Utabisha ila utofauti upo wazi kwenye hadithi ya sauli. Basi ngoja nikupe maandiko mengine na yenyewe tuone utasemaje
hakuna utofauti,labda kama umeuliza ili ubishane sio ueleweshwe,unajua ni kazi ngumu sana kumwelewesha mtu aliyeamua kukumbatia upumbavu???
1. Mungu anatubu au tuseme anaomba msamaha Kwa kumfanya sauli mfalme(I Samuel 15:10 to 11) [hapo kumbuka anajua kila kitu Kwa hiyo alijua mapema sauli ataharibu anajutia nini sasa]
hapa Mungu hajuti,ukisoma kwa utulivu,haya yalikuwa maono ndani ya moyo wa samweli,kwamba inawezekana kabisa Mungu anajutia kunitawadha kuwa mfalme,haya ni mawazo ya kila binaadam hata ukizini wazo linalokujia ni kwamba Mungu atakuwa kanikasirikia.
Huyo huyo samweli tena anasema mungu hawezi kutubu maana sio mwanadamu (I Samuel 15:29)
kabisa kabisa,rejea maelezo yangu hapo juu,Mungu hawezi kujuta,kujuta utajuta wewe mwanadamu,
ndio sababu mnaambiwa someni kitabu hiki mkiwa mmetulia mwili na akili.
Tena samweli anasema mungu alitubu au tuseme kuomba radhi au kujuta kumfanya sauli mfalme wa Israeli utafikiri alikuwa hajui kama ataharibu.
Mungu hawezi kutubu,kama nilivyokueleza haya yote ni maono ya samweli,sababu hata nikikwambia ulete ushahidi Mungu akiomba msamaha hauta kuwa nao
(I Samuel 15:35). [emoji23][emoji23] HUYU NI MWANDISHI MMOJA TU.
2. After the feeding of the multitude, Jesus went to Gennesaret. Mark.6:53.
After the feeding of the multitude, Jesus went to Capernaum. John.6:14-17.
Kati ya Luka na Marko nani yuko sahihi Yesu alienda wapi baada ya kulisha umati mmoja anasema Gennesaret mwingine Capernaum
hii ni sawa na classmate wako 2 waelezee watu kwamba ulipomaliza shule mmoja aseme ulienda tabora mwingine aseme ulinda nzega.
3. Yuda alimbusu yesu? mathayo anasema ndio yohana anasema hakuweza kusogea karibu vya kutosha kumbusu hivyo hakumbusu.
(Matthew 26:48-50)(John 18:3-12)
mbona hapa pia hamna mkanganyiko!!john inazungumzia Yuda kutoa ishara,mathew inazungumzia baada ya kundi lote kumfikia Yesu,na ili usichanganye maelezo yao usichanganyikiwe,kwa John kuna maelezo kwamba walirudi nyuma wakamsujudia,hii inamaana walimkaribia kabisa.hawa si kwamba hawakuielewa ishara ila waliingia ubaridi ghafla mpaka kusujudu.
4.Yesu alikuwa wapi saa la sita la siku ya kusulubiwa Marko anasema kwenye msalaba yohana anasema kwenye mahakama ya pilato
(Mark 15:23) (John 19:14)
lakini si una taarifa kwamba hakuna mwanafunzi aliyethubutu kusogelea zoezi zima isipokuwa petro ambaye naye kabla hakujapambazuka likataka kumkuta jambo!!!!
tufanye walikuwepo wote eneo la tukio wakitizama kama wananchi wengine,nani kati yao hawa wawili alikuwa na saa ya mkononi??rolex,seiko,apple ama hata gilex😅😅
5.Nani alimuua Goliati
David (I Samuel 17:23, 50)
Elhanan (2 Samuel 21:19)
ysoma hii 2 samweli 21:19 kuanzia nyuma utagundua goliath hakiwa mmoja,walikuaa na sifa mbali mbali.
6. Kuna mtu apa alimuona mungu na maisha na hakufa Genesis (Mwanzo) 32:30
24 inasema kuna mtu alikutana na Yakobo wakaanza mieleka,yakobo baada ya kuona kamudu,Yeye ndiye akadai kaonana na Mungu,nawewe unadai ni kweli yakobo alionana na Mungu😃
vipi mtu huyo nikikwambia hakuwa na tofauti na Yesu tumwitaye Mungu utanuna ama utazira kula!!!!
Musa pia alionana na Mungu katika umbo la kichaka kiwakacho moto,lakini tutasema hakuonana naye sababu haikuwa katika utukufu wake.
Yohana alisahau akasema hakuna aliemuona mungu (John 1:18)
hakuna aliyewahi kuwona Mungu katika Mwili huu wa kindezi,wala sio uongo
Tuanzie hapa kwanza mkuu
Sent from my M10_Max using
JamiiForums mobile app