Je, ulifika Third floor(30s) bila kuwa na familia? Hali ilikuwaje?

Comment Bora sana brother, hongera sana una upeo mkubwa sana.
 
Mimi nipo kama wewe, 31 muda si mrefu sina mtoto na hata mchumba wa kuoa sina, kuna muda kichwa kinawaka moto ile mbaya ila ninasema bikra kuchelewa kuliko kuwahi maana ninayo yaona kwenye ndoa zao wengine moyo wangu hubaki na masononeko ila nina tamani sana kuwa na mtoto, yaani mnoooo ila suala la kuoa bado halija nikaa kichwani vizuri ila suala la mtoto ndiyo lipo kichwani sanaa nisije itwa babu badala ya Baba ha ha ha ha . Nina amini nitampata mtu sahihi wa kunipa mtoto na yule wa kumuoa.
Kwahiyo na wewe usijipe presha kupitiliza
 
Mkuu umenena vyema... Lakini how Jamii forums 🤔🤔
 
Well said mkuu. Hii mada imebeba ujumbe mkubwa sana kuna vya muhimu vya kujifunza hapa.
 
Familia inaanza na wawili mkiwa wapenzi kabla ya kuingia uchumba na mwishowe mke na mume ambapo Mungu akijalia watoto nao watazaliwa. Ila siku hizi vijana wa kiume wengi wanakataa ndoa na wengine wanakwepa majukumu yao ya kuwa na familia ambapo inawafanya vijana wa kike kukosa wachumba na mara nyingi wanaishia kuzalishwa tu na kubaki kuwa single mother. Pia ugumu wa maisha umepoteza hamu ya kuingia kwenye ndoa kwa vijana wengi hasa wa kiume ambayo inawaathiri wanawake kukosa wanaume wa kuoa.
 
Dunia ina mambo mengi na changamoto nyingi sana.

Kuna watu kutokuwa na mtoto au kuchelewa kupata mtoto haitokani na maamuzi yake, kuna nguvu ya tofauti inayolizuia/kuchelewesha hilo kuwezekana ukiachana na wale ambao wana changamoto za afya ya uzazi.

Sitaki niende kwenye hili sana kwa kuwa siwezi kulielezea vyema Donatila utanisaidia ufafanuzi mzuri.

Ni hivi kuna watu wamefungwa kupata wenza na watoto, wapo watu wana sifa zote nzuri lakini likija suala la kupata mwenza wa kudumu nae au kupata watoto ni mtihani mgumu. Na hii hali inawatesa wengi sana bila kujua.
 
Mada muhimu sana, hasa kwa wanaohitaji familia na watoto. Kwa personal experience, ukifika 30s lazima kengele ilie kichwani, lazima uhisi kuchelewa, tena ikiwa hujapata mtu 'sahihi' ndio msongo unaongezeka.

Kupata watoto kwenye mid 20s na early 30s ni vizuri zaidi kuliko mid 30s na early 40s, kupanga ni juu yetu lakini nature ndio inatuongoza, huna jinsi.

Muhimu, usiwe too desperate, tulia tafuta mtu sahihi (sio ili mradi), then halalisha maisha yaende, ukiwa too picky pia sio sawa.
 
Thread closed

[emoji3590][emoji3590]
 
Maisha yananipa experience tofauti, Sikuwahi kufikiria kama ningefika third floor bila kuwa na familia wala watoto, kuna muda nahisi kupanic nahofia watoto wasije kuniita bibi badala ya mama, au kukosa kabisa sababu ya umri mkubwa🤔

Usije ukaamua kuwa singo maza tu kwa sababu ya hiyo panic...

Nina cousins zangu wa kike, wanalea watoto tu sasa wasio na address kwa sababu ya pressure hizi za sijui umri kwenda, malengo kutotimia etc...

Ikumbukwe tu kuwa, waoaji nao wamepungua wakati idadi ya wanawake nayo ni kubwa, hivyo soko halipo kwenye uwiano sawa...
 
Na mimi bado dakika kadhaa niiguse 30, sina ndoa, sina mtoto, sina demu wa maana huu mwaka nimedhamiria kumzalisha mtu aisee maana sio poa....
 
Mkuu umenena vyema... Lakini how Jamii forums 🤔🤔
Mwanamke anayetumia JF, maanayake ni mwanamke mwenye EXPOSURE KUBWA, anajielewa na ana thinking kubwa sasa wanawake kama hao mwanaume aliye timamu hawapendi suala sio kuwa na hivyo vitu bali wanawake wengi wakiwa na hivyo vitu inakuwa ngumu wao kuwa SUBMISSIVE kwa mwanaume.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…