TANZIA Jecha Salim Jecha afariki dunia akipatiwa matibabu hospitali ya Jeshi Lugalo

TANZIA Jecha Salim Jecha afariki dunia akipatiwa matibabu hospitali ya Jeshi Lugalo

Kwahiyo maalim seif ni mbaya ??!!! Maana alianza yeye Jecha kafa baadae!
Punguza maswali ya kijinga. Ingekuwa hivyo, mtume angekuwa hai mpaka Leo. Watu wanaongelea ujinga alioufanya huyo Jecha Zanzibar. Watu wameshakabidhiwa vyeti vya ushindi yeye anaamka na kufuta matokeo. Very stupid
 
Unaandika upumbavu halafu unasema eti "wabillaahil tawfiyq.??!!"
Unataja jina la Allaah baada ya kuandika maneno ya jeuri na uadui kwa muislamu mwenzio aliyekufa au wewe ni kafiri?!
Wewe muislamu kweli kuendeleza maneno ya visasi na marehem...
Hakuna kitu kama hicho avune alichopanda, tena wamzike haraka asije akazinduka
 
Hapa ndio mwisho wetu sote ila kwa madhalimu ni mwisho mbaya sana. Majitu yanadanganyika na maisha mafupi ya duniani, wakati tutaiacha tu. Mtu unawezaje kuiingiza nchi kwenye hasara kwa kuiuza kiwepesi hivyo kwa Waarabu? Halafu unalazimishia kila mtu awe upande wako! Kifo kitawakuta mkiwa mmevimbiwa kwa mali za wizi /rushwa.
 
Unguja. Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec), Jecha Salum Jecha amefariki dunia, leo Jumanne, Julai 18, 2023 katika Hospitali ya Rufaa ya Jeshi Lugola, jijini Dar es Salaam.

Jecha ambaye jina lake lilipata umaarufu baada ya kufuta uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kisiwani Zanzibar.

Akizungumza na Mwananchi Digital, Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapindzi (CCM) Zanzibar, Dk Muhamed Dimwa, amesema chama wamepokea kwa masikitiko taarifa za kifo hicho.
Huu ni msiba mkubwa hata Makamu Mwenyekiti wetu wa chama (Dk Hussein Ali Mwinyi) amesitisha ziara yake Pemba kwa ajili ya kuwahi maziko yake," amesema
 
Jecha ninaemjua mimi hajafa naamini yupo ktk harakati za kukata rufaa au kukifutilia mbali kifo kama alivyofuta matokeo ya uchaguzi kule Zenjibar 2015
 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) aliyefuta uchaguzi 2015 na kupata umaarufu mkubwa, Jecha Salim Jecha leo amefariki Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam na mwili wake utapelekwa Zanzibar kwa maziko.

Jecha Salim Jecha alipata umaarufu mwaka 2015 baada ya kufuta matokeo ya uchaguzi Zanzibar. Zaidi soma Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

Aprili 17, 2018 Salim Jecha Salim aling'atuka rasmi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC) baada ya kuhudumu katika nafasi hiyo kuanzia Mei 4, 2013. Zaidi soma Hatimaye 'mtemi' Jecha Salim Jecha ang'atuka

Mwaka 2020, Jecha Salim Jecha alichukua fomu ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi(CCM), jambo ambalo lilizua utata ukizingatia mwaka 2015 alikuwa ni Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar yenye dhamana ya kusimamia chaguzi zote kisiwani humo. Zaidi soma Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC), Jecha Salim Jecha achukua fomu ya urais Zanzibar

Mola amsamehe makosa yake alipoteleza.

View attachment 2691725
Picha maarufu ya Jecha Salim Jecha enzi za uhai wake​
Innalillah wainna ilayhir rajiun. Namuomba ALLAH amsamehe pale alipoteleza na kuwanyima watu haki zao kwa kushinikizwa na watanganyika.
 
Back
Top Bottom