MAISHA YA WASIKUWA WAISLAM
Moto wenye nguvu na mateso yasiyoisha:Katika Surat An-Nisa (4:56), Allah anasema: “Hakika wale waliokataa ishara zetu, tutawachoma katika moto. Kila ngozi zao zitakapoungua tutawabadilishia ngozi nyingine, ili waonje adhabu.”Kunywa maji ya moto:Katika Surat Ibrahim (14:16-17), Qur’an inaeleza jinsi makafiri watakavyopatiwa maji ya moto: “Mbele yake kuna Jahannam, na atanyweshwa maji ya usaha. Atajaribu kuyanywa, lakini hataweza kuyameza, na kifo kitamfikia kutoka pande zote, lakini hatakufa. Na mbele yake kuna adhabu kali.”Vazi la Moto:Katika Surat Al-Hajj (22:19-20), Allah anasema: “Wale waliokufuru, watakatwa mavazi ya moto, na vichwani mwao yatamiminwa maji yanayochemka. Yatakayoyeyusha yaliyomo matumboni mwao na ngozi zao.”