ShesRise_1
JF-Expert Member
- Aug 21, 2025
- 22,235
- 51,111
- Thread starter
-
- #81
Hapa sasa upo kwenye mada husikaKwakuwa kifo kina raha kwa mujibu wa sayansi, nitapendelea kifo kisicho cha ajali kwakuwa natamani kuipata raha hiyo.
Kwa kweliNyie si mnapenda kujipakulia minyama...
Mimi siamini sana kwamba jinsia fulani inaongoza kufarikiIla nina uhakika wanawake mnateseka zaidi kwasababu mnazeeka sana.
Sio kwamba mnaongoza kufa, wanaume ndo tunaongoza!Kwa kweli
Mimi siamini sana kwamba jinsia fulani inaongoza kufariki
Mtu yoyote jinsia yoyote anaweza kufa wa kwanza
Wanasema kuna kemikali zinaachiwa kwenye ubongo zinakufanya upagawe. Ni kama vile ubongo unakuaga.Hapa sasa upo kwenye mada husika
Hivi kumbe kwa mjibu wa sayansi kifo kina raha?😳
Shukran sana mkuu🙏Ni mawazo mazuri sana mkuu.
Mimi bando ngazi chache nitaingia huko kwenye 30Nitajibu tokana na upeo wangu,
Niko late 30s, nashukuru Mungu kuwa hapa na kila siku maombi yangu makuu kwa Mola wangu ni mawili.
Kwa namna ulivyoandika ni dhahiri kwamba furaha inajitegemea yenyewe haihusiani na utajiriFURAHA
Nikisema furaha inaweza ikawa jambo dogo kwako zaidi ya utajiri unauomba, lakini mimi Furaha ni kitu kikubwa sana kwangu na nijukumu kubwa la vitu vingi kwa pamoja namwomba Mola wangu.
Ili niwe na “furaha” lazima niwe na afya njema, lazima nilale pazuri, nile vizuri niwe na familia yenye afya njema na furaha na mahitaji yao na kila kitu kwa ujumla(hope unanielewa)
Huyo Mungu unaemuamini ni matumaini makubwa atakujibu kama uombavyoMWISHO MWEMA
Najua mwisho wetu ni “maradhi” ama “Ajali” ni wachache sana wanakufa wakiwa usingizini. Maombi yangu nimekuwa nikiomba sana nife kifo cha usingizini ama kifo cha ghafla(Mungu aniepushie maumivu).
Namwomba sana Mola wangu asiniache na mtihani wa kuugua sana na kuwatesa ndugu zangu na watu wangu wa karibu, nisiumwe mpaka ikafika hatua ya kuchangiwa na watu kuangaika ili niendelee kuwa hai..
Hapa natamani kukujibu au kukuliza jambo ila nahofia Kukufanya uone nakuchunguza sanaNamwomba Mungu nisiishi umri sana kupitiliza hata sasa akinichukua ni sawa mana nimeshaona mengi na sioni mantiki ya haya maisha ambao kuna watu bado wanang’ang’ania kuendelea kuishi.
NJE YA MADA
Siyafurahi sana maisha sababu nimeshaboeka nayo, na kama kungekuwa na nafasi ya kuchagua kuzaliwa nisingekuwepo, kuna watu wapo dunia bila kuwa na purpose na najiuliza kwa nini Mola aliwaleta na kwanini hakukua na choice ya kuchagua kuwepo dunia, mfano mtu ana mtindio wa ubongo ama mtoto kadhaliwa leo na kafa leo(why cruel world)na sasa naelewa kwanini watu wanajiua(sijasema najiua). Kuna kukinai maisha hata kama unapata kila kitu. System ya maisha ni mzunguko ule ule kwa sababu hatutosheki na kuridhika, maisha tunaona yana maana sababu tunaendelea kutafuta na kujilindikizia akiba iliyopitiliza na tusiohitaji na ambaye hana anajipa moyo kila siku aendelee kutafuta mpaka anakufa.
