kwa Mwanamke kufuatia mfumo dume kuwa vitu Mwanamke hawezi, ukiwemo urais!, hivyo huyu Mwanamke ame wa prove wrong kwa kuonyesha uwezo kuliko wale wanaume 4!. Je, kuna kazi za kike na za kiume? Fupa hili lililowashinda wanaume wanne, mwanamke mmoja ataliweza?
Je, mwanamke ni kiumbe thaifu dhidi ya mwanaume, au una maana gani?
Hili mbona sio swali ni jibu, kwani wewe unaonaje kuhusu strengths na weaknesses kati ya mwanamke na mwanaume, wanafana?. Mwanamke ni kiumbe dhaifu ila kuna wanawake wa shoka, they are strong than men!. Wanawake wengine wenye kujitambua kuhusu strength of a woman, they use that strength and becomes above men!. Siku ya Wanawake Duniani: Je, tuna Wanawake wenye sifa za Presidential Material?
Je, una lengo la kudharirisha wanawake?
No sina lengo la kudhalilisha wanawake bali kumuepushia aibu huyu shujaa wetu, mtu kushindwa na Mwanamke ni aibu ya mwaka, ambayo itapelekea ahamie kule jumla!.
P
 
Kule mashuleni na vyuoni wanaume hawashindwi na wanawake darasani, kwenye tafiti/machaposho?
 
Kule mashuleni na vyuoni wanaume hawashindwi na wanawake darasani, kwenye tafiti/machapisho?
Wanashindwa ila sio aibu kwasababu ni mitihani ni mashindano kwa wote hujui unashindana na nani, hivyo mwanamke akiibuka kidedea, ni wewe tuu ndio unajiaibikia ndani yako kushindwa na demu, lakini hauabiki na jamii, lakini hii ya kujua CCM itasimamisha Mwanamke 2025, halafu Chadema ikasimamisha mgombea mwanaume, mwanaume huyo akishindwa na mwanamke ni aibu!.
Nimewashauri Chadema na wapinzani Iwapo Watanzania wataamua 2025 twende na Mwanamke, mnaonaje tukiwashauri CHADEMA wasimamishe Mwanamke? Maana Mwanaume kushindwa na Mwanamke ni aibu!
P
 
Watu wanataka maji, hospital, barabara, umeme, chakula, mkongo, ajira na amani hawataki maneno na uelewa wa Ulaya sijui sheria. Sheria zote muhimu sana kwetu ziko kwenye Katiba ya nchi.
..samia na ccm yake wameshindwa kutuletea yote hayo uliyoyataja, pamoja na katiba bora, hivyo wanastahili kupumzishwa.
 
Mtu yeyote ambaye hayuko mentally stable hana sifa zozote zinazomqualify kuwa rais. Tuweni serious na urais wa nchi, tafadhali.
 
Rais wa nchi yetu awe na sifa zipi?

Je, ni nani anazo sifa nyingi za kuwa Rais ajae? Je, Tundu Lissu anazo sifa hizo pia?
Sifa anazo tele kwa mujibu wa katiba yetu. Mpeni kura za ndio
 
Ni kweli kaka, hata baba alikuwa ananiambia usishindane na dada zako kwenye kwenda kuchunga ng'ombe, na na mama aliwaambia dada zangu msishindane na kaka yetu kwenye kupika na kuosha vyombo, hata pocket money ya shule dada walikuwa wakipewa kubwa kuliko mimi kwasababu ambazo nilikujaelezwa baadae sana. Ni heri akapima kina cha maji kwa kutumbukiza fito badala ya kuyapima kwa kutumbukia mwenyewe. Mama Samia ni mmoja tu tangu tupate Uhuru miaka zaidi ya 60 iliyopita, wacha amalizie miaka yake 5 mingine kisha turudi kwenye mminyano wa wavaa kaptura menyewe kwa menyewe.
 
Shida ni kiburi,Jeuri,dharau na ubishi pamoja na ubabe kisu anachotumia kuwachinjia mahasimu wake akiwamaliza ataturudia sisi wanyonge tutaburuzwa mpaka basi.

Sifa za Rais lazima awe muungwana asimamie mifumo yote ijiendeshe kwa Sheria tulizokubaliana waajiliwa na wateuliwa wote watimize wajibu wao.

Kila Mwananchi atende wajibu wake na ajione kwamba ni mwenye nchi hii na vizazi vijavyo vinayo haki ya kunufaika na matunda yatakayopatikana.
 
Rais wa nchi yetu awe na sifa zipi?

Je, ni nani anazo sifa nyingi za kuwa Rais ajae? Je, Tundu Lissu anazo sifa hizo pia?
Ni nani huyo aliyewahi kum-rule out TL kuwa hana sifa za kuwa Rais wa JMT?
 
Mkuu 'Drifter', nisingeweza kuliweka hili vizuri kuliko ulivyolieleza hapa mwenyewe. Ninakupongeza sana kwa uwezo wako huu wa kujieleza vizuri.

Sasa tunaona jitihada zinazofanywa kwa maksudi kabisa, kuwachanganya akili wananchi kwa mbinu zilizochoka kama zinavyowasilishwa na haya makundi yanayozileta kwenye jukwaa hili na kwingineko, kujaribu kuvuruga tu akili za wananchi wasitumie haki yao ya kuwachagua viongozi wanaowataka wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…