Na hata tungekuwa tunaishi milele tungekua soool bored 🥱
Wanasema bahati haiji bila juhudu ila ukweli kuna watu wanajuhudi na hawabahatikiOMBI LA ZIADA “BAHATI NJEMA”
Namwomba mola wangu mara zote bahati njema. Bahati ya kuwa na familia njema, afya njema,watoto wema, kifo chema..
Ushawahi kukutana na mtu hana ujuzi, maarifa, elimu wala chochote ila ana bahati njema? Kila anachogusa kinafanikiwa. Kila siku anapanda vyeo
Mfano BASHITE
Huyo jamaa yuko na bahati njema tu ila hana maajabu. Nisimwongelee sana ila ukitafakari utaelewa ninachomaanisha
Shukran sana Bro umejibu vizuri sana napenda aina ya watu wenye kuelewa mada na kuchangia kama weweHope nimejibu mada na ya nje ya mada.
Hii ni kwa mjibu wa utafiti?Sio kwamba mnaongoza kufa, wanaume ndo tunaongoza!
Ni kweli kabisa kuishi mpka unaanza kuanikwa juaniIla kwa vile mnaishi maisha marefu mnateseka zaidi kwasababu siku zote uzee una magonjwa.
Pole maa na nisamehe bure😊Daah! Sijui kwa nini ila nimejikuta tu napata woga. Lol.
Una upendo wewe hutaki kuwaacha uwapendao na Trauma ya kukutafutaKwangu mi chochote tu ilimradi wale watu wangu wa karibu wanione na wajue nimevuta kisiwe cha kupotea au cha kwenye maji nikaenda kufia mbali halafu nisionekane tena.
Ooh hiii tutaithibisha wakati ukiwadiaWanasema kuna kemikali zinaachiwa kwenye ubongo zinakufanya upagawe. Ni kama vile ubongo unakuaga.
Unaona kumbukumbu za maisha yako, ndugu waliotangulia, mwanga mkali nk. Kuna watu hutabasamu kabisa!
Ndio, mfano hapa tz KE mmetuzidi ME miaka 5-6 kwenye life expectancy.Hii ni kwa mjibu wa utafiti?
Sasa mbona sisi unatuuliza maswali?Wewe ukiulizwa swali kama hilo uliloniuliza utajibu vipi?😅
Yaani hilo swali fanya kama unajiuliza mwenyewe?
Kisha angalia umepata jibu gani ?
Mimi siwezi kukujibu aisee
Tosheka tu na majibu yako utakayojijibu mwenyewe 😊
So Tanzania kuna uhaba wa wanaume?Ndio, mfano hapa tz KE mmetuzidi ME miaka 5-6 kwenye life expectancy.
Sio lazima wote mjibu kwa sababu sio kila mada mtu yoyote ana mudu kuijiibu na hilo si kosa mtu kushindwa kujibuSasa mbona sisi unatuuliza maswali?
Heh ama kweli 😁Immortal
Hapana, ni kwamba wanaume hufa mapema zaidi kwa wastani. Ulevi, kazi ngumu na msongo wa mawazo vinatumaliza.So Tanzania kuna uhaba wa wanaume?
Kuna kitu kinaitwa the art of dying ambacho wengi huwa wanakikwepa kwa sababu ya hofu ya kisaikolojia waliyo nayo.Pia, kwa nini kuzungumzia kifo huonekana kama uchuro?
Binafsi sitaki kifo changu kiwe ni kifo cha kuhurumiwa, sitaki siku zangu za mwisho ziwe za watu kuniletea chai kitandani huku wakati huo wakisubiri nimeluke ili watafute nafasi ya kugawana mali zangu, hii ni dignity erosion.Umewahi kutamani kifo chako kiwe cha aina fulani?
Kifo kizuri ni kile ambacho hakikupi nafasi ya kuanza kujuta "laiti ningejua" , kwa maana nyingine hiki ni kile kifo kinachokuja baada ya wewe kuwa umetimiza malengo yako yani unakuwa umeshafanya uliyopaswa kufanya (huu ni mtazamo wangu) , kinakuwa ni final stop of your successful journey na sio msiba wa kusikitisha.Mara nyingi husikia watu wakisema,
Yule amekufa kifo kibaya
inasikitisha sana🥲
Hapo unajiuliza, kama kuna kifo kibaya, je, kuna kifo kizuri?
Ukifuatilia watu wengi ambao huwa wanaogopa kifo au kukiongelea kifo naweza kusema kwa namna moja ama nyingine ni kwa sababu wanaishi maisha ya impulse yani wanaishi bila mpango, bila maadili, na bila kusudi.Kuna mtu aliwahi kujinunulia jeneza lake mapema na akaonekana kama ana matatizo ya afya ya akili au kama anajichulia
Lakini ukitafakari, hata usipolinunua mapema bado ukweli ni kwamba siku moja utakufa tu
Kwa nini jamii hulichukulia jambo hilo tofauti?
Ndugu mdau,Binadamu tuna ndoto, malengo na matamanio mengi kuhusu maisha Tunapanga kuwa na nyumba nzuri, gari, ardhi, biashara na mafanikio mengine mengi
Lakini umewahi kujiuliza kuhusu mwisho wa safari yako?
Umewahi kutamani kifo chako kiwe cha aina fulani?
Mara nyingi husikia watu wakisema,
Yule amekufa kifo kibaya
inasikitisha sana🥲
Hapo unajiuliza, kama kuna kifo kibaya, je, kuna kifo kizuri?
Labda kile kisichoambatana na maumivu makali, mateso ya muda mrefu au taabu nyingi
Je, hicho ndicho kifo kizuri?
Pia, kwa nini kuzungumzia kifo huonekana kama uchuro?
Kuna mtu aliwahi kujinunulia jeneza lake mapema na akaonekana kama ana matatizo ya afya ya akili au kama anajichulia
Lakini ukitafakari, hata usipolinunua mapema bado ukweli ni kwamba siku moja utakufa tu
Kwa nini jamii hulichukulia jambo hilo tofauti?
Cha kushangaza ni kwamba watu wengi husema
Nataka nioe /kuolewa nipate watoto na nyumba kalii gari kaliii
Biashara zaidi yaani uwekezaji wa kila namna (na hii sio mbaya ni sawa kabisa kua na future)
Lakini ni nadra sana kusikia mtu akisema anatamani kifo chake kiwe cha namna fulani
Maana ukweli ni kwamba baada ya yote hayo mwisho ni kifo!
Lakini sasa ikitokea mtu akasema anatamani kifo chake kiwe cha namna fulani watu humuona kama hayuko timamu
Na akisema hivyo, wengi huanza kuona kama hayuko sawa kiakili
Sijui kwa nini huwa hivyo🤔
Binafsi, sitamani kufa sasa😅
Natamani niishi miaka mingi zaidi kwa sababu sijui chochote kuhusu maisha baada ya kifo
Sehemu ninayoijua ni hii dunia, na ningependa niendelee kuwepo kwa muda mrefu zaidi
Lakini pia najua ipo siku moja nitaondokana wewe pia utaondoka📌
Ila sasa kwa upande wangu siku hiyo ikifika
Natamani au ningependa 👇
Nife kwa amani🤗
Nisiwe na chuki wala kinyongo na mtu yeyote
Sitamani kuugua magonjwa ya muda mrefu yanayomchosha mgonjwa mwenyewe na kuwachosha wanaomlea& wanaomuuguza
Pia sitamani kifo cha ajali au kifo chenye maumivu makali sana
Kama ni kuugua, basi iwe kwa muda mfupi
Hii huwapa nafuu hata wanaobaki, kwani hawabebeshwi mzigo mkubwa wa muda, nguvu na gharama za kukuuguza
Kama ningekuwa na choice, ningependa siku yangu ifike nikiwa nimelala kwa utulivu, kisha niondoke kimya kimya bila kelele, bila taharuki na bila mateso makubwa
Je, wewe umewahi kuwaza kuhusu kifo chako? Kama ungepewa nafasi ya kuchagua, ungependa kifo chako kiwe cha namna gani?
Team Messi 🔥🔥🔥🔥
ShesRise_1 🤚